Na. James K. Mwanamyoto-Arusha
Tarehe 11 Februari, 2023
Mhe. Jenista ametoa maelekezo
hayo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao kilichowashirikisha
wadau zaidi ya 1500 wa serikali mtandao nchini.
“Tumekubaliana mifumo yote ya TEHAMA
iliyojengwa na itakayojengwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao ni lazima iwe
endelevu ili iwe na tija kiutendaji hivyo taasisi zote za umma hazina budi
kutumia mifumo hiyo shirikishi ya TEHAMA,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa ni
lazima kwa kila taasisi ya umma kuhakikisha sheria na miongozo ya serikali mtandao
inazingatiwa wakati wa kusanifu mifumo ya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na kuomba
kibali Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ili kupata idhini ya kutengeneza
mifumo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.
Xavier Daudi amesema ofisi yake imejipanga kuhakikisha eGA inasimamia vema
matumizi ya TEHAMA katika taasisi za umma na inajenga mifumo jumuishi
inayowasiliana ili kurahisisha utendaji kazi katika utumishi wa Umma ikiwa ni
pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba amesema kuwa,
washiriki wa kikao kazi hicho wametoa maoni na mapendekezo ya namna ya
kuimarisha serikali mtandao na kushauri uboreshaji wa baadhi ya mifumo inayotoa
huduma kwa umma pamoja ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma mtandao, hivyo
mamlaka yake itahakikisha inayafanyia ushauri, maoni na mapendekezo
yaliyotolewa kwa lengo la kuboresha matumizi ya serikali mtandao nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao, Dkt. Jasmine Tiisekwa amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa agizo lake
la kuimarisha Serikali Mtandao nchini ikiwa ni pamoja na utashi wake wa kisiasa
wa kuijenga Tanzania kuwa ya kidijitali.
Kaulimbiu ya kikao kazi hicho
cha tatu cha Serikali Mtandao ni ‘Mifumo Jumuishi ya TEHAMA kwa Utoaji Bora wa
Huduma za Umma’.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na washiriki wa kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao wakati akifunga kikao
kazi hicho jijini Arusha kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Washiriki wa kikao kazi cha
tatu cha serikali mtandao wakisikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista (hayupo pichani)
wakati akifunga kikao kazi hicho jijini Arusha kilichoandaliwa na Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA).
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufunga kikao kazi cha
tatu cha serikali mtandao jijini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao, Dkt. Jasmine Tiisekwa akitoa neno
la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya waziri huyo kufunga kikao kazi
cha tatu cha serikali mtandao jijini Arusha kilichoandaliwa na Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba akieleza lengo la kikao kazi
cha tatu cha serikali mtandao kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kukifunga
kikao hicho jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TEHAMA
Serikalini Bw. Priscus Kiwango akieleza maazimio ya washiriki wa kikao kazi cha
tatu cha serikali mtandao kabla ya kikao kazi hicho kufungwa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa
katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kikao kazi cha tatu cha
serikali mtandao (waliosimama) na viongozi mara baada ya kukifunga rasmi kikao
kazi hicho jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment