Thursday, September 29, 2022

WAZIRI JENISTA AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA, MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALINI NA UWEZESHAJI WA KAYA MASKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan walipokutana jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo ya kuendeleza ushirikiano katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma, matumizi ya TEHAMA serikalini na uwezeshaji wa kaya maskini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan (hayupo pichani) alipokutana naye jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo ya kuendeleza ushirikiano katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma, matumizi ya TEHAMA serikalini na uwezeshaji wa kaya maskini.

Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan (kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipokutana jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo ya kuendeleza ushirikiano katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma, matumizi ya TEHAMA serikalini na uwezeshaji wa kaya maskini. Kushoto kwa Balozi ni Balozi Msaidizi, Mhe. Manoj Verma.


Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji akichangia hoja kwenye kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akichangia hoja kuhusu matumizi ya TEHAMA serikalini wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. 


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Dkt. Edith Rwiza akichangia hoja kuhusu masuala ya mafunzo kwa watumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akipokea zawadi toka kwa Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan kuashiria ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na India.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan (wa pili kulia), Balozi Msaidizi, Mhe. Manoj Verma (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji.


 

Wednesday, September 28, 2022

MHE NDEJEMBI AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWAHAMASISHA WANANACHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TASAF

 Na. Veronica Mwafisi - Maswa

Tarehe 28 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watendaji wa serikali kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya TASAF nchini, ukiwemo wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa ili kuunga mkono jitihada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuliletea taifa maendeleo.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo, mara baada ya kukagua ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Budekwa akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Kiloleli wilayani Maswa. 

Mhe. Ndejembi amesema, njia pekee ya watendaji wa serikali kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya TASAF ni kuwahamasisha wananchi kushiriki utekelezaji wake kuanzia ngazi ya kijiji, kata, tarafa hadi wilaya ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa kupeleka mradi huo wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Budekwa ili kuwalinda na kuwaepusha watoto wa kike na changamoto zinazokwamisha malengo yao katika elimu.

“Mwanafunzi anapoishi katika mazingira ya shule kutokana na uwepo wa bweni, itamsaidia fikra zake zote kuzielekeza katika masomo, na hilo ndio lengo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,” Mhe. Ndejembi amesema.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo    amesema Serikali imetekeleza wajibu wake kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo wa TASAF, hivyo wananchi wa Kijiji cha Kiloleli wanapaswa kuhakikisha wanashiriki kukamilisha mradi huo ili wanafunzi waweze kupata elimu bora.

Aidha, Bi. Kayombo amesema ujenzi wa bweni hilo ukikamilika utasaidia pia kupunguza changamoto ya uwepo wa mimba zisizotarajiwa kwa wanafunzi wa kike ambao baadhi yao hulazimika kukatisha masomo yao.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa bweni, Afisa Mtendaji wa Kata ya Budekwa, Bw. Masesa Madirisha amesema, mradi huo una faida kubwa katika kuboresha mazingira ya kusoma kwa watoto wa kike ambao wanapaswa kutimiza ndoto zao kama ilivyo kwa watoto wa kiume.

Kijiji cha Kiloleli ni miongoni mwa vijiji vitano vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambavyo vinatekeleza miradi ya kupunguza umaskini ya OPEC IV Awamu ya Kwanza.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wanafunzi na wananchi wa Kijiji cha Kiloleli wilayani Maswa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Budekwa unaotekelezwa na TASAF. 


Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa. 


Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Asengwe Kaminyoge (Wakwanza kulia) akitoa neno la utangulizi kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa Kijiji cha Kiloleli wilayani Maswa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Budekwa unaotekelezwa na TASAF. 



Mwonekano wa bweni la wasichana wa shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa, linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF kupitia miradi ya kupunguza umaskini –OPEC IV.

 


Tuesday, September 27, 2022

MHE. NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJITOA KIKAMILIFU KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI

 Na. Veronica E. Mwafisi-Meatu

Tarehe 27 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kujituma na kujitoa kikamilifu katika kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali kupitia taasisi zake.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.

Mhe. Ndejembi amesema, watumishi wa umma ni mabalozi wa serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, kujituma na kujitoa kwa ajili ya serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Mtumishi wa umma ni mwakilishi wa serikali mahali anapofanya kazi, hivyo hana budi kutambua kuwa serikali imemuajiri ili kuwatumikia wananchi kwa kuwapatia huduma bora kama ambavyo serikali imekusudia,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira mpya 104 katika Halmashauri hiyo zikiwemo kada za elimu na afya ili kuwahudumia wananchi wilayani humo.

Aidha, Bw. Msoleni ameishukuru ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutoa kipaumbele cha kuwapatia stahiki watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Naye, Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa kwa niaba ya watumishi wengine, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wake kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia ufafanuzi wa hoja za masuala ya kiutumishi walizoziwasilisha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi Mkoani Simiyu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.


Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.


Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa, akitoa taarifa ya utelezaji wa majukumu ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.


Mkuu wa Shule ya Kimali, Bw. Marco Ng’wendamunkono wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kushoto) akijibu hoja iliyokuwa imewasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo. Kulia Kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura na kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw.  Oscar Maduhu.

Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa  akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri  ya Wilaya ya Meatu.



SERIKALI KUPITIA TASAF YAJENGA BWENI KIJIJI CHA BUKUNDI KUONGEZA UFAULU WA WANAFUNZI NA KUWAEPUSHA NA MIMBA ZA UTOTONI

 Na. Veronica Mwafisi - Meatu

Tarehe 27 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imejenga bweni katika Shule ya Sekondari Bukundi iliyopo Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu, ili kuweka mazingira rafiki ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwaepusha na changamoto ya mimba za utotoni.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo, mara baada ya kukagua bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari Bukundi akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

Mhe. Ndejembi amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametafuta fedha hizo za TASAF na kujenga bweni hilo kwa ajili ya kutatua changamoto na adha zinazowakabili wanafunzi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu ili kuhudhuria masomo.

Kutokana na umuhimu wa bweni hilo, Mhe. Ndejembi ametoa mwenzi mmoja kwa viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa bweni hilo kushirikiana kikamilifu na TASAF ili likamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

“Bweni hili likikamilika kwa wakati litaongeza ufaulu na kusaidia kuondoa changamoto ya mimba za utotoni, kwani wanafunzi wataishi katika eneo hili la shule badala ya kwenda kuishi kwenye jamii ambayo ina changamoto nyingi,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, licha ya TASAF kuwezesha mradi wa bweni hilo lakini imejenga miradi ya maji, zahanati na vituo vya afya katika kipindi kifupi cha uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo amewataka wananchi wa Kijiji cha Bukundi kulinda miradi hiyo ili iwanufaishe wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.

“Sisi wananchi wa Bukundi tuna jukumu moja la kulinda miradi hii kwa manufaa yetu kwani serikali imetumia fedha nyingi kuitekeleza miradi hiyo,” Mhe. Ndejembi ameongeza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Bukundi ambalo litaboresha mazingira ya wanafunzi kusoma.

Mhe. Fauzia amesema, shule ambayo bweni hilo limejengwa ipo katika jamii ya wafugaji ambao wanaishi maeneo ya mbali na shule hiyo, kutokana na umbali huo watoto wengi walitamani kusoma lakini walishindwa kutokana na kutembea umbali mrefu, hivyo bweni hilo litasaidia kuondoa changamoto hiyo.

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu amewasisitiza wananchi wa Kijiji cha Bukundi kuilinda miundombinu ya bweni hilo kwani litawawezesha wanafunzi kupata elimu bora kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Bukundi wilayani Meatu, linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF litakuwa na uwezo wa kuwahudumia wanafunzi 80.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wanafunzi na wananchi wa Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Bukundi unaotekelezwa na TASAF wilayani humo.


Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukundi wilayani Meatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wapili kutoka kushoto) akizungumza jambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu (Wakwanza kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Bukundi wilayani Meatu. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe. Fauzia Ngatumbura.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia) akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Bukundi wilayani Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Bukundi wilayani humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura na wakwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Mhe. Prisca Kayombo. 


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu akitoa salamu za TASAF wilayani Meatu, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) yenye lengo la kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Bukundi wilayani humo.


Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu wakimsikiliza Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Bukundi wilayani humo.


Mwonekano wa bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari Bukundi wilayani Meatu, linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF.




Sunday, September 25, 2022

TAARIFA KWA UMMA


 

KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF YATAKIWA KUZITEMBELEA KAYA MASKINI ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZITAKAZOKWAMISHA LENGO LA SERIKALI LA KUBORESHA MAISHA YA KAYA MASKINI NCHINI

Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Tarehe 25 Septemba, 2022 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwa na utamaduni wa kuwatembelea walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF ili kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango huo ambao Serikali inautekeleza kwa lengo la kuboresha maisha ya kaya maskini nchini. 

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma, wakati akizindua Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyoteuliwa hivi karibuni mara baada ya kamati iliyopita kumaliza muda wake kiutendaji.  

Waziri Jenista amewahimiza wajumbe wa kamati hiyo, kuhakikisha wanakwenda kuzungumza na viongozi, waratibu na walengwa katika maeneo yote ambayo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa, ili kufikia lengo la Serikali la kuzikwamua kaya maskini kutoka katika lindi la umaskini. 

“Mhe. Mwenyekiti na wajumbe wa kamati hii, tembeleeni maeneo ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa ili mjiridhishe namna ambavyo unawafikia walengwa na kuwanufaisha,” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, wajumbe wa kamati wakitembelea maeneo ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa, watapata fursa ya kujionea namna walengwa walivyonufaika, ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ambazo walengwa hao wa TASAF wanakabiliana nazo. 

Akizungumzia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuzikwamua kaya maskini, Mhe. Jenista amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan haitomuacha mtu nyuma katika kufikia malengo ya maendeleo kama yalivyoainishwa katika dira ya maendeleo (Vision 2025), na ndio maana imejipanga vema katika kuhakikisha inaboresha maisha ya kaya zote maskini kwenye vijiji, mitaa na shehia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Ilomo amemhakikishia, Mhe. Jenista kuwa yeye pamoja na kamati yake watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa ili kutimiza lengo la serikali la kuboresha maisha ya kaya maskini. 

Naye, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dkt. Moses Kusiluka amesema, ataendelea kushirikiana na TASAF ili kuhakikisha inatimiza lengo lake la kuboresha maisha ya wananchi ambao wanaishi katika familia zenye hali duni kiuchumi.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, TASAF imekuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya kaya maskini ikiwa ni pamoja na kujenga rasilimaliwatu ya kutosha kwa kuwawezesha kielimu wanafunzi wanaotoka kwenye kaya maskini kutoka hatua moja kwenda nyingine.

“Mwaka jana, TASAF kwa kushirikiana na bodi ya mikopo tumewawezesha wanafunzi 1200 kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini, na mwaka huu mchakato bado unaendelea lakini tunatarajia kuwawezesha wengi zaidi kwani walioomba wako zaidi ya 3000,” Bw. Mwamanga amefafanua.

Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa sasa inaundwa na Mwenyekiti Bw. Peter Ilomo, pamoja na wajumbe wengine ambao ni Balozi Zuhura Bundala, Bw. Richard Shilamba, Dkt. Charles Mwamwaja, Dkt. Ruth Lugwisha, Dkt. Naftali Ng’ondi, Bw. Ali Salim Matta, Mhandisi Rogatus Mativila na Dkt. Grace Magembe. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF pamoja na watendaji wa TASAF, wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma. 




Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF na baadhi ya watendaji wa TASAF wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Bw. Peter Ilomo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na wajumbe wa kamati na watendaji wa TASAF wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma.



Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kuiongoza Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Dkt. Moses Kusiluka akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Jenista Mhagama na watendaji wa TASAF, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati mpya iliyoteuliwa hivi karibuni iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa taarifa ya utekelezaji na majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF uliofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi tuzo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kuiongoza Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Dkt. Moses Kusiluka ya kutambua mchango aliotuoa wakati wa uongozi wake. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa mjaukumu ya TASAF, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na   Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, mara baada ya kuizindua kamati hiyo jijini Dodoma.

 




Tuesday, September 20, 2022

WAAJIRIWA WAPYA 553 WA TAKUKURU WATAKIWA KUTUMIKIA MIAKA 5 BILA KUHAMIA TAASISI NYINGINE ILI KUTIMIZA LENGO LA MHE. RAIS LA KUTOKOMEZA RUSHWA NCHINI

 Na. James K. Mwanamyoto-Moshi

Tarehe 20 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuweka kipengere kwenye mkataba wa waajiriwa wapya 553 wa TAKURURU chenye sharti la kutumikia miaka mitano katika taasisi hiyo kabla ya kufikiria kuhamia taasisi nyingine ili kutimiza lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutokomeza vitendo vya rushwa nchini. 

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakati akifunga mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU, yaliyotolewa katika Shule ya Polisi Tanzani iliyopo Moshi ili kuwajengea uwezo wa kupambana na vitendo vya rushwa nchini.

Mhe. Ndejembi amesema, amelazimika kutoa maelekezo hayo ili kukomesha tabia iliyoibuka ya baadhi ya watu kuomba kazi yoyote inayotangazwa serikalini na pindi akiajiriwa anataka kuhamia taasisi nyingine kwa maslahi yake binafsi, wakati serikali imemuajiri ili kuutumikia umma wa watanzania katika taasisi aliyopangiwa.

“Ninaelekeza kwa ajira hizi 553 za TAKUKURU, kiwekwe kipengere kinachoainisha kuwa, ni lazima waitumikie TAKUKURU si chini ya miaka 5 bila kuhamia taasisi nyingine kwani serikali imewekeza kiasi kikubwa katika kuwapatia mafunzo na kuwaajiri, hivyo ni lazima muutumikie umma katika mapambano dhidi ya rushwa ili thamani ya fedha iliyowekezwa ionekane,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuichukia rushwa na hataki kuona maendeleo ya taifa yanakwamishwa na vitendo kwa rushwa, hivyo amewataka waajiriwa hao wapya wa TAKUKURU kuunga mkono kwa vitendo azma hiyo ya Mheshimiwa Rais.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amesema kuwa Mhe. Rais amefanya mengi mazuri ikiwa ni pamoja na kutoa ajira hizo 553 za TAKUKURU, ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini na amewataka watakaopangiwa kwenye mkoa wake wafanye kazi kwa bidii na uadilifu katika kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ambazo Mhe. Rais amezitoa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi mkoani Kilimanjaro.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni amesema waliohitimu mafunzo hayo watapangiwa vituo vya kazi na kuwataka kila mmoja akubali kituo atakachopangiwa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kupambana na rushwa.

“Sitarajii kuona vimemo vya kuniomba niwabadilishie vituo vya kazi kwani wakati mnaomba ajira na wakati mnafanya usaili tuliwauliza kama mko tayari kufanya kazi popote nchini, na kila mmoja wenu alisema kuwa yuko tayari kufanya kazi sehemu yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” ACP Hamduni amesisitiza.

Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea na jitihada za kuijengea uwezo kiutendaji Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuipatia rasilimaliwatu yenye tija katika kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini ambavyo vinakwamisha maendeleo ya taifa.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU kabla ya kufunga mafunzo hayo mjini Moshi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akikaribishwa kukagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU kabla ya kufunga mafunzo hayo mjini Moshi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akipokea heshima ya gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU wakati akifunga mafunzo hayo mjini Moshi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akishuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakionyeshwa na wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU (hawapo pichani) kabla ya kufunga mafunzo hayo mjini Moshi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Polisi Tanzania SACP Ramadhani Mungi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifunga mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.

 

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifunga mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.

Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akifunga mafunzo hayo mjini Moshi.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu akitoa salamu za mkoa wake kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kufunga mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU mjini Moshi. 


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akielezea lengo la mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania mjini Moshi kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kufunga mafunzo hayo.

 



 

Sunday, September 18, 2022

KAMATI YA USEMI YAELEKEZA UMILIKI WA HATI MILIKI ZA ARDHI ZA FAMILIA UWE WA AKINA MAMA NA BABA

 Na. James K. Mwanamyoto-Chamwino

Tarehe 18 Septemba, 2022

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo ameipongeza MKURABITA kwa kuwapatia Hati Miliki za Ardhi za Kimila wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino, na kuelekeza hati zote zinazohusisha familia pindi zinapoandaliwa umiliki wake uwe na majina ya akina mama pia badala ya majina ya akina baba pekee.

Mhe. Chaurembo ametoa maelekezo hayo akiwa katika Kijiji cha Manyemba wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake wilayani Chamwino, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani humo.

Mhe. Chaurembo amesema, MKURABITA licha ya kutekeleza vizuri wajibu  wa kujenga masijala na kuwapatia wananchi wa kijiji hicho hati miliki za ardhi, lakini wanapaswa kuzingatia kuwa hati zote za kifamilia umiliki wake uwe na majina ya akina mama na akina baba kwani wote wana haki sawa katika umiliki wa ardhi.

“Kama eneo ni la familia, baba na mama wanamiliki hakikisheni majina ya wote wawili yameandikwa kwenye hati, jina la mama liwepo na la baba liwepo kwani si dhambi kwa hati moja kuwa na jina zaidi ya moja, hivyo tunapaswa kujenga utamaduni wa akina mama nao wawe sehemu ya kumiliki ardhi,” Mhe. Chaurembo amesisitiza.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa, MKURABITA katika Kijiji cha Manyemba imefanya kazi kubwa sana ya kutoa hati zilizosaidia kutatua migogoro mingi ya umiliki wa ardhi.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, mara baada ya MKURABITA kuwezesha upimaji wa ardhi kwenye kijiji hicho, migogoro mingi na mikubwa ya ardhi imekwisha na kubaki changamoto ndogo ndogo zinazotatulika ambapo kipindi cha nyuma kulikuwa na migogoro mikubwa sana ya ardhi.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Manyemba aliyekabidhiwa hati ya kumiliki ardhi, Bw. Timothy Lesi ameishukuru MKURABITA kwa kuwapatia hati ambazo zitatatua migogoro ya ardhi inayotokana na wageni katika kijiji chao kuvamia ardhi za wenyeji jambo ambalo linahatarisha amani iliyopo.

Kwa upande wake, Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema uzinduzi wa jengo la masijala ni kiashiria cha wananchi wa Kijiji cha Manyemba kuwa karibu na maendeleo na kuongeza kuwa, mara baada ya MKURABITA kuwapimia mashamba wananchi wa kijiji hicho tayari wameshawapatia mafunzo kwa kushirikiana na benki ya NMB na CRDB ya namna gani wanaweza kutumia hati kupata mikopo.

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) umeendelea kuwa ni sehemu ya utatuzi wa migogoro mingi ya ardhi nchini hususani katika maeneo ya vijijini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (Mb) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake wilayani humo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA).


Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo wilayani humo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino, wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani humo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (Mb) akimkabidhi hati mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake wilayani humo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA). Anayeshuhudia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb).


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (Mb) akizindua jengo la masijala ya ardhi la Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake wilayani humo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA). Wengine ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi na Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe.


Mkurugenzi wa Urasimishaji MKURABITA, Bi. Jane Lyimo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya MKURABITA kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo katika Kijiji cha Manyemba wilayani Chamino iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA.


Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe akieleza manufaa ya utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) katika Kijiji cha Mayemba wilayani Chamwino, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhitimisha ziara ya kikazi wilayani Chamwino.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati yake pamoja na wananchi wa Kijiji cha Manyemba wilayani Chamwino waliokabidhiwa hati, mara baada ya kamati yake kuhitimisha ziara ya kikazi wilayani humo iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA.