Monday, October 19, 2015

WAANDISHI WA HABARI NCHINI WAPATA FURSA KUSHIRIKI MKUTANO KWA NJIA YA VIDEO ULIORATIBIWA NA WAKALA YA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO Ukitaka kujua namna wakala hiyo inavofanya kazi tembelea tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi (www.utumishi.go.tz) na bofya taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na TaGLA....

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia),  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. Florence Temba (katikati) na Mratibu wa Mafunzo wa TaGLA Bw. Dickson Mwanyika (kushoto) wakishiriki mkutano kwa njia ya video (Video Conference) uliofanyika kwa kushirikiana na Kenya School of Government. Wengine ni Waandishi wa Habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia)  akifafanua jambo kwa  Waandishi wa Habari namna ofisi yake inavyoratibu uendeshaji wa mikutano kwa njia ya video (Video Conference). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. Florence Temba.

Thursday, October 1, 2015

MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS-UTUMISHI MHE. CELINA O. KOMBANI (MB) WAPUMZISHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE.......

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akisoma wasifu wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa Ibada ya kuuga mwili wake iliyofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma (kulia) ukiwa mbele ya wafiwa wakati wa Ibada ya kuuga iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Baadhi ya waombolezaji wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. 

Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Ghalib Bilali (wa tano kutoka kulia) akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa nne kutoka kulia) wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. 

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma.