Thursday, February 26, 2015

Baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kwa kuunganisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Kilimanjaro  na Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara,Lindi, Kilimanjaro na Dodoma.  

Maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara,Lindi, Kilimanjaro na Dodoma. Uendeshaji wa vikao kwa njia ya mtandao umepunguza gharama na muda uliokuwa unatumika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Friday, February 13, 2015

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliokuja kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini. 

Sehemu ya wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliokuja nchini kutoa huduma kwa kujitolea katika maeneo mbalimbali wakitoka nje ya Ofisi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha nchini.

Wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani wakipiga makofi kumshukuru Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi mara baada ya kuwakaribisha nchini kufanya kazi sekta mbalimbali.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (katika kiti kikubwa) akiongea na wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliomtembelea ofisini kwake kujitambulisha.

Wednesday, February 4, 2015

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiagana na ujumbe kutoka Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Bw. Klaus Liepert (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake.

Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation  Tanzania Bi.  Julia Berger (wa pili kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mkuu wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na kanda ya Sahara Bw. Klaus Liepert akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Mkuu wa Afrika na Kanda ya Sahara  Bw. Klaus Liepert.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation Bi.  Julia Berger (wa kwanza kulia) na Bw. Claus Liepert (wa pili kulia).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwakaribisha ofisini kwake  Mkuu wa Taasisi ya Ujerumani iitwayo Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na ukanda wa Sahara Bw. Klaus Liepert (wa pili kushoto) pamja na mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo hapa Tanzania Bi. Julia Berger (wa kwanza kushoto).