Thursday, April 30, 2026
Tuesday, April 28, 2026
KIKAO KAZI CHA MAAFISA BAJETI KUTOKA OFISI YA RAIS, -UTUMISHI KWA KILICHOLENGA KUKAMILISHA MPANGO MKAKATI WA OFISI HIYO
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas
Ngangaji (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Bajeti kutoka Ofisi hiyo kwa
ajili ya hatua za kukamilisha Mpango Mkakati wa Ofisi hiyo kilichofanyika
kuanzia tarehe 28 Aprili-2 May, 2026 katika Ukumbi wa Ofisi ya Idara ya
kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Washiriki wa kikao kazi cha
Maafisa Bajeti kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kilicholenga kukamilisha Mpango Mkakati
wa Ofisi hiyo, wakiwa wanafuatilia Mafunzo katika Ukumbi wa Ofisi ya Idara ya
kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Washiriki wa kikao kazi cha
Maafisa Bajeti kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kilicholenga kukamilisha Mpango Mkakati
wa Ofisi hiyo, wakiwa wanafuatilia Mafunzo katika Ukumbi wa Ofisi ya Idara ya
kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Monday, April 27, 2026
WATUMISHI WALIOZALIWA MWEZI APRILI WAPONGEZWA
Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe
27 Aprili, 2026
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Ofisi hiyo Bi. Mwanaamani Mtoo niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI amewapongeza na kuwatakia kila la kheri watumishi wawote waliozaliwa mwezi Aprili ambapo kwa kumbukizi hiyo wamepata nafasi ya kukata keki kama ishara ya kuendeleza umoja na mshikamano ili kuimarisha utendaji kazi.
Matukio mbalilmbali ya picha za watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, waliokuwa wanaadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa ya mwezi Aprili, yaliyofanyika katika Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma
MKURUGENZI OFISI YA RAIS UTUMISHI AAGWA RASMI
Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe
27 Aprili, 2026
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda kwa niaba ya
Katibu Mkuu na Watumishi wote wa Ofisi hiyo amemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa
ambaye amestaafu kwa kwa mujibu wa Sheria.
Bw. Kipanda ameyasema hayo Aprili 27, 2026 katika eneo maalum
la mafunzo lililopo katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi itamkumbuka Mkurugenzi huyo
kwa upendo wake, umahiri, ujasiri, mchango na kazi nzuri aliyoifanya ya kuleta
tija katika utumishi wa Umma.
Kwa upande wake, Bi. Mwanilwa amewaasa watumishi hao kufanya
kazi kwa umoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili
kutoa huduma kwa haki na usawa.
Bi. Mwanilwa aliwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa
kujituma huku wakizingatia maadili ya utendaji ili kuufikia mwisho mwema wa
utumishi wao.
Wakurugenzi
wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma wakimkabidhi kwa niaba ya Katibu Mkuu –UTUMISHI keki aliyekuwa Mkurugenzi
wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa
(wanne kutoka kulia) ambaye amestaafu, utumishi wake kwa mjibu wa sheria, kama
ishara ya kumshukuru kwa mchango wake chanya katika Ofisi hiyo na kumtakia
maisha mema anapohitimisha utumishi wake.
Maafisa wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI waliowahi kufanya kazi na Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na
Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa wakipata picha ya pamoja na
Mkurugenzi huyo mara baada ya kumuaga rasmi katika eneo la Ofisi hiyo lililopo
Mtumba jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na
Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha
keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na
watumishi hao, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Leila Mavika (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi zawadi aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) mara baada ya Mkurugenzi huyo kufikia ukomo wa Utumishi wake kwa mujibu wa sheria .
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda (kushoto) akisisitiza
jambo kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na
Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (wa pili kutoka kushoto) wakati wa
alipokuwa akiagwa rasmi katika eneo maalumu la mafunzo la Ofisi hiyo lililopo
Mtumba jijini Dodoma. Wa pili na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI
na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Ofisi hiyo Bi. Mwanaamani Mtoo
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu Ofisi Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa akifurahia jambo wakati alipokuwa akitoa neno la kuwaaga watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 katika eneo maalumu la mafunzo lililopo katika Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda (kushoto) akitoa neno la shukrani pamoja na kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (aliyesimama katikati) katika eneo maalumu la mafunzo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kwa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na
Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha
keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na
watumishi hao, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na watumishi wa Ofisi hiyo, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma.
MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI KWA WATUMISHI WA UMMA KUONGEZA UFANISI
Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 27 Aprili, 2026
Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bi. Leila Mavika amesema mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa
watumishi wa umma ni muhimu kwa kuwa yanaongeza uelewa wa kutambua, kuchambua na
kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi wa shughuli za Serikali.
Bi. Mavika
ameyasema hayo Aprili 27, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw.
Juma Mkomi katika kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi
hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Bi. Mavika meongeza
kuwa, kutokana na uelewa ambao umepatikana wakati wa mafunzo hayo ni imani yake
kuwa kila mtumishi wa ofisi hiyo atakuwa na uwezo wa kuchambua na kutambua vihatarishi
vilivyopo katika eneo lake la kazi na kuvidhibiti kabla ya madhara kutokea.
Awali,
Afisa Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando amesema, Serikali
imeweka msisitizo kwa Wizara na Taasisi za umma kuimarisha mifumo ya udhibiti
wa vihatarishi ili kuboresha uwajibikaji.
Vilevile Bi. Lugando alitoa wito kwa watumishi wa kila Idara na vitengo kuhakikishe wanatambua vihatarishi vinavyoweza kutokea katika Idara na vitengo vyao ili kuimarisha usalama.
Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bi. Leila Mavika akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo
pichani) wakati mkurugenzi huyo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa kiutendaji watumishi hao katika eneo maalumu lla Ofisi hiyo ililopo Mtumba
jijini Dodoma.
Viongozi na watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia
mafunzo yaliyokuwa yakitolewa katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma
na mwezeshaji kutoka Wizara ya fedha Bi. Adolphina Lugando (hayupo pichani) kuhusu kutambua,
kuchambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi kwa lengo
la kuwajengea uelewa watumishi hao.
Afisa
Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando akitoa mafunzo ya
uelewa kuhusu usimamizi wa vihatarishi kwa watumishi wa umma wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora (hawapo pichani) yaliyofanyika
katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijin i Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya uelewa leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatun ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijin i Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma
Sunday, April 26, 2026
Wednesday, April 22, 2026
NAIBU KATIBU MKUU,OFISI YA RAIS-UTUMISHI BW. XAVIER DAUDI AKUTANA NA VIONGOZI WA JICA KWA MAZUNGUMZO
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma. Viongozi hao wamemtambulisha Mwakilishi Mkuu Mpya Bw.Kuge Katsuya baada ya Bw.Ara Hitoshi kumaliza muda wake.
Tuesday, April 21, 2026
WATUMISHI WA UMMA WASISITIZWA KUSHUGHULIKIA MREJESHO WA WANANCHI KWA HAKI NA KWA WAKATI
Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe
21 Aprili, 2026
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli amewasisitiza Watumishi wa Umma kushughulikia kwa haki na kwa wakati mrejesho unaowasilishwa na wananchi kupitia Mfumo wa (e- Mrejesho) ili kujenga imani na heshima ya Serikali kwa umma.
Bi. Shuli ameyasema hayo leo
Aprili 21, 2026 wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika
ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi
zilizo chini yake.
“Ili kufikia utumishi wa umma unaowajibika
na uliotukuka, ni vizuri tukashughulikia mrejesho wa wananchi kwa haki na
uharaka zaidi.” Bi Shuli alisema.
Amesema, Watumishi wa Umma
wanapaswa kuwa na mabadiliko katika fikra, mitazamo, mifumo na tabia walizonazo
ili kuwa na Utumishi wa Umma wenye matokeo chanya na thamani halisi kwa mwananchi.
Bi Shuli ameongeza kuwa uzingatiaji
wa maadili katika utumishi wa umma si kuzifuata tu Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo ya Utumishi wa Umma bali ni pamoja na kuutumia ipasavyo utaalamu unaohusu
ushughulikiaji wa mrejesho wa wananchi .
Amesema ni jukumu la kila
mshiriki kuonesha ushirikiano na kuzingatia utu hususani wanapotoa huduma kwa
wateja pamoja na kuwa waaminifu hasa katika utunzaji siri kwa kuwa kazi
watakazofanya zitahitaji kuwa na matumizi sahihi ya taarifa.
Aidha, amewapongeza washiriki
wote kwa kuhudhuria mafunzo hayo na kuwataka wajifunze kwa bidii ili wawe
wataalamu watakaowajibika kikamilifu
Kwa upande wake mwenyekiti wa
kikao hicho ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka Watumishi Housing Investiments (WHI) Bw.
Albano Lukiano amemshukuru Bi. Shuli kwa
kuwafungulia mafunzo hayo na kuahidi kuwa yale yote watakayofundishwa watayazingatia
na kuyafanyia kazi ili kutoa huduma bora kwa manufaa ya umma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister (kushoto)
akiteta jambo na Mwenyekiti wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho
ambaye pia ni Afisa TEHAMA kutoka Watumishi Housing Investiments (WHI) Bw.
Albano Lukiano (kulia) kabla ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli (aliyekaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea
na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi mara
baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli
(kushoto) akifurahia jambo mara baada
ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya kutumia Mfumo wa e-Mrejesho
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Maadili wa Ofisi hiyo Bi. Janet Mishinga
Afisa
tawala kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Bi. Semeni Muyabhaga akiwasilisha mada ya Uwasilishwaji wa Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi kwa kutumia Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Aprili 21, 2026 katika ukumbi wa
Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kikao cha mafunzo ya kutumia Mfumo wa e-Mrejesho Bw. Albano Lukiano akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.
Afisa
Rasilimaliwatu Mwandamizi Kutoka Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Hassan Kilenza akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mjadala
wa hoja mbalimbali kuhusu matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Washiriki
wa mafunzo ya matumizi ya kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko,
mapendekezo, maulizo na pongezi kwa watumishi wakifuatilia hotuba ya mgeni
Rasmi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 21, 2026
jijini Dodoma.
Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Stella Teri akiwasilisha mada kuhusu uzingatiaji wa Kanuni za Maadili ya Utendeji kwa watumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Mrejesho yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma
Afisa
rasilimali watu mwaandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Bi. Saada Ibrahim akiwasilisha mada ya Mwngozo wa Ushughulikiaji wa Mrejesho katika Utumishi wa Umma katika mafunzo ya matumizi ya Mfumo huo yaliyofanyika Aprili 21, 2026 katika ukumbi wa Ofisi
ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Jijini Dodoma.


