Monday, April 27, 2026

MKURUGENZI OFISI YA RAIS UTUMISHI AAGWA RASMI

 Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 27 Aprili, 2026

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda kwa niaba ya Katibu Mkuu na Watumishi wote wa Ofisi hiyo amemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa ambaye amestaafu kwa kwa mujibu wa Sheria.

Bw. Kipanda ameyasema hayo Aprili 27, 2026 katika eneo maalum la mafunzo lililopo katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi itamkumbuka Mkurugenzi huyo kwa upendo wake, umahiri, ujasiri, mchango na kazi nzuri aliyoifanya ya kuleta tija katika utumishi wa Umma.

Kwa upande wake, Bi. Mwanilwa amewaasa watumishi hao kufanya kazi kwa umoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kutoa huduma kwa haki na usawa.

Bi. Mwanilwa aliwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujituma huku wakizingatia maadili ya utendaji ili kuufikia mwisho mwema wa utumishi wao.


Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimkabidhi kwa niaba ya Katibu Mkuu –UTUMISHI keki aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (wanne kutoka kulia) ambaye amestaafu, utumishi wake kwa mjibu wa sheria, kama ishara ya kumshukuru kwa mchango wake chanya katika Ofisi hiyo na kumtakia maisha mema anapohitimisha utumishi wake.


Maafisa wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI waliowahi kufanya kazi na Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa wakipata picha ya pamoja na Mkurugenzi huyo mara baada ya kumuaga rasmi katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma



Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na watumishi hao, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma



Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI , Menejimenti na watumishi wote wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi chote alipokuwa Ofisini hapo mara baada ya Mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Leila Mavika (kulia) akikabidhi  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi zawadi  aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) mara baada ya Mkurugenzi huyo kufikia ukomo wa Utumishi wake kwa mujibu wa sheria .


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda (kushoto) akisisitiza jambo kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (wa pili kutoka kushoto) wakati wa alipokuwa akiagwa rasmi katika eneo maalumu la mafunzo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma. Wa pili na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Ofisi hiyo Bi. Mwanaamani Mtoo

Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu Ofisi Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa akifurahia jambo wakati alipokuwa akitoa neno la kuwaaga watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 katika eneo maalumu la mafunzo lililopo katika Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma  

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda (kushoto) akitoa neno la shukrani pamoja na kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa (aliyesimama katikati) katika eneo maalumu la mafunzo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kwa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika 



Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na watumishi hao, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma



Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mariam Mwanilwa (kushoto) akimlisha keki Afisa wa Ofisi hiyo kama ishara ya umoja na mshikamano kati yake na watumishi wa Ofisi hiyo, mara baada ya mkurugenzi huyo kuagwa rasmi katika Ofisi hiyo Aprili 27, 2026 jijini Dodoma.

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment