Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 27 Aprili, 2026
Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bi. Leila Mavika amesema mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa
watumishi wa umma ni muhimu kwa kuwa yanaongeza uelewa wa kutambua, kuchambua na
kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi wa shughuli za Serikali.
Bi. Mavika
ameyasema hayo Aprili 27, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw.
Juma Mkomi katika kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi
hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Bi. Mavika meongeza
kuwa, kutokana na uelewa ambao umepatikana wakati wa mafunzo hayo ni imani yake
kuwa kila mtumishi wa ofisi hiyo atakuwa na uwezo wa kuchambua na kutambua vihatarishi
vilivyopo katika eneo lake la kazi na kuvidhibiti kabla ya madhara kutokea.
Awali,
Afisa Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando amesema, Serikali
imeweka msisitizo kwa Wizara na Taasisi za umma kuimarisha mifumo ya udhibiti
wa vihatarishi ili kuboresha uwajibikaji.
Vilevile Bi. Lugando alitoa wito kwa watumishi wa kila Idara na vitengo kuhakikishe wanatambua vihatarishi vinavyoweza kutokea katika Idara na vitengo vyao ili kuimarisha usalama.
Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bi. Leila Mavika akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo
pichani) wakati mkurugenzi huyo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa kiutendaji watumishi hao katika eneo maalumu lla Ofisi hiyo ililopo Mtumba
jijini Dodoma.
Viongozi na watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia
mafunzo yaliyokuwa yakitolewa katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma
na mwezeshaji kutoka Wizara ya fedha Bi. Adolphina Lugando (hayupo pichani) kuhusu kutambua,
kuchambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi kwa lengo
la kuwajengea uelewa watumishi hao.
Afisa
Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando akitoa mafunzo ya
uelewa kuhusu usimamizi wa vihatarishi kwa watumishi wa umma wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora (hawapo pichani) yaliyofanyika
katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijin i Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya uelewa leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatun ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijin i Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando leo Aprili 27, 2026 ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment