Sunday, May 31, 2026

RIDHIWANI: SERIKALI YALIPA ZAIDI YA BILIONI 24 MADAI YA WATUMISHI AONYA WATUMISHI WANAOGHUSHI BARUA ZA UHAMISHO, ASEMA 6 MBARONI KESI UHUJUMU UCHUMI

Na. Jawadu Kinyobwa


Serikali imeendelea kuboresha ustawi wa watumishi wa umma kwa kulipa malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya Tsh. Bilipni 24,699,256,645.7 na kulipa watumishi 1,249 waliokoma utumishi yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 5,548,386,177.90.


Hayo yamebainishwa Juni Mosi, 2026 Mabele Hall jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa.


Pamoja na maboresho hayo, Mhe. Ridhiwani amesema  wapo baadhi ya waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo wajibu wao katika kushughulikia madai ya aina hiyo ambapo hadi kufikia Mei 28,2026 madai ya watumishi 18,021 yenye jumla ya Shilingi 50,917,523,216 hayajawasilishwa Ofisini kwake.


“Baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwasilisha katika Ofisi hii madai yenye kasoro ambazo walipaswa kuzibaini kabla hawajayawasilishwa.  Vile vile, yapo madai ya malimbikizo ya mshahara yanayotokana na waajiri kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika uendeshaji wa mashauri ya kinidhamu na hivyo kuzalisha madeni makubwa kwa Serikali” amesema.


Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani ametoa onyo kali kwa waajiri na viongozi wa taasisi za umma wanaokiuka sheria na taratibu za kiutumishi hususani kwa Waajiri kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi, kutopokea watumishi wanaohamishiwa kwenye Taasisi zao, Waajiri kujimilikisha Taasisi na kuficha barua zenye maelekezo mahsusi ikiwemo barua za uhamisho.


Sambamba hayo, amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na Taasisi za Haki Jinai imeanza kuchukua hatua mbalimbali kwa watumishi wanaojihusisha na ukiukwaji wa maadili ikiwemo kughushi barua za Ofisi hiyo ambapo hadi sasa jumla ya watuhumiwa Sita wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya Uhujumu Uchumi na kesi zinaendelea.


Awali akizungumza Katibu Mkuu Ofisi hiyo Juma Mkomi, amesema kikao hicho kimeandaliwa mahsusi kwa lengo la kutathmini nafasi ya wasimamizi wa Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, kubadilishana uzoefu katika kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali hususan katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma hasa tunapoelekea kwenye utekelezaji wa Dira Mpya ya Taifa ya 2050.


Pia, Mkomi  amesema kikao hicho kitajikita  zaidi katika kujadili masuala muhimu ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma, Usimamizi  na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA Serikalini, changamoto zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na namna bora ya kukabiliana nazo.


Kikao kazi hicho kina kauli mbiu isemayo “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Sikivu, Jumuishi, Wenye Matokeo na Uwajibikaji kuelekea Dira 2050”.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza   na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu  (hawapo pichani) katika ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu,Ofisi ya Raia-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi, akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa kilichofanyika Juni 1, Jijini Dodoma.



Sehemu ya Viongozi na Watendaji kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete wakati alipokuwa akizungumza nao katika  wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma 


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akitoa utambulisho wa viongozi na washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kabla ya ufunguzi wa kikao hicho Juni 1, 2026 Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (kulia ) akiteta jambo na Katibu Mkuu-UTUMISHI  Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa kilichofanyika Juni 1, Jijini Dodoma. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya Waziri huyo kufungua 
kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma

Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza   na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu  (hawapo pichani) katika ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete (mwenye suti ya kijivu ) akifurahia jambo na viongozi wengine kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, mara baada ya Wazuri huyo kufungua kikao kazi kilichofanyika Juni 1, 2026 katika ukumbi wa Mabele Hall jijini Dodoma. 

Wednesday, May 27, 2026

KATIBU MKUU-UTUMISHI AWAITA DODOMA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SERIKALINI.

Na Antonia Mbwambo na Eric Amani-Dodoma

Tarehe 26 Mei, 2026

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,   Bw. Juma Mkomi, amewasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kushiriki kikao kazi muhimu kilichopangwa kufanyika tarehe 1-3 Juni, 2026 katika ukumbi wa mabele hall jijini Dodoma.

Bw. Mkomi ametoa msisitizo huo Mei 26, 2026 wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI uliopo Mtumba jijini Dodoma

“Natoa wito kwa Wakuu wa Idara na vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhudhuria wao wenyewe katika kikao hicho bila kukosa kwakuwa kikao hiki kitakuwa na maelekezo mahususi ya kuboresha utendaji kazi.” Bw. Mkomi alisema.

Aidha, Bw. Mkomi amebainisha kuwa kikao hicho kitajadili na kufafanua kuhusu matumizi ya Mifumo mbalimbali ya kidijiti ikiwemo e-uhamisho, e-watumishi, e-utendaji, e-mrejesho na hr-assesment kwa kuzingatia shabaha za vipaumbele vya Taifa kuelekea dira 2050.

Ameongeza kuwa kikao hicho kitatoa nafasi ya kujadili kuhusu changamoto na mafanikio yaliyopo katika utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu na mapendekezo ya namna bora ya kuzishughulikia changamoto hizo. Pia washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuimarisha utendaji kazi katika Taasisi za Umma.

Bw. Mkomi amewataka washiriki kujisajili katika mfumo kupitia link ya tsms.gov.go.tz huku wakizingatia kwamba mwisho wa usajili ni tarehe 29 Juni, 2026.

Vile vile, Wakuu wa Idara na vitengo vya Usimamizi wa Rasilimaliwatu wamesisitizwa kufika katika ukumbi wa Mabele Hall uliopo jijini Dodoma tarehe 31 Mei, 2026 kuanzia saa 4 asubuhi kwa ajili ya kuchukua vitambulisho vyao vitakavyotumika katika kikao hicho.Kikao kazi hicho kitaongozwa na kauli mbiu isemayo; “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ulio Sikivu, Jumuishi wenye Matokeo na Uwajibikaji kuelekea Dira 2050”.

Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha habari cha ITV Ndg. Michael Msilo akimuuliza swali katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kwenye mkutano na waandishi hao leo Mei 26, 2026 juu ya Kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara, Idara zinazojitegemea pamoja na Wakala wa serikali za Mtaa kinachotarajiwa kufanyika Juni 1 hadi 3 jijini Dodoma


Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (Katikati) wakati walipohudhuria mkutano wa waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi hiyo uliyopo Mtumba Jijini Dodoma Mei 26, 2026




Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha habari cha BBC Ndg. Ronald Sonyo akimuuliza swali katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kwenye mkutano na waandishi hao leo Mei 26, 2026 juu ya Kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara, Idara zinazojitegemea pamoja na Wakala wa serikali za Mtaa kinachotarajiwa kufanyika Juni 1 hadi 3 jijini Dodoma  


Baadhi ya Wakurugenzi Wakuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi hiyo leo Mei 26, 2026 Mtumba, Dodoma.




Tuesday, May 26, 2026

HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA

 


KATIBU MKUU MKOMI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA NA UHUSIANO MZURI KAZINI NA NJE YA KAZI

 Na Eric Amani. Mtumba-Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amewataka watumishi wa umma kujenga na kudumisha uhusiano mzuri katika maeneo yao ya kazi na nje ya kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, kuimarisha mshikamano na kujenga taswira nzuri ya Utumishi wa Umma kwa jamii.

Akizungumza leo Mei 25, 2026 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mkomi amesema kuwa mazingira mazuri ya kazi hujengwa kupitia ushirikiano, kuheshimiana, mawasiliano bora na kuthaminiana miongoni mwa watumishi.

“Watumishi wa Umma tunapaswa kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kuzingatia maadili, nidhamu na kujenga mahusiano chanya siyo tu ofisini bali hata nje ya maeneo ya kazi. Umoja wetu una mchango mkubwa katika kuongeza tija na ubora wa huduma tunazozitoa kwa Umma,” amesema Bw. Mkomi.

Aidha, amewapongeza watumishi kwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ya kila Jumatatu ambayo yamekuwa yakisaidia kuongeza uelewa, kuimarisha utendaji kazi na kujenga ari mpya ya kuwahudumia wananchi kwa weledi na uwajibikaji mkubwa zaidi.

Katibu Mkuu Mkomi pia amewataka watumishi kuendelea kushikamana, kusaidiana na kudumisha heshima baina yao ili kuifanya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma bora Serikalini.

Mafunzo hayo hutolewa kila siku ya Jumatatu katika eneo la Ofisi hiyo Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji, maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akitoa neno kwa watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao Mei 25, 2026 Mtumba, Jijini Dodoma.

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Ummma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi( Wa kwanza Kulia)  akiwa na Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mei 25, 2026 wakimsikiliza mwezeshaji SACP Ibrahim Mahumi (Hayupo kwenye Picha) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayofanyika kila jumatatu katika eneo la Ofisi hiyo Mtumba, Dodoma. 

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma SACP. Ibrahim Mahumi akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI Mei 25, 2025 Mtumba, Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi (Aliyevaa Suti ya Blue) akiwa pamoja na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Ummma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi (watatu kutokea kushoto) wakimsikiliza mwezeshaji (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo. 

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakisikiliza mafunzo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) Mei 25, 2026 katika eneo la ofisi hiyo iliyopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.







Monday, May 18, 2026

UWEKEZAJI WA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI KUONGEZA UFANISI NA UWAZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA

 Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 18/05/2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema uwekezaji wa matumizi ya Mifumo ya Tehama Serikalini utasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ufanisi na Uwazi wa huduma zinazotolewa na Watumishi wa umma kwa wananchi kwa maslahi ya Taifa

Mhe. Qwaray ameyasema hayo Mei 18, 2026 wakati akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC), Menejimenti pamoja na Watumishi kutoka Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Kituo hicho Jijini Dodoma.

“Ni lazima tufahamu kwamba, katika dunia ya sasa, mageuzi ya kidijiti si chaguo tena bali ni msingi wa ufanisi wa Serikali, ushindani wa kiuchumi na maendeleo ya kijamii”. Mhe. Qwaray alisema.

Amesema,Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, kupunguza urasimu na rushwa, kuongeza uwazi, na kurahisisha upatikanaji wa huduma za wananchi popote walipo.

Mhe.Qwaray ameongeza kuwa, Serikali imepata mafanikio makubwa katika matumizi ya mifumo ya Kidijiti katika Sekta mbalimbali ikiwemo kuongeza uwajibikaji, kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuboresha utendaji kazi wa Utumishi wa Umma.

Aidha, Mhe Qwaray amesema kituo hicho kimekuwa na mchango chanya katika matumizi ya Mifumo mbalimbali kama vile Mfumo wa kielektroniki unaoiwezesha Serikali kupokea na kushughulikia malalamiko, maoni, pongezi, na maulizo kutoka kwa wananchi kwenda kwenye taasisi zote za umma (e-Mrejesho) pamoja na Mfumo wa Dirisha la Huduma za Serikali ikiwemo tangazo la Gazeti la Serikali na Utoaji wa Vibali vya Likizo bila Malipo.

Mhe. Qwaray ametoa wito kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Vyuo Vikuu, taasisi za tafiti pamoja na Sekta Binafsi ili tafiti zinazofanyika ziweze kutatua changamoto halisi za wananchi na taasisi za umma.

Vilevile ameitaka Taasisi hiyo kusimamia utekelezaji wa Sheria, Kanuni, na Miongozo ya Serikali Mtandao ili mifumo yote inayotengenezwa iwe salama, yenye kuwasiliana na mifumo mingine na kuleta tija kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)   Mhandisi Benedict Ndomba, amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ilianzisha Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (e-GOVRIDC) kwa lengo la kuratibu shughuli za kitafiti, kubuni na kuendeleza jitihada za Serikali Mtandao, ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa umma, kuwajengea uwezo na kukuza vipaji vya vijana wabunifu katika eneo la TEHAMA.

Mhandisi Ndomba amemshukuru Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kwa kuitikia wito wa kutembelea kituo hicho na kuahidi kwamba wameyapokea na wataenda kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi huyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo Jijini Dodoma.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akikaribishwa na viongozi wa kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) mara baada ya kuwasili Kituoni  hapo Jijini Dodoma.

wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na viongozi, na Watumishi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC), mara baada ya kuwasili na kutembelea miradi mbalimbali ya kituo hicho Mei 18, 2026 jijini Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) katika ziara ya kikazi kituoni hapo Jijini Dodoma.



Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) Jijini Dodoma

Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) Jijini Dodoma.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)   Mhandisi Benedict Ndomba akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kabla Naibu Waziri huyo kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma.


Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)   Mhandisi Benedict Ndomba  (hayupo pichani) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuhusu utendaji wa kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC)   kilichopo Jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (aliyeka katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza nao katika ziara ya kutembelea kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) Jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya kuzungumza nao alipokuwa katika ziara ya kutembelea kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) Jijini Dodoma


Friday, May 15, 2026

WAZIRI RIDHIWANI ASISITIZA UADILIFU, NIDHAMU WAHITIMU TAASISI YA UONGOZI

Na. Jawadu Kinyobwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Wahitimu wa Taasisi ya Uongozi kuwa waadilifu, wenye nidhamu na uthubutu ili kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Mei 15, 2026 katika Sherehe ya Tisa ya Mahafali ya Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika Mlimani City, Jijini Dar es salaam.

Aidha, amesema katika ulimwengu wa sasa uadilifu ndio sifa kuu ya kiongozi bora na mwenye kuaminika, hivyo watumie maarifa na ujuzi walioupata chuoni kuwa viongozi wanaozingatia haki, uwajibikaji na weledi katika kila jambo.

“Nawakumbusha umuhimu wa kuwa Viongozi Wenye Uzalendo. Tukumbuke msemo wa wahenga: Adhabu ya msaliti ni malipo ya usaliti wake. Usaliti mkubwa katika uongozi wa umma ni sawa na ubadhirifu wa mali za Umma” amesema.

Akizungumza kuhusu umuhimu wa uadilifu katika uongozi, amewasihi wahitimu hao kuwa viongozi wenye maadili mema, wanaolinda mali za umma na kuweka mbele maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Amesema Taifa linahitaji viongozi waaminifu, wenye uwajibikaji na wanaotumia nafasi zao kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya Watanzania wote.

Sambamba na hayo, Mhe. Ridhiwani amesisitiza kuwa, uongozi bora na wa kuzingatia misingi ya haki na uwazi utasaidia kuendelea kuitangaza vyema Tanzania pamoja na Taasisi ya Uongozi ndani na nje ya nchi.

Awali akizungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo, amesema Taasisi hiyo imetimiza miaka kumi na tano tangu ilipoanzishwa rasmi Julai 2010 kwa Hati ya Rais kama Kituo cha Utaalamu wa Hali ya Juu (Centre of Excellence) cha kujenga na kuimarisha viongozi barani Afrika ili kuleta maendeleo endelevu.

Amebainisha kuwa, Taasisi hiyo imeendelea kufanya kazi kubwa na nzuri katika utoaji wa programu za mafunzo ya uongozi, uandaaji wa mijadala ya kisera, upanuzi wa dimbwi la maarifa kupitia tafiti na machapisho mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Juma Burhan Mohamed amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika fikra, uwezo wa uongozi na namna ya kufanya maamuzi yenye tija kwa taasisi na jamii.

Amesema mahafali hayo hayakuwa tu sherehe ya kukamilisha mafunzo, bali yalikuwa ishara ya mabadiliko na ukuaji wa kiuongozi walioupata washiriki ndani ya kipindi cha miezi sita ya programu hiyo.

MWISHO.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisoma nyaraka kabla ya kuzungumza na Wahitimu kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi. 


Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mary Mwakapenda akitunukiwa cheti cha Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi iliyotolewa na Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wahitimu wa Programu ya Uongozi kwa Wanawake wakiwa mbele mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Mwalibora Mwamtuya kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, akitunukiwa cheti cha Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Judith Shoo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora akitunukiwa cheti cha Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo akizungumza na Wahitimu wa Programu ya Uongozi kabla ya wahitimu hao kutunukiwa vyeti vyao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Programu ya Uongozi mara baada ya wahitimu hao kutunukiwa vyeti vyao na Waziri huyo kwenye mahafali ya tisa ya programu za uongozi zitolewazo na Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Monday, May 11, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

Na. Antonia Mbwambo-Arusha

Tarehe 12 Mei, 2026.

Watumishi wa Umma nchini wamehakikishiwa kuboreshewa mazingira ya kazi kadri uchumi utakavyoruhusu ili kuleta tija katika utendaji kazi kwa maslahi ya umma.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika leo tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Mhe. Qwaray amesema, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Watumishi wa Umma wote nchini wakiwemo Wauguzi, hivyo itazingatia changamoto wanazokutana nazo watumishi hao, pamoja na kushughulikia kwa uzito unaostahili ili kutengeneza mazingira mazuri ya utendaji kazi.

"Niwahakikishie Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi wa Umma kadri uchumi utakavyoruhusu kwani tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuwahudumia Watanzania, fanyeni kazi, Serikali ipo nanyi." Mhe. Qwaray alisema.

Aidha Mhe. Qwaray ameongeza kuwa, ili kuwa na ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi Serikali itaendelea kuisimamia sekta ya afya pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma bila kuathiri misingi ya Utumishi wa Umma, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ikiwemo uzingatiaji wa maadili.

Aidha amewataka kuwa na kauli nzuri,  huruma na upendo utakaoongeza tija katika utendaji kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika Sekta ya afya.

"Ninyi ndiyo watu wa kwanza kukutana na mgonjwa pindi anapofika hospitali na ni watu wa mwisho mgonjwa anapotoka hospitali baada ya matibabu, ikiwa mtakuwa na nyuso za ukatili na ulimi mkali au wa kebehi, mtawakwaza wagonjwa na hata kuwakatisha tamaa jambo ambalo litaonyesha mapungufu katika sekta ya afya.”Mhe. Qwaray alisema.

Vilevile, Mhe. Qwaray amewaahidi Wauguzi hao kuwa Ofisi imepokea masuala yote waliyoyaeleza katika risala yao na kuwaahidi kuyawasilisha kwa ajili ya kufanyiwa kazi ikiwemo masuala ya Muundo Mpya wa Utumishi wa Kada ya Uuguzi na Ukunga na Muundo wa Utawala katika Sekta ya Afya ili kuboresha huduma ya afya na maslahi ya watumishi wa afya nchini.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Qwaray, ametoa wito kwa wauguzi kuhahakisha wanabadili mienendo na tabia zisizopendeza wala kuendana na maadili ya kazi yao, lakini pia amewapongeza kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi na kuboresha afya zao.

Kwa upande wake  Rais wa Chama cha Wauguzi (TANNA), Dkt. Ezekiel Mbao amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kujumuika nao kwenye maadhimisho ya siku hiyo adhimu.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Wauguzi Duniani yamebeba kauli mbiu isemayo Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu, Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Wauguzi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania (hawapo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani mara tu baada ya Naibu waziri huyo kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika  kuanzia tarehe 9 hadi 12, Mei, 2026 jijini Arusha

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, akitembelea mabanda ya maonesho ya Wauguzi kujionea baadhi ya shughuli wanazozifanya katika kuwahudumia Watanzania kabla ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika tarehe 12 Mei, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Dunuani wakifuatilia hotuba ya Mheni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati walipokuwa katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akikabidhiwa zawadi ya Chama cha Wauguzi (TANNA) na Raisi wa chama hicho Dkt. Ezekiel Mbao mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, akisaini kitabu cha wageni,mara tu baada ya kuwasili katika ukumbi wa AICC Arusha kwenye Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akisalimiana na baadhi ya viongozi wa chama cha wauguzi (TANNA) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12 Mei,2026.

Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Dunuani wakifuatilia hotuba ya Mheni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati walipokuwa katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akikabidhi zawadi kwa aliyekuwa Raisi wa chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani Jijini Arusha kama ishara ya kutambua mchango alioutoa Raisi huyo wakati alipokuwa kiongozi wa Chama hicho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akipokea maelezo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya Wauguzi katika kuwahudumia wananchi, mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea mabanda ya maonesho katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akiwasili katika ukumbi wa AICC Arusha tayari kwa kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12, Mei, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray,akifurahia jambo wakati alipokuwa akifuatilia Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani,yaliyofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.