Thursday, March 30, 2017

MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI (MB) APONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA KWA KUSIMAMIA UTENDAJI MZURI WA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS-MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 kwa ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akimsikiliza kwa makini. 
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Ahmed Juma Ngwali (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Margaret S. Sitta (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Saada Mkuya (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Mwanne I. Mchemba (Mb) (hayupo pichani) wakati akiongoza kikao cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).



Tuesday, March 21, 2017

KAZI YA UHAKIKI WA TAARIFA ZA WATUMISHI


Mtumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Deograsius Michael, akiwa na Kitambulisho cha Taifa ili kuhakiki taarifa zake za kiutumishi.

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Ibrahim Mahumi wakihakiki taarifa za Watumishi wa Umma zilizowasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Ibrahim Mahumi akiangalia taarifa za Watumishi wa Umma zilizowasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Wednesday, March 15, 2017

WAAJIRI NA WATUMISHI WA UMMA NCHINI: OPRAS IPO KWA SHERIA HIVYO NI WAJIBU KUITEKELEZA IPASAVYO

Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (wa kwanza kulia) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC One kuhusu Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS). Wengine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo (katikati) na Mwongozaji wa kipindi hicho, Bw. Rashid Salim.
Mtangazaji wa Kipindi cha “JAMBO” kinachotangazwa na TBC One, Bw. Rashid Salim (kushoto) katika mahojiano na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo. Kipindi cha Jambo maudhui yake yalikua kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kulia) akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo. Wengine ni waongozaji wa kipindi hicho, Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo (kushoto) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC Taifa kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba. Wengine ni waongozaji wa kipindi hicho kushoto ni Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.