Monday, December 23, 2019

SALAMU ZA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2020


RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAGIZA VIJANA WENYE SHAHADA YA KWANZA WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT “OPERESHENI MAGUFULI” WAAJIRIWE SERIKALINI




Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kuhusu ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa “Operesheni Magufuli” na masuala mbalimbali ya kiutumishi. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kuhusu ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa “Operesheni Magufuli na masuala mbalimbali ya kiutumishi. 



Thursday, December 12, 2019

Wadau watakiwa kutoa mchango utakaoboresha utendaji kazi na kuleta tija katika Utumishi wa Umma




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wadau wa Tija katika Ukumbi wa HAZINA Ndogo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau hao kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wenye lengo la kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kuongeza Tija. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wadau wa Tija wenye lengo la kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kuongeza Tija katika Ukumbi wa HAZINA Ndogo jijini Dodoma kabla ya kufungua kikao cha wadau hao kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Baadhi ya wadau wa Tija wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika Ukumbi wa HAZINA Ndogo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau hao kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wenye lengo la kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kuongeza Tija.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bi. Mariam Mwanilwa akimshukuru Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufungua mkutano wa wadau wa Tija wenye lengo la kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kuongeza Tija katika Ukumbi wa HAZINA Ndogo jijini Dodoma.


Taasisi za Umma zatakiwa kutekeleza Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kabla ya kufungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka.
Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Harold R. Nsekela akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)(katikati mstari wa mbele) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.


Thursday, December 5, 2019

TAKUKURU YATAKIWA KUDHIBITI RUSHWA KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo akitoa taarifa ya utekelezaji ya TAKUKURU kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma leo.

Baadhi ya viongozi wa TAKUKURU wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma leo.

Wednesday, November 27, 2019

UTUMISHI YASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, JIJINI DODOMA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa  tarehe 26/11/2019 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Wednesday, November 20, 2019

KAMISHNA WA TUME YA MAADILI NA KUZUIA RUSHWA NCHINI KENYA ATEMBELEA OFISI YA RAIS UTUMISHI

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi akimkabidhi Miongozo mbalimbali ya Mapambano dhidi ya Rushwa Kamishna wa Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa nchini Kenya, Bibi Rose Mghoi Machaira baada ya kikao kilichofanyika tarehe 18/11/2019 Ofisi ya Rais Utumishi, Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa nchini Kenya, Bibi Rose Mghoi Machaira mara baada ya kikao kilichofanyika tarehe 18/11/2019 Ofisi ya Rais Utumishi, Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa-Kenya.


Tuesday, November 19, 2019

MIAKA MINNE YA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA ENEO LA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA


MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA KUZUNGUMZIA NAMNA YA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mbele) wakiwa kwenye kikao kazi na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo ndiye mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya muungano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Friday, November 15, 2019

WATUMISHI 44,800 WA KADA YA AFYA KUAJIRIWA NCHINI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Silafu Jumbe Maufi  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.


Thursday, November 14, 2019

TAASISI ZA UMMA NCHINI ZATAKIWA KUWAPATIA HUDUMA YA USAFIRI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Amina S. Mollel  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango  wa Serikali wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.


Tuesday, November 12, 2019

TASAF YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE KWA MAFANIKIO YA MALIPO YA RUZUKU KIELEKRONIKI KWA KAYA MASKINI


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson Rweikiza (Mb) akifungua kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mada kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana. 
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Rehema Migilla (Mb) akichangia hoja kuhusu mada ya matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilshwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Mb) akifunga kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.