Monday, November 30, 2015

WIKI YA UADILIFU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

 


Simu ya Upepo "UTUMISHI", DSM.                               Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Simu: 2118531/4 au 2122908                                      Utumishi House,
Barua Pepe:permsec@estabs.go.tz                                8 Barabara ya Kivukoni,
                                                                                       11404 Dar es Salaam.

                                                            30/11/2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WIKI YA UADILIFU

Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenza Wiki ya Uadilifu katika Utumishi wa Umma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu leo ameongoza zoezi la kutoa Ahadi za Uadilifu kwa viongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Bw. Mkwizu alisema zoezi hilo ni endelevu na muhimu sana kwa Watumishi wa Umma hapa nchini.

“Tuishi viapo vyetu tulivyoahidi leo” Bw. Mkwizu alisisitiza na kusema ahadi hiyo iwe sehemu ya kazi ambapo inahusisha  ujazaji wa fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma (PL.4), ambayo mhusika husaini kwa cheo alichonacho na Mtendaji Mkuu wa Taasisi yake.

Pamoja na masuala mengine, fomu hiyo itatumika pia kwa Watumishi wapya katika Utumishi wa Umma, mtumishi akibadilishwa cheo au kuhama ofisi.

Moja ya malengo ya fomu hiyo ni kuendeleza dhana ya Uwajibikaji, Usikivu kwa Umma na kuzingatia weledi katika Utumishi wa Umma. Fomu ya Ahadi ya Uadilifu inapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye anuani, www.utumishi.go.tz.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kny: KATIBU MKUU - UTUMISHI



VIONGOZI OFISI YA RAIS- UTUMISHI WALA KIAPO CHA UADILIFU

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu akitia saini fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kulia).

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akielekeza namna ya kutoa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma. 

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiweka Ahadi za Uadilifu katika fomu maalum wakati wa zoezi hilo lililoratibiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu .

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakila kiapo cha  Uadilifu kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto).
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Mathew Kirama fomu maalum ya kuweka Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma.

Sunday, November 29, 2015

WATUMISHI WA UMMA WAHIMIZWA KUFANYA MAZOEZI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Utumishi Bw.Tixon Nzunda (kulia) akiwahimiza watumishi kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara katika bonanza lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakifanya mazoezi ya viungo katika bonanza lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.  
Baadhi  ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakishiriki bonanza lililoandaliwa na ofisi hiyo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Utumishi yasisitiza Taasisi za Umma kutumia teknolojia ya mikutano kwa njia ya video ( Video Conference)

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Florence Temba akisisitiza matumizi ya teknolojia ya video Serikalini (Video Conference) alipokuwa akihojiwa na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji TBC Bi. Angella Michael.

KATIBU MKUU UTUMISHI AWAHIMIZWA WATUMISHI KUWAJIBIKA

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Watendaji Wakuu wa ofisi zilizo chini yake katika kikao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika ofisini kwake. 
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wote kilichofanyika ofisini hapo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Wednesday, November 25, 2015

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kupunguza gharama za utekelezaji wa majukumu kwa watendaji na watumishi wa Umma nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais , Utumishi Bw. Florence Temba (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano kwa njia ya Video (video conference) ambayo inapunguza gharama za uendeshaji wa vikao kazi serikalini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Florence Temba (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)faida za kutumia TEHAMA katika kuendesha vikao kazi serikalini. Kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Florence Temba (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu faida za matumizi ya TEHAMA katika kuendesha vikao kazi serikalini.Kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhusu matumizi ya TEHAMA kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za Serikali. 

Taarifa kwa vyombo vya Habari




Friday, November 20, 2015

ANNOUNCEMENT OF INTERNATIONAL MASTER OF PUBLIC ADMINISTRATION FROM FEBRUARY 2016 – JANUARY 2017

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  
PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE MANAGEMENT

Applications are invited from qualified Tanzanians from the Public Sector to apply for the Master Degree tenable in China for the year 2016/2017.

Application procedures and forms are available at:  http://is.tsinghua.edu.cn

The entire cost of these training courses which include the return international airfare, tuition fees, accommodation, is born by the Government of the People’s Republic of China.

Eligibility requirements:
·   Be government official no less than 5-years working experiences
·   A Bachelor degree holder and G.P.A is above 3.0
·   Excellent in Administrative Skills and High English Proficiency
·  Be preferably under 40 years of age in good health and physically and mentally to complete the programme.

Mode of Application:
The nominated candidate should submit two (2) printed and typed copies of completed application forms (attached), with 2-inch recent photo, three recent photos of passport size, Bachelor’s degree certificate, Academic transcript, Personal statement signed by the applicant (in English), Two letters of recommendation (signed and sealed by the employer), copy of passport, Foreigner Physical Examination Form, Chinese Government Scholarship Application Form, Curriculum Vitae and formal letter of introduction from their employer not later than 30th November, 2015, and submits to this office, Human Resources Development Division Room No 017, Ground Floor.

NB: For online application (directly to the International Students Office, Tsinghua University please refer to(http://is.tsinghua.edu.cn

Deadline for submissionof application forms is on 30th November, 2015.


The completed application forms should be sent to the following address:-

Permanent Secretary,
President’s Office,
Public Service Management,
Utumishi House,
8 Kivukoni Road,
P.O. BOX 2483,
11404 DAR ES SALAAM.Att: Division of Human Resource Development


Friday, November 6, 2015

Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akila kiapo

Rais  wa Serikali ya  Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akila kiapo cha kuliongoza Taifa katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.