Monday, November 17, 2014

UBALOZI WA INDIA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MPANGO WA USHIRIKIANO WA KIUFUNDI NA UCHUMI WA SERIKALI YA INDIA (ITEC)




Baadhi ya wageni waalikwa na wanufaika wa Mpango wa Mafunzo Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi wa Serikali ya India (ITEC)  wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mpango huo yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India jijini Dar es Salaam.

Balozi wa India nchini Tanzania Mh.Debnath Shaw akizungumza wakati wa sherehe za  maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Mafunzo Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi wa Serikali ya India (ITEC)  yalichofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India jijini Dar es Salaam.


 Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto),Balozi wa India nchini Tanzania Mh.Debnath Shaw (wa pili kutoka kushoto)  na wageni waalikwa wakiangalia filamu ya mpango wa mafunzo ya India wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi na Uchumi wa Serikali ya India (50 YEARS ITEC DAY) yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India  jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi na Uchumi wa Serikali ya India (50 YEARS ITEC DAY) yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India  jijini Dar es Salaam