Tuesday, December 20, 2016

Kwa Watumishi wa Umma

Kwa Watumishi wa Umma, sasa unaweza kupata taarifa mbalimbali za kiutumishi zinazokuhusu, mfano makato katika mshahara kama umekopa, kutafuta mtu wa kubadilishana kituo na kukamilisha taratibu nyingine muhimu, kutoa maoni au kuwasilisha lalamiko. Tembelea kiunganisho hiki >>/Watumishi portal


SERIKALI YAWASHUKURU WATAALAM WA KUJITOLEA WALIOMALIZA MUDA WAO WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika mazungumzo na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akimkabidhi zawadi Mtaalam wa kujitolea kutoka Japani aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini, Bw. Hiroshi Mikuni, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiagana na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi

Friday, December 16, 2016

WANUFAIKA WA MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA SERIKALI YA JAMHURI YA KOREA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Kimataifa la Korea (KOICA), Bw. Joonsung PARK, akitoa neno la utangulizi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma nchini Korea (KOICA/KAAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma nchini Korea (KOICA/KAAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo yanayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia KOICA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma nchini Korea (KOICA/KAAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa mafunzo yanayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia KOICA mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma nchini Korea (KOICA/KAAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Thursday, December 15, 2016

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA KUHUSU MASUALA YA UTAWALA BORA

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi Bella Bird akiongea kuhusu masuala ya utawala bora na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisimkiliza Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi Bella Bird (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akijadili masuala ya utawala bora na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi Bella Bird alipomtembelea ofisini kwake.

MHE. KAIRUKI AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MADEREVA WA SERIKALI TANZANIA (CMSP) KUJADILI MASUALA YA KIUTENDAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMSP) mara baada ya kukutana na viongozi hao kwa lengo la kujadili masuala ya kiutendaji ofisini kwake leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMSP) mara baada ya kukutana na viongozi hao kwa lengo la kujadili masuala ya kiutendaji ofisini kwake leo.

Tuesday, December 13, 2016

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHITIMISHA WIKI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI KITAIFA NA HAKI ZA BINADAMU NCHINI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na Idara ya Ukuzaji Maadili ya Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Dini wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa nchini na wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipokuwa akifunga rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihitimisha kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Makati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu siku ya kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.