Na. Veronica Mwafisi-Singida
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewaasa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania (TPSC) kusimamia na kutunza maadili ya taaluma walizosomea kwa
ustawi wa taifa.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo tarehe 30 Mei, 2025 kwenye Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
“Kuhitimu ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada katika fani mbalimbali
sio jambo dogo, elimu mliyoipata ni kubwa, hakikisheni mnasimamia na
kutunza maadili ya elimu hiyo kwa manufaa yenu na ustawi wa taifa” amesisitiza
Mhe. Simbachawene.
Mhe. Simbachawene amewataka wahitimu
walioajiriwa katika Utumishi wa Umma na watakaoajiriwa kufanya kazi kwa
bidii kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma
ikiwa ni pamoja na kutunza siri za Serikali na kuepuka rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao na wahitimu ambao hawana ajira
kutumia ujuzi walioupata kujiajiri kwa maendeleo ya taifa.
Aidha, ametoa
rai kwa wahitimu hao kutunza afya zao pamoja na kuepuka Magonjwa Yasiyoambuza kwa kuwa taifa linawahitaji katika kukuza uchumi wa nchi.
Vilevile, Mhe. Simbachawene ameueleza uongozi wa chuo hicho kuwa
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ina matarajio makubwa na Chuo hicho kwa kuwa kimeimarika
sana hasa katika kuwajengea uwezo watumishi wa Umma na kutoa wahitimu mahiri na
wenye uzalendo wanaoleta chachu ya maendeleo nchini.
Kadhalika, Mhe. Simbachawene amewapongeza Walimu, Wazazi na Walezi wa wahitimu hao kwa jitihada kubwa ambazo
kila mmoja kwa nafasi yake amezifanya ili kufanikisha kupata wahitimu hao wa ngazi
za Shahada, Stashahada na Astashahada katika fani mbalimbali.
Awali, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania Dkt. Ernest Mabonesho amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kukubali
mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo na kumtaarifu kuwa jumla ya
wanafunzi 1330 wamehitimu kozi mbalimbali katika chuo hicho wakiwemo wanawake
906 na wanaume 224.
Dkt. Mabonesho ameongeza kuwa pamoja na jitihada nyingine
zinazofanywa na chuo hicho, wameendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za ndani
ikiwemo Chuo cha Hombolo na vyuo vingine mbalimbali pamoja na vya nje ya nchi
kwa lengo la kuboresha ujuzi na kubadilishana uzoefu katika utendajikazi.
“Mhe. Mgeni rasmi tumefanya jitihada mbalimbali ili kuboresha
mafunzo yetu kwa kushirikiana na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi hasa vinavyohusika
na masuala ya Utumishi wa Umma ikiwemo chuo cha Hombolo pamoja na vyuo vingine
ili kuweza kupata fursa ya kujifunza na kuboresha utendajikazi” alisema Dkt.
Mabonesho.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema taifa
limepata wahitimu ambao ni nguvukazi nyingine watakaosaidia utendajikazi katika
Utumishi wa Umma
na taifa kwa ujumla.
Aidha, SACP. Mahumi amemshukuru na kumpongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene kwa kusimamia miongozo mbalimbali pamoja na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo ambayo imekisaidia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kuhitimisha wanafunzi wanaoweza kutekeleza majukumu mbalimbali pasipokuwa na changamoto zozote.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na wahitimu
wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika
mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mahafali hayo
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC
Mission mkoani Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia
nyekundu) akijumuika katika maandamano ya wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo
pichani) katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu hao
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi akitoa akitoa
neno la utangulizi kwa wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wahitimu hao
wakati wa Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta
jambo na Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.
Ernest Mabonesho (kushoto) wakati wa Mahafali
ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC
Mission mkoani Singida.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha taarifa ya utendaji wa chuo kwa
mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa mahafali ya 41 ya Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi
wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika
mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakifurahi wakati wa
maandamano yaliyofanyika nje ya Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia
nyekundu) akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania, Prof. Masoud Muruke (wa kwanza kulia) ambaye amemwakilisha Mwenyekiti
wa bodi hiyo kwenye Mahafali ya 41 wakati Waziri huyo
alipowatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa chuo hicho (hawapo pichani) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social
Rwoma RC Mission mkoani Singida. Wa kwanza
kushoto ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.
Ernest Mabonesho.
Sehemu ya wazazi na
walezi wa wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa Mahafali ya 41 ya
chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani
Singida
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia
nyekundu) akitazama maandamano ya wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani)
katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu hao wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Social Rwoma RC Mission mkoani Singida. Wengine ni Viongozi wa mkoa huo na
Watendaji wa chuo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na sehemu ya wahitimu
wa ngazi mbalimbali
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
wakati wa Mahafali ya 41 ya chuo hicho yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.
Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, wakielekea kwenye Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission wakati
walipojumuika kwenye msafara wa wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi huo
mkoani Singida.