Friday, August 25, 2017

MHE. KAIRUKI AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NA UJUMBE WAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimkaribisha Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Inmi Patterson (kushoto) na ujumbe alioambatana nao alipotembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Inmi Patterson (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Inmi Patterson (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Inmi Patterson (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

MHE. KAIRUKI AAGANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ALIYEMALIZA MUDA WAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Dr.Lu Youqing (katikati), aliyefika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kumuaga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Dr.Lu Youqing (katikati), aliyefika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kumuaga. 

Balozi wa China nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Dr.Lu Youqing (kulia), akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipokwenda kumuaga ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wengine ni watumishi walioambatana na Balozi. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akikabidhi zawadi kwa Balozi wa China nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Dr.Lu Youqing, aliyefika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kumuaga. 

Thursday, August 24, 2017

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO YA KIKAZI NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Masaharu Yoshida (kushoto) alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Masaharu Yoshida (kushoto) alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Masaharu Yoshida ()kulia alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake. 

Monday, August 21, 2017

Watanzania nane wapata ufadhili wa masomo chini ya Mpango wa ABE

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga Watanzania waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga Watanzania waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Watanzania waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Mafunzo ya ABE akielezea alivyonufaika na mafunzo hayo wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kuwaaga Watanzania nane waliopata ufadhili wa masomo chini ya Mpango huo. 


Sunday, August 13, 2017

Ofisi ya Rais-UTUMISHI yawakaribisha Wataalam watano wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliokuja kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani (hawapo pichani) waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini 
baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI.Wengine ni wafanyakazi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Thursday, August 3, 2017

KATIBU MKUU UTUMISHI AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA MADEREVA WA SERIKALI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro  (mwenye tai) katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali (CMSP) mara baada ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ofisini kwake mjini Dodoma leo.


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MASAA YA KUNYONYESHA KWA MAMA ALIYEAJIRIWA



Miundo ya Utumishi wa Umma

Tembelea link ifuatayo kusoma Waraka Na.1 wa mwaka 2004 kuhusu Utekelezaji wa Miundo ya Utumishi wa Umma;
http://www.utumishi.go.tz/utumishiweb/index.php?option=com_phocadownload&view=file&id=398:waraka-wa-utumishi-na-1-wa-2004-kuhusu-utekelezaji-wa-miundo-ya-utumishi&Itemid=180&start=20&lang=en

Miundo ya UTUMISHI

"Watumishi wa Umma ambao Miundo yao ya Maendeleo ya Utumishi iliwataka kuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha Nne wakati wanaajiriwa, na ambao hawajawasilisha vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania mishahara yao isimamishwe kuanzia mwezi Julai, 2017 hadi watakapowasilisha vyeti hivyo kwa ajili ya kuhakikiwa"
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Julai 13/2017