Saturday, April 29, 2017

UTUMISHI YACHAGUA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2017

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017 uliofanyika leo katika ofisi hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru akitoa maelekezo ya kumchagua mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.

Wawakilishi wa wafanyakazi bora wa Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru wakishuhudia kura zikihesabiwa ili kumpata mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.

Waziri Kairuki azindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya UmmaKatibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro(aliyesimama) akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mapema leo. 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)(kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyofanyika mapema leo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma Bi.Gertrude Mpaka (katikati) akizungumza baada ya uzinduzi wa bodi hiyo katika  ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mapema leo.

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (wa nne kutoka kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro  (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma baada ya kuizindua bodi hiyo mapema leo.

Thursday, April 20, 2017

Tuesday, April 18, 2017

Mhe. Kairuki awasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Taasisi zake

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka wa Fedha wa 2017/18. 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-Ikulu Bw. Alphayo Kidata, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. SusanMlawi wakiwa pamoja na watendaji wa ofisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka wa Fedha wa 2017/18.


Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka wa Fedha wa 2017/18. MHE. KAIRUKI AWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA...

Saturday, April 8, 2017

SERIKALI YAWAPOKEA WATANZANIA WALIOHITIMU MASOMO CHINI YA MPANGO WA ABE UNAORATIBIWA NA JICAMkurugenzi-Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Utumishi Bi. Roxana Kijazi akizungumza kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bi. Susan Mlawi katika hafla fupi ya kuwakaribisha watanzania walionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam

Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania walionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE unaoratibiwa na shirika la JICA, baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha watanzania hao iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam

Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha watanzania walionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam

Wageni waalikwa walioshiriki hafla fupi ya kuwakaribisha watanzania walionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam


Thursday, April 6, 2017

Baraza Maalum la Watumishi laendeshwa kwa Njia ya Video Kwa mara ya Kwanza Nchini

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (katikati) akifungua mkutano wa baraza maalumu la wafanyakazi wa Utumishi kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza nchini Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa baraza maalumu la wafanyakazi wa Utumishi kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza nchini.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (wa pili kutoka kulia) akifungua mkutano wa baraza maalumu la wafanyakazi wa Utumishi kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza nchini.

Washiriki wa kikao maalum cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kilichofanyika kwa njia ya mtandao ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLA).
Washiriki wa kikao maalum cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kilichofanyika kwa njia ya mtandao wakifuatilia kikao hicho kutoka Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)(kushoto) akifungua mkutano wa baraza maalumu la wafanyakazi wa Utumishi kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza nchini. Kulia ni washiriki wa mkutano wakiwa Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi(kushoto) akizungumza na watumishi baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza maalumu la wafanyakazi wa Utumishi kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza nchini. Kulia ni washiriki wa mkutano wakiwa Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi -Idara ya Mipango Utumishi Bw. Lumuli Mtaki akiwasilisha mada kwa njia ya mtandao kutoka Makao Makuu ,Dodoma.