Saturday, September 28, 2019

DKT. MWANJELWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA JIJINI MWANZANa Happiness Shayo – Mwanza
Tarehe 28 Septemba, 2019

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kilichopo eneo la Pasiansi jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho, Dkt. Mwanjelwa amesema ujenzi wa mradi huo uko katika hatua nzuri hivyo, ameipongeza Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kwa kufikia hatua hiyo.
 “Hakika jengo hili ni la viwango, linaridhisha na vifaa vya ujenzi vilivyotumika viko katika viwango bora” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutenga bajeti iliyowezesha ujenzi wa kituo hicho kwani mradi huo ulianza tangu mwaka 2008.
“Matumizi ya mkandarasi na mshauri binafsi yalisababisha kuwapo kwa gharama kubwa za ujenzi zilizosababisha kusimama kwa ujenzi katika hatua za awali, lakini mwaka 2017/2018 Serikali ya Awamu ya Tano ilithamini mradi na kutoa fedha zilizofanikisha mradi kama unavyoonekana sasa” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amesema, Serikali iliamua kujenga kituo hicho cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa  kwa lengo la kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za ofisi za serikali zilizopo kanda ya ziwa.
Bw. Msiangi amesema, kituo kitakapokamilika kitatumika kama kituo mbadala cha kuhifadhi mifumo ya kumbukumbu na nyaraka iliyopo katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu cha jijini Dodoma.
Naye, Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar amemthibitishia Dkt. Mwanjelwa kuwa, ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2019.
“Mpaka sasa tumejenga jengo la utawala, maghala ya kuhifadhia nyaraka kwa asilimia 95 na pia tumejenga uzio, eneo la kuegesha magari, eneo la bustani, banda la walinzi na madereva kwa asilimia 60” Bw. Baltazar amefafanua.

Ziara ya Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ya kutembelea kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Mwanza ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake la kukagua utekelezaji wa miradi iliyo chini ya Ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo


Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firmin Msiangi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.

Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akitoa ufafanuzi wa michoro ya ramani ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akielekeza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar.

Thursday, September 26, 2019

WAZIRI MKUCHIKA AZITAKA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS KUWA MFANO WA KUIGWA KIUTENDAJI NA KIMAADILI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Baadhi ya Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua hoja za Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao kazi na Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel S. Shindika akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) kwa kufanya ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.Sunday, September 22, 2019

WATUMISHI WA UMMA KATIKA HALMASHAURI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na  Kilombero (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.

Watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Ifakara na  Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani)  wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini..

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyesimama)  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na  Kilombero (pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.