Tuesday, July 29, 2025

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA TANZANIA

 Na. Lusungu Helela-Dodoma 

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) tarehe 27 Agosti, 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dare s Salaam.

 Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema pamoja na kufungua rasmi mkutano huo, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa pia ataendesha zoezi la harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Maarifa kitakachokuwa na masijala ya mfano, kumbi za mikutano pamoja na ofisi za TRAMPA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma.

 Kufuatia mkutano huo wa kitaaluma, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Waajiri wote kuwaruhusu Watunza kumbukumbu ili waweze kushiriki kwani ni jukwaa muhimu la  kuwajengea uelewa wa majukumu wanayoyatekeleza ukizingatia kwa sasa majukumu ya kazi zao kwa zaidi ya asilimia 99 yanaendeshwa kwa mfumo wa kidijitali.

 Aidha, ameongeza kuwa, ushiriki wao ni muhimu katika mkutano huo kutokana na taaluma yao hasa katika utunzaji wa siri za ofisi za umma.

 Akizungumzia maandalizi ya mkutano huo, Mwenyekiti wa TRAMPA, Bi. Devotha Mrope amesema maandalizi yanakwenda vizuri huku akibainisha kuwa mwitikio wa wadhamini waliojitokeza kwa ajili ya kuhakikisha mkutano huo unafanyika umekuwa mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

 "Tumebahatika kupata wadhamini zaidi ya 24 na tunaamini tutawapata wengi zaidi kadiri siku zinavyokwenda" amesema Bi. Mrope

 Bi. Mrope ameongeza kuwa mwitikio wa washiriki katika mkutano huo ni wa kuridhisha huku akitaja idadi ya washiriki zaidi ya 5000 watashiriki mkutano huo huku akibainisha moja ya ajenda katika mkutano huo itakuwa ni kuhamasisha wataalamu wa kada hiyo kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kuwa  Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana leo jijini Dodoma na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.



  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) Bi.  Devotha Mrope

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza leo jijini Dodoma na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam



 Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) Bi.  Devotha Mrope akizungumza leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuhusiana na mkutano  utakaofanyika Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.

 

 

 

Monday, July 28, 2025

WATUMISHI WAKUMBUSHWA KUTANGULIZA UZALENDO KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 28 Julai, 2025

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamekumbushwa kutanguliza uzalendo wanapotoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa maslahi ya Taifa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake kwenye eneo maalum la mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika Mtumba jijini Dodoma kila Jumatatu ya mwanzo wa wiki.

“Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, tutangulize uzalendo na tuhakikishe tunafahamu majukumu yote ya ofisi hii ili tuweze kuwahudumia Watumishi wa Umma na Wananchi kwa maslahi ya Taifa.” amesema Bw. Daudi.

Aidha, Bw. Daudi amesisitiza watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwa waadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma wanapotekeleza majukumu yao.

Awali akiwasilisha mada kuhusu Maslahi ya Taifa na Ulinzi wa Taifa, Balozi Omar Mjenga amesema, watumishi wa umma wana wajibu wa kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuzingatia utii usiokuwa na shaka, kiapo cha utii pamoja na kujitoa kikamilifu kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, Balozi Mjenga ameupongeza Uongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora pamoja na watumishi wa ofisi hiyo kwa kuwa na utayari wa kuandaa na kushiriki mafunzo kila Jumatatu ya mwanzo wa wiki ili kujenga uelewa kwa watumishi hao kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Afisa kutoka Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Oswin Mkinga (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu masuala ya utendaji kazi ktk taasisi za umma wakati wa mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Sehemu ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Balozi Omar Mjenga (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Maslahi ya Taifa na Ulinzi wa Taifa wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.



Friday, July 25, 2025

KATIBU MKUU MKOMI AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MAKAZI YA WATUMISHI KIJIJI CHA KIJIWENI

Na. Veronica Mwafisi-Lindi

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma unaojengwa katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ili kuwasaidia watumishi hao kuwa karibu na ofisi wanazofanyia kazi kwa lengo la kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo leo, Katibu Mkuu Mkomi amesema ujenzi wa makazi ya watumishi hao utawasaidia kuepeukana na changamoto ya makazi ambayo imekuwa ikiwakabili na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiwajali sana watumishi wa umma katika kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo utekelezaji wa mradi wa makazi ya watumishi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kuujenga utumishi wa umma pamoja na kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa watumishi wa umma ili wawe na tija katika utoaji wa huduma kwa maendeleo ya taifa,” Katibu Mkuu Mkomi ameongeza.

Bw. Mkomi amesema mradi wa ujenzi wa makazi hayo ya watumishi upo katika hatua ya majaribio katika Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi ambapo pia unatekelezwa katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Ruvuma.

Katibu Mkuu Mkomi katika ziara hiyo aliambatana na baadhi ya Wakurugenzi wa ofisi yake ambapo kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute amesema Watumishi Housing Investments ndiyo kandarasi inayojenga makazi katika mradi huo.

Bw. Allute ameongeza kuwa, mradi huo unafuatiliwa na kusimamiwa kikamilifu ili uweze kukamilika kwa wakati.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo (wapili kutoka kulia) na Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Bw. Samson Bihole mara baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka katika ofisi yake na Viongozi na Watendaji wa Shule ya msingi Kijiweni mara baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.

Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.

 

 





Wednesday, July 23, 2025

IBADA MAALUM YA KUMBUKIZI YA MIAKA MITANO (5) YA KIFO CHA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI BENJAMIN WILLIAM MKAPA



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi na Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara wakati wa Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.

Wananchi wakisikiliza hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Ibada maalaum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (watatu kutoka kulia) akifuatilia Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki Ibada hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (watatu kutoka kulia) akielekea kushiriki Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene na kulia kwake ni mjane wa Hayati Benjamin Mkapa ambaye ni Bi. Anna Mkapa.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa kijijini Lupaso wakati wa Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais huyo iliyofanyika kijijini hapo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa wakati wa Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais huyo iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.

 

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakiwa Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa utambulisho wa viongozi na wageni walioshiriki Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.


Wananchi wakiwa katika Ibada maalaum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Nicholas Mkapa (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa ofisi hiyo, Bi. Salome Kessy (wa kwanza kulia) kabla ya kuanza kwa Ibada maalaum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakiwa katika Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.


Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhadhama Kardinali Pengo akiongoza Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.


Viongozi mbalimbali wakiwa katika Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano (5) ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara.




Tuesday, July 22, 2025

KIKAO KAZI CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI

 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Salome Kessy (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (kushoto) wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Tairo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kuhusu Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma na Taasisi (e-Utendaji) wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Tairo (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo kuhusu Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma na Taasisi (e-Utendaji) wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Msaidizi, Usimamizi wa Mifumo na Viwango vya Kimenejimenti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Veila Shoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kuhusu Daftari la Huduma za Serikali wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Paul Seadin (kulia) akifuatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Sera za Tehama na Viwango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Toure (wa kwanza kulia) akiwa katika kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

 


KIKAO KAZI CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI






 

Sunday, July 20, 2025

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI WALETA MAPINDUZI MAKUBWA YA TEHAMA NCHINI IKIWEMO KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI NA WATUMISHI WA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam

Mradi wa Tanzania ya Kidijitali umeleta mapinduzi makubwa ya miundombinu ya TEHAMA nchini ikiwemo kuunganisha jumla ya taasisi za umma 600 ambazo ni Wizara, Mikoa, Halmashauri na Taasisi zote zilizohamia Dodoma ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na watumishi wa umma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mradi huu umeleta mafanikio makubwa katika kuunganisha Serikali kwenye mitandao ya TEHAMA ambapo taasisi 600 ikiwemo Wizara, Mikoa, Halmashauri na Taasisi zote zilizohamia Dodoma zimeunganishwa na mifumo ya TEHAMA ili kutoa huduma kwa wananchi na watumishi wa umma nchini,’’ amesema Bw. Kiwango

Ameongeza kuwa katika kutoa huduma bora, watumishi wa umma wameendelea kutekeleza majukumu yao kupitia mifumo mbalimbali na kupimwa kupitia mifumo iliyojengwa ya Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma na Taasisi (e-Utendaji).

Aidha, Mfumo wa Daftari la Huduma za Serikali utawasaidia wananchi kupata huduma sehemu moja kwa urahisi, kwa wakati na kwa uwazi.

Mkurugenzi Kiwango ametoa wito kwa wananchi kutumia simu zao za viganjani kupiga namba *152*00# kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za Serikali bila kufika katika ofisi husika endapo hawatakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akizungumza kwenye kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Salome Kessy (katikati) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (kushoto kwake) wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Mifumo na Huduma za TEHAMA, Bw. Mohamed Mashaka.  


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Salome Kessy (katikati) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (kushoto kwake) wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Mifumo na Huduma za TEHAMA, Bw. Mohamed Mashaka.  


Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mary Mwakapenda (wa kwanza kulia) akiwa katika kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

 


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo kuhusu TEHAMA wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Paul Seadin (aliyesimama) akichangia hoja wakati wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo kuhusu TEHAMA wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Salome Kessy (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Sera za Tehama na Viwango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Toure (wa kwanza kulia) akiwa katika kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Salome Kessy (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.