Na. Lusungu
Helela-Dodoma
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya
Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) tarehe 27 Agosti, 2025 katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dare s Salaam.
Akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dodoma, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene amesema pamoja na kufungua rasmi mkutano huo, Waziri Mkuu
Mhe. Majaliwa pia ataendesha zoezi la harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha
Maarifa kitakachokuwa na masijala ya mfano, kumbi za mikutano pamoja na ofisi
za TRAMPA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma.
Kufuatia mkutano
huo wa kitaaluma, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Waajiri wote kuwaruhusu
Watunza kumbukumbu ili waweze kushiriki kwani ni jukwaa muhimu la
kuwajengea uelewa wa majukumu wanayoyatekeleza ukizingatia kwa sasa majukumu ya
kazi zao kwa zaidi ya asilimia 99 yanaendeshwa kwa mfumo wa kidijitali.
Aidha, ameongeza
kuwa, ushiriki wao ni muhimu katika mkutano huo kutokana na taaluma yao hasa
katika utunzaji wa siri za ofisi za umma.
Akizungumzia
maandalizi ya mkutano huo, Mwenyekiti wa TRAMPA, Bi. Devotha Mrope amesema
maandalizi yanakwenda vizuri huku akibainisha kuwa mwitikio wa wadhamini
waliojitokeza kwa ajili ya kuhakikisha mkutano huo unafanyika umekuwa mkubwa
ukilinganisha na miaka iliyopita.
"Tumebahatika
kupata wadhamini zaidi ya 24 na tunaamini tutawapata wengi zaidi kadiri siku
zinavyokwenda" amesema Bi. Mrope
Bi. Mrope ameongeza
kuwa mwitikio wa washiriki katika mkutano huo ni wa kuridhisha huku akitaja
idadi ya washiriki zaidi ya 5000 watashiriki mkutano huo huku akibainisha moja
ya ajenda katika mkutano huo itakuwa ni kuhamasisha wataalamu wa kada hiyo
kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba
mwaka huu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana leo jijini
Dodoma na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa mwaka wa
Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika
Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana leo jijini
Dodoma na Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania
(TRAMPA) Bi. Devotha Mrope
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza leo jijini Dodoma
na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa mwaka wa Chama cha
Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) utakaofanyika Agosti 27,
2025 jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na
Nyaraka Tanzania (TRAMPA) Bi. Devotha
Mrope akizungumza leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene kuhusiana na mkutano utakaofanyika
Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment