Na Eric Amani - Dodoma
Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ameishukuru timu ya wawekezaji kutoka Benki ya NMB Dodoma kwa kufika katika Ofisi za Utumishi kwa ajili kutoa elimu ya musuala mbalimbali yanayohusiana na huduma za kibenki kwa watumishi wa Ofisi hiyo.
Bw. Mkomi amesema hayo Jumatatu Agosti 11, 2025 katika Ofisi za Utumishi Jijini Dodoma, Ikiwa ni utaratibu wa kila siku ya Jumatatu ya wiki ambapo watumishi wa ofisi hiyo hupewa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Baada ya kupata elimu hiyo ya masuala ya fedha Katibu Mkuu Mkomi amewasisitizia watumishi wa Ofisi yake kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba pamoja na kukata bima za mali zao ili wanapopata majanga ya mali hizo wasichanganyikiwe
''Nawashukuru sana NMB kwa elimu nzuri ya masuala ya fedha hususan kuhusu ukataji wa bima ya mali tulizo nazo na kusema kuwa nina hakika wengi wetu hapa hatujakata bima ya nyumba zetu wakati tumejenga nyumba zenye thamani, tunakimbilia kuweka bima ya magari pekee na kuongeza kuwa elimu tuliyoipata hapa itusaidie kutekeleza haya tuliyofundishwa kwa mustabali wa maisha yetu na ya watoto wetu''
Awali, Meneja wa Benki ya NMB tawi la Dododma Bw. Amos Daniel amewashauri watumishi wa umma kujenga tabia ya kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali yalioainishwa katika Benki hiyo na kukata bima ya mali zao ili inapotokea majanga basi bima hiyo iwasaidie kufidia upotevu wa mali zao kulingana na bima waliyokata.
![]() |
| Sehemu wa Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia kwa vitendo Mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa Ofisi hiyo Jumatatu Agosti 11, 2025 |
![]() |
| Meneja wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma, Bw. Amos Daniel akitoa elimu ya uwekezaji na kukata bima kwa watumishi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora siku ya mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi Agosti 11, 2025 ikiwa ni utaratibu wa Ofisi hiyo kila Jumatatu. |
![]() |
| Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika Agosti 11, 2025. |






No comments:
Post a Comment