Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora,
Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments (WHI) imehitimisha ziara ya kikazi katika Mikoa ya Singida, Ruvuma, Lindi, Pwani na Dodoma iliyolenga kukagua
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Patrick Allute, amesema
watumishi wa umma wanafurahia utekelezaji wa mradi huo ambao wanaamini utaleta
motisha ya utendajikazi kwa kuwa karibu na eneo la kazi lenye makazi bora.
Kwa niaba ya timu hiyo Mkurugenzi Allute ameishukuru Serikali ya
Awamu ya Sita kwa kutekeleza kwa vitendo azma yake ya
kuwathamini watumishi wa umma kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi.
Kwa upande wake, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya fedha,
Bw. Ezekiel Odipo ameeleza kuwa, Serikali inawajali watumishi wa umma hivyo
imetoa fedha za kutosha ili kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo utekelezaji wa
mradi wa makazi ya watumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Naye, Mhandisi Salum Chanzi kutoka Watumishi Housing Investments, amesema WHI ndiyo kandarasi inayojenga makazi katika mradi huo ambao kwa sasa umefikia 85%.
Aidha, Mhandisi Chanzi amesema makazi hayo yatakuwa na ubora wa hali ya juu utakaoongeza ufanisi wa kazi kutokana na mazingira bora watakayokuwa nayo watumishi wa umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (watatu kutoka kulia) akizungumza jambo na Afisa
kutoka ofisi hiyo Bw. Rashid Shedafa (wakwanza
kushoto) wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa makazi ya watumishi
wa umma katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani
Dodoma.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa
umma lililopo katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikijadili jambo wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi iliyolenga kukagua
maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa
makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Msingi
Mlezi, mkoani Dodoma.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikikagua
maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa
makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya
Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment