Tuesday, June 30, 2026
Monday, June 29, 2026
KATIBU MKUU MKOMI AMPONGEZA NA KUMTAKIA HERI KATIBU MTEULE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, AMUASA KUZINGATIA FALSAFA YA KAZI NA UTU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Katibu Mkuu ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, Bw. Juma Mkomi amempongeza na kumtakia heri aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye
ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda.
Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo jijini Dodoma
baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo yanayofanyika kila Jumatatu kwa watumishi wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambapo pia alitumia wasaa huo kumuaga Bw. Kipanda.
Bw. Mkomi amemuasa Katibu mteule huyo kutumia
falsafa ya kazi na utu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ili aweze kutenda
haki katika kufanya maamuuzi.
Amesema, matatizo mengi yanayowapata Watumishi wa Umma
wakati mwingine yanatokana na kukosekana kwa utu wa waajiri hivyo, amemtaka Bw.
Kipanda kufanya maamuzi yaliyo sahihi ili kutenda haki.
“Ninaamini Bw. Kipanda
utaenda kutenda haki na kutuwakilisha vizuri, fanya kazi kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni, Taratibu na Utu. Taasisi uliyoteuliwa kufanya kazi inahusika na utoaji
wa haki kwa Watumishi wa Umma, hivyo pamoja na kutumia taratibu, ukazingatie
pia suala la utu katika kufanya maamuzi.
Vilevile, Bw. Mkomi amemuahidi
Bw. Kipanda ushirikiano pale atakapohitaji ikiwa ni pamoja na ushauri katika
kazi kwani itasaidia kuimarisha zaidi utendaji kazi.
Kwa upande wake Katibu
Mteule wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na
kumteua kuiongoza Taasisi hiyo.
Bw. Kipanda amewashukuru
Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora kwa kufanya kazi nao kwa muda mrefu na kuomba kuendelea kumpatia
ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake mapya kwa maendeleo ya Taifa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (kushoto). Kulia ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
jambo kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda baada ya kumaliza mafunzo kwa
watumishi wa ofisi hiyo yaliyolenga kuwajengea uwezo katika Mji wa Serikali
Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha wakati wa kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda (kulia)akipokea keki alipokuwa akiagwa na Watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji wa Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda ambaye kwa sasa ni Katibu wa Tume ya Utumishi
wa Umma akikata keki akiwa anaagwa na watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
jijini Dodoma
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa
Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco
Kipanda akitoa neno la shukrani
kwa Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI alipokuwa
akiwaaga katika ofisi hiyo Mji wa Serikali
Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye
ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda (hayupo pichani) wakati akitoa neno
la shukrani kwa Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
alipokuwa akiwaaga baada ya kupata teuzi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Musa Magufuli akimlisha keki aliyekuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipandabaada ya kutoa neno la shukrani kwa
Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI alipokuwa akiwaaga
baada ya kupata teuzi hiyo.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi
(hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha wakati wa kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa
Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco
Kipanda.
SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATUMISHI WA UMMA KUPITIA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI
Na. Antonia Mbwambo- Mbeya
Tarehe 29
Juni, 2026
Serikali
imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wa Umma kupitia
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi, hatua inayolenga kuongeza
ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute,
wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi katika Shule za Msingi
Ngolela, Wilaya ya Kyela na Idweli, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya,
iliyohusisha wataalamu kutoka Ofisi hiyo pamoja na Watumishi Housing Investments
(WHI).
Bw.
Allute amesema makazi bora yataongeza ari ya kazi kwa Walimu na kuboresha
utoaji wa huduma. Aidha, amewataka Watumishi watakaonufaika na nyumba hizo
kuzitunza vizuri mara zitakapokamilika kwa kuwa ni mali za umma na zinazopaswa
kudumu ili kuwanufaisha Watumishi wa baadae.
"Serikali
inaendelea kuwekeza fedha nyingi katika kuboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi
wa Umma, hivyo ni wajibu wa kila mnufaika kuhakikisha nyumba hizi zinatunzwa
vizuri mara zitakapokamilika na kuanza kutumika ili ziendelee kuhudumia
watumishi wa sasa na wa baadae," Bw. Allute amesema
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bi. Julieth Magambo, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika ujenzi wa
nyumba za watumishi ili kuhakikisha wanapata mazingira bora, salama na yenye
utulivu yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Awali,
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye, ameishukuru
Serikali kwa mradi huo, huku akieleza kuwa nyumba zilizopo zimechakaa na
hazifai kwa matumizi, hali iliyowalazimu Walimu wengi kuishi mbali na shule.
Naye
Mwalimu wa Shule ya Msingi Idweli, Bw. Tejile Mathew, amesema kukamilika kwa
nyumba hizo kutaleta motisha ya kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma ya Elimu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitaka ufafanuzi wa jambo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti,Bi Julieth Magambo wa Ofisi hiyo.
Muonekano wa mbele wa jengo la
mradi wa makazi ya watumishi wa umma wa Shule ya msingi
Ngolela, iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye (wanne kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha
Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa kwanza kutoka kulia) wakati wa ukaguzi
wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya msingi
Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa mbele wa jengo la
zamani walilokuwa wakiishi Waalimu wa shule ya msingi Ngolela iliyopo Kyela
Mkoani Mbeya kabla ya jengo hilo kuchakaa na kushindwa kutumika kwa makazi
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing
Investment (WHI) ikiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Ngolela, Bw. Samsoni Anyosisye (wanne kutoka kushoto) mara baada ya timu
hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Shule ya
msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa nyuma wa jengo la
zamani walilokuwa wakiishi Waalimu wa shule ya msingi Ngolela iliyopo Kyela
Mkoani Mbeya kabla ya jengo hilo kuchakaa na kushindwa kutumika kwa makazi
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing
Investment (WHI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi
Idweli, Bw. Tejile Mathew pamoja na mafundi wanaosimamia mradi huo mara baada
ya timu hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa
Shule ya msingi Ngolela iliyopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya
Muonekano wa mbele wa jengo la
mradi wa makazi ya watumishi wa umma wa Shule ya msingi Idwelu,
iliyopo Wilaya ya Rugwe Mkoa wa Mbeya
UZINGATIAJI WA ITIFAKI KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA UADILIFU KIUTENDAJI
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Katibu Mkuu ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuzingatia Itifaki
katika Utumishi wa Umma ili kuongeza uwajibikaji na uadilifu kiutendaji kwa maslahi mapana ya Taifa.
Bw. Mkomi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa
ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo
kwa watumishi hao mara baada ya mkufunzi aliyekuwa akitoa mafunzo kuhusu
Itifaki kuhitimisha mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wa
Itifaki katika Utumishi wa Umma.
Akiwasilisha mada kuhusu Itifaki, Mwezeshaji wa Mafunzo, Mhadhiri wa Diplomasia, kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Lucas Humo amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua wajibu wake ili aweze kuwahudumia Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa kuzingatia Itifaki mbalimbali zitakazosaidia kuonesha taswira nzuri ya ofisi.
Aidha, Bw. Humo amesema, Itifaki inahusisha namna inavyopaswa kuwasiliana, kushirikiana, na
kufanya maamuzi kwa njia inayoheshimu sheria na taratibu zilizowekwa.
“Watumishi wa umma
wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uadilifu na uwazi kwa namna
ya kuwasiliana, kushirikiana na kufanya maamuzi hivyo, wakifuata Itifaki na
kuzitekeleza kwa ufanisi itaboresha utendaji kazi”, amesema Bw. Humo.
Bw. Humo, amewaasa
watumishi hao kutunza taarifa za ofisi, kuzingatia muda wa kazi wakati wa
kuingia na kutoka, kuwajali wageni wanapowasilisha masuala yao ya kiutumishi, kuzingatia
mavazi wanapokuwa katika eneo la kazi pamoja na kuwatambua wageni wanapofika
katika ofisi hiyo kwa vyeo vyao ili kutoa huduma kwa haki na usawa.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Bw. Juma Mkomi akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma.
Mhadhiri
wa Diplomasia, kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed
Salim, Bw. Lucas Humo akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Itifaki wakati
wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma. Wanaomsikiliza ni Wakurugenzi na Watumishi wa
ofisi hiyo.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini
Dodoma.
Sehemu ya Viongozi, Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki
wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mhadhiri wa Diplomasia, kutoka
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Lucas Humo (kulia)
akionyesha kwa vitendo Itifaki ya kusalimiana wakati wa mafunzo kwa watumishi
wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha
utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa
Umma, Bw. Nolasco Kipanda.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada kuhusu Itifaki
wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi
kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Joyce Atanas akiuliza swali kuhusu Itifaki mara baada ya Mhadhiri
wa Diplomasia, Bw. Lucas Humo (hayupo pichani) kuwasilisha mada kuhusu Itifaki
mbalimbali katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyolenga kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali
Mtumba, jijini Dodoma.
Sunday, June 28, 2026
TIMU YA WATAALAMU OFISI YA RAIS - UTUMISHI NA WATUMISHI HOUSING INVESTMENTS (WHI) YAFANYA UKAGUZI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUANGWA NA MASASI.
Timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments (WHI) ipo katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi ambapo leo tarehe 28 Juni, 2026 imekagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa nyumba ya Watumishi 6:1 katika Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan - Ruangwa, pamoja na mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi 3:1 katika Kituo cha Afya Mtandi , Masasi-Mtwara
Saturday, June 27, 2026
TIMU YA WATAALAMU OFISI YA RAIS - UTUMISHI NA WATUMISHI HOUSING INVESTMENTS (WHI) YAENDELEA NA UKAGUZI WA UTEKELEZAJI MIRADI
Timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments (WHI) imeendelea na ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi katika Mkoa wa Lindi ambapo leo tarehe 27 Juni, 2026 imekagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za Watumishi katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu, Shule ya Sekondari Matanda, Shule ya Msingi Runyu, Kituo cha Afya Mvuleni na Shule ya Sekondari Mvuleni.
Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikikagua ubora wa kazi
za ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu, Wilaya ya
Kilwa, Mkoani Lindi leo tarehe 27 Juni 2026
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.
Patrick Allute (aliyenyoosha mkomo) akijadili jambo na Wataalamu kutoka Ofisi
hiyo na Watumishi Housing Investments (WHI) mara baada ya kukagua utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Shule ya Sekondari Mvuleni iliyopo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Mkoa wa Lindi
Muonekano wa mbele wa jengo la mradi
wa makazi ya Watumishi wa Umma wa
Kituo cha Afya Mvuleni kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi.
Muonekano wa ndani wa jengo la mradi
wa makazi ya Watumishi wa Umma wa
Kituo cha Afya Mvuleni kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi.
Timu ya wataalam
kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments ikiongozwa na Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Patrick Allute kukagua mradi wa
maendeleo wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mvuleni kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi.
Mhandisi Salum Chanzi kutoka Watumishi Housing Investments (wa nne kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mvuleni kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi






.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


