Tuesday, June 23, 2026

TIMU YA OFISI YA RAIS–UTUMISHI YAKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI DODOMA


Na Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 24 Juni, 2026

Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais–UTUMISHI kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investment imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi awamu ya pili katika Wilaya ya Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na ratiba iliyopangwa.

Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute, ambaye amesema Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bw. Allute amesisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi, matumizi sahihi ya rasilimali za umma na ukamilishaji wa kazi kwa wakati huku viwango vya ubora vikizingatiwa. Aidha, ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi na wakandarasi kushughulikia kwa haraka changamoto zilizobainika ili kuhakikisha malengo ya miradi hiyo yanafikiwa kama ilivyopangwa.

Ziara hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.

Katika ukaguzi huo, timu imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya Hombolo, Shule ya Sekondari Mtemichiloloma, Kituo cha Afya Mkonze na Shule ya Sekondari Bihawana, ambapo imejionea maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na imefanya majadiliano na wasimamizi pamoja na wakandarasi kuhusu hatua zilizofikiwa na changamoto zinazojitokeza.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya wataalamu wa ukaguzi wa miradi  mara baada ya  timu hiyo kukagua mradi wa ujenzi wa
 nyumba ya Watumishi  katika kituo cha Afya Mkonze , mtaa wa hospitali Mkoani Dodoma

Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma lililopo katika Kijiji cha hospitali, kata ya Mkonze,Wilaya ya Dodoma na Mkoa wa Dodoma.



Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa shule ya sekondari Mtemichiloloma Hombolo
, Mkonze mara baada ya Mkurugenzi huyo na timu ta Wataalamu aliofuatana nao kuwasili katika mradi huo kwa ukaguzi Juni 25, 2026 jijini Dodoma

Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma lililopo mtaa wa Hombolo senta, kata ya Hombolo,Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Wataalamu aliofuatana nao mbele ya jengo la Mradi wa shule ya sekondari Bihawana uliopo Mkonze jijini Dodoma mara baada ya kukagua maendeleo ya Mradi huo Juni 24, 2026


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Mwalimu ambaye ni Mtumishi katika shule ya sekondari Bihawana, Mkonze mara baada ya Mkurugenzi huyo na timu ta Wataalamu aliofuatana nao kuwasili katika mradi huo kwa ukaguzi Juni 25, 2026 jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitaka ufafanuzi wa jambo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya kilichopo mtaa wa Hospitali kata ya Mkonze Mkoani Dodoma  Juni 24,2025  


 Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma wa shule ya sekondari Bihawana lililopo  kata ya Mkonze, Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma

No comments:

Post a Comment