Na
Antonia Mbwambo –Dodoma
Tarehe
3 Juni, 2026
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
Serikalini kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki,
uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria katika Utumishi wa Umma ili kuongeza
ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mhe.
Qwaray ameyasema hayo Juni 3, 2026 wakati akifunga Kikao Kazi cha Wakuu wa
Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi waRasilimaliwatu Serikalini kilichowakutanisha
viongozi kutoka Wizara, Wakala, Taasisi za Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka
za Serikali za Mitaa Jijini Dodoma.
Amesema,
mafanikio ya Serikali yanategemea kwa kiwango kikubwa ubora wa usimamizi wa
rasilimaliwatu.
“Rasilimaliwatu ndiyo injini ya maendeleo ya taifa;
isimamiwe kwa weledi, haki na uwajibikaji.” – Mhe. Regina
Qwaray alisema.
Aidha
Mhe. Qwaray alibainisha kuwa Serikali imeendelea kupokea malalamiko
yanayohusiana na ucheleweshaji wa kupandishwa vyeo, malipo ya stahili za
watumishi na ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi, hivyo kuwataka wataalamu wa
Utawala na Rasilimaliwatu kuwa washauri waaminifu kwa viongozi wao na walinzi
wa utawala wa sheria katika taasisi wanazozihudumia.
Pia
alisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, matumizi salama
ya teknolojia na ulinzi wa taarifa za Serikali, huku akitoa wito kwa waajiri
kuwajengea watumishi uwezo kuhusu matumizi sahihi ya Akili Unde (AI) na mifumo
ya kidijiti.
Katika
kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, aliagiza utekelezaji wa Mfumo wa e-Utendaji
usimamiwe kwa ukaribu zaidi, na kwamba wasimamizi watakaoshindwa kutekeleza
wajibu wao wa kutathmini utendaji wa watumishi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Ameongeza kuwa kufungwa kwa
kikao hicho hakumaanishi mwisho wa juhudi za kuboresha Utumishi wa Umma, bali
ni hatua ya kuanza kutekeleza kwa vitendo maazimio na maelekezo yaliyokubaliwa.
“Kumalizika
kwa kikao hiki si mwisho wa kazi, bali ni mwanzo wa utekelezaji wa maazimio na
maelekezo yaliyotolewa kwa lengo la kujenga Utumishi wa Umma sikivu, jumuishi, na
wenye matokeo,” alisisitiza Mhe. Qwaray.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amesema ni matarajio yake kuwa kikao hicho
kitaleta matokeo chanya kwa viongozi hao yatakayoboresha utekelezaji wa
majukumu na kuongea tija katika utumishi wa umma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray akizungumza katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu (hawapo pichani) wakati Naibu Waziri
huyo alipokuwa akifunga kikao kazi kilicholenga kuimarisha utawala na
usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi wa Ofisi hiyo Bw. Nolasco Kipanda tuzo ya shukrani kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI mstaafu Dkt. Laurean Ndumbaro, kwa kushiriki na kuwasilisha mada katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray,(kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Huma Mkomi, wakati wa kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini Tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray,(kushoto) akisalimiana na viongozi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mabele jijini Dodoma kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi hiyo, mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2023 jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi hiyo, mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2023 jijini Dodoma
Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2023 jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya watumishi kutoka Ofisi hiyo, mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (wa pili kushoto) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Taasisi ya Uongozi Bw. Deo Usangira tuzo ya shukrani kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Kadari Singo kwa kushiriki na kuwasilisha mada katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini jijini Dodoma
Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akimkabidhi Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kwa kushiriki katika mkutano wa Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini leo Tarehe 3 Juni, 2023 jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment