Friday, January 27, 2017

WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA WAKALA ZA SERIKALI, AZITAKA ZIFANYE KAZI NA KUJITEGEMEA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini leo jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali leo jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Dkt. Jabiri Bakari akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali leo, jijini Dar es salaam.

Washiriki wa mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala hizo nchini leo, jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini leo, jijini Dar es salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisikiliza mada pamoja na washiriki wengine wakati wa mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini, uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Thursday, January 26, 2017

Pongezi





Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inampongeza Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma Bw.Nyakimura Muhoji kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tuesday, January 24, 2017

IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA YAFANYA UKAGUZI WA HALI YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KATIKA OFISI ZA MAMLAKA YA MAPATO MKOANI MBEYA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Charles G. Magaya (aliyevaa koti la kijivu) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya kuhusu namna bora ya Utunzaji wa Kumbukumbu za ofisi alipofanya ziara ya kikazi kujionea hali ya utunzaji kumbukumbu mkoani humo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Charles G. Magaya akikagua utunzaji wa kumbukumbu katika masijala ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kikazi kujionea hali ya utunzaji kumbukumbu mkoani humo.


Monday, January 23, 2017

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAHAMIA RASMI MAKAO MAKUU YA NCHI - DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwatakia watumishi wake safari njema ya kuhamia Makao Makuu ya nchi - Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipunga mkono kwa madereva wa magari yaliyobeba vitendea kazi vya Ofisi  vinavyohamishiwa  Makao Makuu ya nchi - Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakitawanyika baada ya kuagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kwa safari ya kuhamia Makao Makuu ya nchi- Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya habari kuhusu ofisi yake kuhamia rasmi Makao Makuu ya nchi - Dodoma. Kushoto kwake Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya habari kuhusu ofisi yake kuhamia rasmi Makao Makuu ya nchi - Dodoma. 

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipokuwa akizungumza nao kuhusu ofisi yake kuhamia rasmi Makao Makuu ya nchi - Dodoma. 




Thursday, January 19, 2017

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa yatembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa walipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akitoa neno la utangulizi wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw.  Peter Ilomo akitoa maelezo ya namna  Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) unavyotekeleza majukumu yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa makini.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Bi. Haighat Kitala akifafanua majukumu ya ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua majukumu ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw.  Peter Ilomo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kumaliza kikao cha kupokea taarifa ya kiutendaji ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).

Monday, January 16, 2017

TANZIA


Misa ya kuaga mwili wa Mkurugenzi mstaafu Bw. Emmanuel Mlay kufanyika leo nyumbani kwake Banana-Ukonga, Dar es salaam. 

Hadi anastaafu Bw. Mlay alikua ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimali Watu katika Utumishi wa Umma-DHCM. Mazishi yatafanyika Moshi-Kilimanjaro.

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la Milele.


Tuesday, January 10, 2017

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO YA KIKAZI NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea kitabu kilichojikita katika Tafiti ya Kazi za Sanaa za Tanzania kutoka kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea  Waziri huyo ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea ofisini kwake. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli (kulia) alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake . Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa ubalozi wa Uswisi nchini Bi. Romana Tadeschi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli (hayupo pichani) alipotembelewa na Balozi  huyo ofisini kwake.

Friday, January 6, 2017

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO YA KIKAZI NA KAMISHNA WA MAADILI KATIKA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Reginald Nsekela akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela (wa pili kulia) alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela (hayupo pichani) alipotembelewa na Kamishna huyo ofisini kwake.