Tuesday, August 30, 2022

DKT. NDUMBARO AELEKEZA MWONGOZO WA MPANGO WA URITHISHANAJI MADARAKA UBORESHWE KUENDANA NA DHAMIRA YA MHE. RAIS YA KUUJENGA UTUMISHI WA UMMA WENYE UADILIFU NA UWAJIBIKAJI

 Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 30 Agosti, 2022 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ameelekeza Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2011 uboreshwe ili kuendana na dhamira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu, nidhamu na unaowajibika kwa hiari kwa wananchi katika kutoa huduma bora. 

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo leo jijini Dodoma, wakati akifungua kikao kazi cha wadau cha kujadili Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji madaraka katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Dkt. Ndumbaro amesema, mwongozo huo ni vema ukaainisha taratibu zitakazowezesha urithishanaji wa madaraka kwa viongozi wenye uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi ili watoe mchango katika maendeleo ya taifa na uweke misingi madhubuti ya kuwa na Utumishi wa Umma wenye kuwajibika, uzalendo wa kitaifa na moyo wa kujitolea. 

“Mwongozo ujenge mazingira wezeshi ya kuwa na watumishi wa umma wanaowajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora, wanaowajibika kwa kuzingatia taaluma, wanaowajibika kwa wanaowasimamia na kwa viongozi,” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wanaoshiriki kujadili mwongozo huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Marko Masaya amemhakikishia Dkt. Ndumbaro kuwa, watawasilisha maoni na mapendekezo ambayo yatawezesha kuandaa Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma ambao utaliwezesha taifa kuwa na mpango mzuri wa kurithishana madaraka.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Edith Rwiza amesema Serikali imekuwa ikitumia Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 11 sasa, ambapo kumekuwa na mabadiliko na changamoto mbalimbali za kimenejimenti na za kiutumishi, hivyo mamlaka imeelekeza kuupitia upya mwongozo huo wa mwaka 2011 ili kuona kama unahitaji maboresho, au kuhuishwa au kuandikwa upya ili kuendana na mahitaji.

Kikao kazi hicho kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kimehudhriwa na wadau kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na wadau walioshiriki kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma kilichofanyika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.


Sehemu ya wadau kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma kilichofanyika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Edith Rwiza akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) kufungua kikao kazi cha wadau kujadili Mwongozo wa Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma kilichofanyika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. 



Afisa Utumishi Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Judith Shoo akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Mpango wa Urithishanaji Madaraka wakati wa kikao kazi cha kujadili mwongozo huo kilichowashirikisha wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali kilichofanyika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.


Mshiriki wa kikao kazi cha kujadili mwongozo wa urithishanaji madaraka katika utumishi wa umma, Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya usimamizi wa Rasilimaliwatu-TAMISEMI, Bw. Marko Masaya akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha kujadili mwongozo wa urithishanaji madaraka katika utumishi wa umma mara baada ya kufungua kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

 


 



 

Saturday, August 27, 2022

WAZIRI JENISTA AFANYA KIKAO KAZI NA WAKUU WA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YAKE.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya ofisi yake wakati wa kikao kazi chake na wakuu hao kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika jijini Dodoma.

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika jijini Dodoma.

 

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Dkt. Seraphia Mgembe akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia moja ya taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao kazi chake na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika jijini Dodoma.

 








Monday, August 22, 2022

MHE. JENISTA AMTEMBELEA MAMA FATMA KARUME KUMJULIA HALI IKIWA NI SEHEMU YA KUTAMBUA MCHANGO ALIOUTOA KATIKA TAIFA MAELEZO YA PICHA




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mama Fatma Karume alipomtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango alioutoa katika taifa.

 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha salamu za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mama Fatma Karume alipomtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango alioutoa katika taifa.

 

Mama Fatma Karume (katikati) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na watendaji alioambatana nao, wakati waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango alioutoa katika taifa.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na baadhi ya watendaji wa ofisi yake, wakimsikiliza Mama Fatma Karume (hayupo pichani) walipomtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar.

Mama Fatma Karume akimuonesha shamba lake la migomba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, mara baada ya waziri huyo kumtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na Mama Fatuma Karume mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango alioutoa katika taifa.

 

 

Mama Fatma Karume akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, mara baada ya waziri huyo kumtembelea nyumbani kwake Bumbwini Zanzibar.