Na. James K. Mwanamyoto-Bagamoyo
Tarehe 03 Agosti, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ameridhishwa na namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Nia Njema wilayani Bagamoyo walivyoboresha maisha yao kupitia ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mhe. Mhe. Ndejembi amesema hayo leo wakati akizungumza na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Nia Njema wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utelekezaji wa mpango huo wilayani humo.
Mhe. Ndejembi amesema mafanikio waliyoyapata walengwa hao kwa kujishughulisha na masuala mbalimbali ya ujasiriamali ikiwemo ushonaji wa nguo, ususi wa mikeka, vikapu, ufugaji wa kuku na kilimo yanaendana na lengo la Serikali la kuinua uchumi wa wananchi wake kupitia TASAF.
“Mafanikio mliyoyapata kupitia TASAF yanafurahisha sana na yanampa nguvu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuiwezesha TASAF ili wananchi wengi waendelee kunufaika na kuboresha maisha yao,” Mhe. Ndejembi ameongeza.
Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka walengwa wa TASAF kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo ikiwemo ya miradi inayotekelezwa na TASAF.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, walengwa wa TASAF wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa wengine kushiriki zoezi la Sensa ili Serikali ipate idadi kamili ya watu na kupanga mipango yake ya maendeleo.
Akizungumzia namna TASAF ilivyoboresha maisha yake, mmoja wa walengwa wa TASAF, Bibi Elizabeth Stephen ameishuru Serikali kwa kumpatia ruzuku inayomuwezesha kulea watoto wake wawili wenye ulemavu, kufuga kuku na kufungua genge ambalo linamuingiza kipato kinachoendesha maisha yake.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akizungumza na mlengwa wa TASAF wa Kijiji cha Nia
Njema anayejishughulisha na ushonaji wa nguo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini Wilayani Bagamoyo.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akisisitiza jambo kwa walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Nia Njema
(hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Bagamoyo.
Walengwa
wa TASAF wa Kijiji cha Nia Njema wilayani Bagamoyo wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri
huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini Wilayani ya Bagamoyo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Nia Njema
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Bagamoyo.
Mlengwa
wa TASAF wa Kijiji cha Nia Njema Wilayani Bagamoyo, Bibi Elizabeth Stephen
akitoa ushuhuda kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) jinsi
alivyoboresha maisha yake kupitia TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini Wilayani Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment