Thursday, December 31, 2020

MHE. NDEJEMBI AENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA NA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA TAASISI ZAKE


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)     Bw. Ladislaus Mwamanga alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi aliyoifanya katika Taasisi hiyo Jijini Dodoma kwa lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakati wa ziara yake ya kikazi katika taasisi hiyo yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.

 

 

MHE. NDEJEMBI AENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA NA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA TAASISI ZAKE



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi aliyoifanya leo katika Mamlaka hiyo Jijini Dodoma kwa lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifuatilia historia ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Jabiri Bakari wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari akimwonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kitabu chenye taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka yake wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi aliyoifanya katika Mamlaka hiyo Jijini Dodoma kwa lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuhimiza uwajibikaji.










 

Tuesday, December 29, 2020

MHE. NDEJEMBI AHIMIZA UTUNZAJI WA NYARAKA KATIKA TAASISI ZA UMMA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifuatilia taarifa kuhusu mifumo ya kuhifadhi nyaraka iliyokuwa ikiwasilishwa na Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji. 


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Salum Kyando akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi katika Idara hiyo Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji. 

 

MHE. NDEJEMBI AWATAKA MKURABITA KUONGEZA KASI YA URASIMISHAJI ILI KUEPUKA MIGOGORO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Dkt. Seraphia Mgembe Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji. 


Baadhi ya Watumishi wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi katika taasisi hiyo leo Jijini Dodoma yenye lengo la kufahamiana na watumishi hao na kuhimiza uwajibikaji.

 

Wednesday, December 23, 2020

TAASISI YA UONGOZI YATAKIWA KUWAPIKA VIONGOZI WA AINA ZOTE BILA KUJALI TOFAUTI ZAO

Na James Mwanamyoto - Dar es Salaam

Tarehe 23 Desemba

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameitaka Taasisi ya Uongozi kuwaandaa Viongozi wa aina zote bila kujali tofauti zao ili waweze kutoa mchango katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kufahamiana na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa taasisi hiyo.

Mhe. Ndejembi amesema Taasisi ya Uongozi ikijikita katika kuwaandaa viongozi bora itakuwa ni taasisi ya mfano na kuigwa Barani Afrika jambo ambalo litaleta sifa nzuri kwa nchi yetu.

“Taasisi ya uongozi ikifanikiwa kuwaandaa viongozi bora nchini, itawawezesha Watanzania popote walipo kujivuna kwa kuwa na taasisi yenye mchango mkubwa wa kutoa mafunzo kwa watu waliopewa mamlaka ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo”, Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewahimiza watumishi wa Taasisi ya Uongozi kuwa na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

Akiwasilisha utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo amesema taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo ya viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam kuzisaidia taasisi na viongozi wake kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi ilianzishwa Julai, 2010 lengo likiwa ni kuwa na Kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza Viongozi Barani Afrika kwa kuanzia Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Uongozi (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi aliyoifanya leo katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifuatilia historia ya Taasisi ya Uongozi iliyokuwa ikiwasilishwa leo na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Watumishi wa Taasisi ya Uongozi, wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi wakati wa ziara yake ya kikazi leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


 

Tuesday, December 22, 2020

WATUMISHI HOUSING YATAKIWA KUTUMIA ‘FORCE ACCOUNT’ KATIKA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA ILI KUWAWEZESHA WATUMISHI KUPANGA NA KUNUNUA NYUMBA





Na James Mwanamyoto - Dar es Salaam

Tarehe 22 Desemba, 2020.

 

Watumishi Housing Company imetakiwa kuacha kuendelea kutumia Wakandarasi katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia na kuwapangisha Watumishi wa Umma na badala yake watumie ‘force account’ ili kuokoa gharama na kujenga nyumba ambazo watumishi wataweza kupanga na kuzinunua.

Maelekezo hayo yametolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Watumishi Housing Company ikiwa ni pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Mhe. Ndejembi amesema madhumuni ya kuanzishwa kwa Watumishi Housing Company ni kujenga nyumba za gharama nafuu zinazoweza kununuliwa na Watumishi wa kada zote, hivyo hakuna sababu ya kutumia wakandarasi ambao gharama zao za ujenzi ni kubwa na kusababisha gharama kubwa za upangishaji na uuzaji wa nyumba hizo.

“Watumishi wa Umma wanajitoa sana katika kulitumikia taifa hili, sasa ni wakati wa Serikali kutambua mchango wao kwa kuwawezesha ikiwa ni pamoja na kuwapatia nyumba za gharama nafuu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, kuna majengo mbalimbali ya Serikali yaliyojengwa kwa ubora kwa kutumia ‘force account’ na kutolea mfano wa baadhi ya majengo hayo ambayo yako katika Mji wa Serikali-Mtumba kuwa ni TARURA na TAMISEMI.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa amesema wamepokea maelekezo ya Mhe. Naibu Waziri ya kutumia ‘force account’ na wameshajiandaa kwa ajili ya hilo.

Ameongeza kuwa, walishaanzisha Kampuni ndani ya Watumishi Housing ambayo imetumika kujenga nyumba 61 na nyingine wanatarajia kuzijenga Jijini Dodoma na Mwanza na maeneo mengine nchini.

Ujenzi wa miradi ya nyumba za Watumishi Housing kwa kutumia force account itahusisha njia ya ununuzi wa kazi ya ujenzi kwa kutumia taasisi ya umma au watumishi wake na vifaa au wafanyakazi wa kukodi, njia ambayo itawezesha Watumishi wa Umma kupanga au kununua nyumba kwa gharama nafuu.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Watumishi Housing Company ikiwa ni pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoka kukagua moja ya nyumba za Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Watumishi Housing Company ikiwa ni pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa alielezea namna watakavyotekeleza maelekezo ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ya kutumia ‘force account’ kwenye miradi ya ujenzi wa nyumba za kupangisha na kuwauzia Watumishi wa Umma kwa bei nafuu wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Watumishi Housing Company ikiwa ni pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

 


Mradi wa nyumba za Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole-Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

 

WATUMISHI SEKRETARIETI YA AJIRA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU ILI KUTENDA HAKI KWA WAOMBAJI WA AJIRA


Na. James K. Mwanamyoto – Morogoro

Tarehe 22 Disemba, 2020


Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na uwajibikaji ili kutenda haki kwa kila mwombaji wa ajira Serikalini ambaye ana sifa za kupata kazi kwa mujibu wa nafasi husika zinazotangazwa na Taasisi mbalimbali za umma.

Wito huo umetolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kilichofanyika mjini Morogoro.

Mhe. Mkuchika amewasisitiza watumishi hao kuendelea kuzingatia Uadilifu, Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma nchini kwani kazi wanayoifanya ni nyeti na inagusa maisha ya watu, hivyo inahitaji watu waadilifu, wapenda haki na ambao ni mfano wa kuigwa na jamii kwa uadilifu.

Akizungumzia utoaji wa huduma kwa wateja, Mhe. Mkuchika amesema, ni muhimu watumishi wa Sekretarieti ya Ajira kuwahudumia wateja wao kwa lugha nzuri kwani ndio nyenzo muhimu katika utoaji wa ajira.

“Tumieni lugha nzuri na zenye staha kwa kuwasikiliza na kuwahudumia vizuri wateja wenu kwani nyie ndio lango kuu la kuingiza watu katika Utumishi wa Umma, hivyo mienendo yenu ndio picha ya aina ya watumishi watakaopatikana kwa ajili ya kuja kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayofanywa na Serikali”, Mhe. Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika amewahimiza watumishi hao, kufanya kazi kwa kushirikiana na waajiri kwani jukumu walilopewa la kuendesha mchakato wa ajira ni kwa niaba ya waajiri hivyo ni muhimu wakashirikiana kuhakikisha mchakato wa ajira unakwenda vizuri na kwa wakati na hatimaye kupata watumishi wenye sifa stahiki ambao watalisukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa kwa kasi zaidi.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka watumishi wa Sekretarieti ya Ajira kurahisisha mchakato wa ajira kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuchuja waombaji wa kazi, hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais kuhimiza matumizi ya TEHAMA ikizingatiwa kuwa, suala hili amelipa uzito mkubwa mpaka kuliundia Wizara.

Akizungumzia kuhusu matumizi ya TEHAMA, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema, Mifumo ya TEHAMA imeiwezesha ofisi yake kuthibiti matumizi ya vyeti vya kughushi katika uendeshaji wa mchakato wa ajira Serikalini kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine zenye dhamana katika sekta za elimu na mafunzo katika zoezi la uhakiki.

Bw. Daudi ameongeza kuwa, kupitia mifumo ya kiutendaji ya TEHAMA wamewawezesha waombaji kazi kupata na kufuatilia taarifa za matangazo ya kazi kupitia teknolojia rahisi ya simu za kiganjani popote alipo mteja ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo imewapunguzia adha wafuatiliaji wa fursa za ajira kwani taarifa zinawafakia popote walipo.

Kuhusiana na suala la uadilifu, Bw. Daudi amesema Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imejiwekea malengo kuhakikisha wanaoajiriwa  katika Taasisi za Umma wanakuwa na sifa ya uadilifu na uwajibikaji.

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kilichofanyika jana mjini Morogoro.




Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kilichofanyika jana mjini Morogoro.



Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Hayupo pichani) kabla ya Waziri huyo kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kilichofanyika jana mjini Morogoro.


Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika mara baada ya Waziri huyo kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jana mjini Morogoro.


 

Monday, December 21, 2020

TATIZO LA WATUMISHI KUKAIMU NAFASI ZA UONGOZI KWA MUDA MREFU LINATOKANA NA WAAJIRI KUTOZINGATIA TARATIBU

 

Na. James K. Mwanamyoto – Morogoro

Tarehe 21 Disemba, 2020

Tatizo la Watumishi wa Umma kukaimu nafasi za uongozi kwa muda mrefu bila kupata stahili ya vyeo wanavyokaimishwa, linatokana na waajiri kutozingatia taratibu za kiutumishi pindi wanapowakaimisha watumishi hao kama Waraka wa Utumishi Namba 2 wa Mwaka 2018 unavyoelekeza.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Morogoro na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika alipoitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.

Mhe. Mkuchika amesema, kumekuwa na tabia ya Waajiri wengi hususan katika halmashauri kuwakaimisha watumishi ambao hawana sifa za kukaimu wala kibali cha kukaimu ambacho kinatolewa na Katibu Mkuu - UTUMISHI.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, ili mtumishi aweze kukaimu, anapaswa kuwa na cheo cha Afisa Mwandamizi na kuendelea na pia awe amepatiwa kibali cha kukaimu nafasi husika na Katibu Mkuu- UTUMISHI ambacho atakitumikia kwa miezi isiyozidi 6 kabla ya kithibitishwa rasmi iwapo atakidhi vigezo vya kukitumikia cheo hicho.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, kitendo cha Watumishi kukaimishwa bila kufuata taratibu kimekuwa ni chanzo cha malalamiko ya watumishi wengi, hivyo amewataka Waajiri kuzingatia taratibu ili kuepuka malalamiko ambayo yanashusha morali ya utendaji kazi.

Wakati huo huo, Mhe. Mhe. Mkuchika amewataka Waajiri kuhakikisha wanawawezesha wastaafu kupata mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu ili kuwaondolea usumbufu wa wa kufuatilia mafao yao pindi wanapostaafu ikizingaatiwa kuwa wamelitumikia taifa kwa bidii na uadilifu.

Mhe. Mkuchika amesema, ili Wastaafu wapate mafao kwa wakati, Maafisa Utumishi wanapaswa kufanya maandalizi kwa kukusanya vielelezo vyote vinavyohitajika mapema miezi 6 kabla.

"Kutokana na changamoto hii, nitafanya mkutano na Maafisa Utumishi nchi nzima kama nilivyoahidi hapo awali ili kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu suala hili,” Mhe. Mkuchika amesisitiza

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekekezaji ya Mkoa wa Morogoro, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alimwambia Mhe. Waziri kuwa, pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana katika Mkoa wa Morogoro, Ofisi yake ina changamoto ya watumishi kukaimu kwa muda mrefu na wastaafu kutokapata mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Morogoro (hawapo pichani) alipoitembelea Ofisi hiyo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.



Baadhi ya Watendaji wa Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) alipoitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Ole Sanare akielezea changamoto za kiutumishi za Mkoa wake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika, alipoitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, alipoitembelea Ofisi hiyo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.





 

Friday, December 18, 2020

MILIONI 569 ZA TASAF KUWANUFAISHA WANANCHI WILAYANI CHATO KWA KUJENGA KITUO CHA AFYA

 

Na. James K. Mwanamyoto – Chato

Tarehe 19 Disemba, 2020

Wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi na maeneo ya jirani Wilayani Chato watanufaika na huduma za afya zitakazotolewa katika Kituo cha afya cha Nyabilezi baada Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuchangia kiasi cha shilingi milioni 569 kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika amesema kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na TASAF kitakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya.

Kutokana na umuhimu wa kituo hicho, Mhe. Mkuchika amewahimiza Viongozi Wilayani Chato kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha afya ifikapo tarehe 30 Machi, 2021 kama ilivyopangwa ili wananchi wapate huduma ya afya inayostahili.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nyabilezi kwa kutoa mchango wa fedha na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa kuchota maji, kusomba mchanga, kokoto na mawe.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia TASAF kwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho kikikamilika kitakuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za afya katika Kijiji cha Nyabilezi na maeneo jirani.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Kalemani amemuomba Mhe, Mkuchika kupitia TASAF kujenga kituo kingine cha afya katika Kijiji cha Makurugusi ili kupunguza msongamano wa wananchi watakaofuata huduma za afya katika Kituo cha Nyabilezi.

Awali, Kituo cha Afya cha Nyabilezi kata ya Bukome kilikuwa ni Zahanati, hivyo kutokana na umuhimu wa huduma za afya katika kata hiyo, TASAF imetoa kiasi cha fedha cha shilingi milioni 569 ili kukidhi uhitaji wa huduma za afya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi na maeneo ya jirani Wilayani Chato watakaonufaika na huduma za afya zitakazotolewa katika Kituo cha afya cha Nyabilezi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi.



Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi na maeneo ya jirani Wilayani Chato wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Nyabilezi Wilayani Chato. 


Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato, Dkt. Benedicto Ngaiza akisoma taarifa ya ujenzi wa Kituo cha afya cha Nyabilezi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika alipotembelea kituo hicho ili kukagua maendeleo ya ujenzi.


Kaimu Mtendaji Mkuu wa TASAF, Bw. Paul Kijazi akielezea mchango wa TASAF katika ujenzi unaoendelea katika kituo cha Nyabilezi Wilayani Chato. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi.


Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akimshukuru Mhe. Mkuchika kwa taasisi yake ya TASAF kutoa mchango katika ujenzi wa kituo cha afya cha Nyabilezi Wilayani Chato. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi.


Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi, akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi na maeneo ya jirani mara baada ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha afya cha Nyabilezi Wilayani Chato.

 


CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUJENGA KAMPASI KANDA YA ZIWA ILI KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI NA WANANCHI

 

Na. James K. Mwanamyoto – Chato

Tarehe 19 Disemba, 2020

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kiko mbioni kujenga kampasi Wilayani Chato, Mkoani Geita itakayotoa fursa ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma na wananchi wa Kanda ya Ziwa.

Akikagua eneo litakalojengwa Kampasi hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika ameridhika na eneo lililotengwa kwani ni rafiki kwa usalama na utoaji wa elimu.

Mhe. Mkuchika amesema, Kanda ya Ziwa pekee ndiyo ilikuwa haijabahatika kuwa na Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo fursa hii ni muafaka na itakuwa na manufaa kwa Watumishi wa Umma na wakazi wa eneo la Kanda hii.

Akizungumzia uamuzi wa kujenga Kampasi hiyo Wilayani Chato, Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Chato imetoa kiwanja hicho bure tofauti na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa ambayo yangekigharimu Chuo fedha nyingi kununua kiwanja.

Mhe. Mkuchika ameishukuru halmashauri kwa kutoa kiwanja na kumhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati kwani Chuo kiko tayari kuanza ujenzi mapema iwezekavyo.

Naye Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika amewathibitishia wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa, fedha za kuanza ujenzi zimeshapatikana, hivyo kinachosubirikiwa ni hati.

“Tukikabidhiwa hati ya kiwanja, tutaanza ujenzi wa madarasa mapema iwezekanavyo ili wakazi wa Kanda ya Ziwa wanufaike na huduma zinazotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma kama ilivyo katika Kanda zingine,” Dkt. Shindika amesisitiza.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani amemtaka Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo kuwasilisha maombi ya kupatiwa umeme katika eneo hilo ili kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa kampasi hiyo.

Mhe. Kalemani ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo itatoa fursa ya mafunzo na ajira kwa wakaohitimu na kuongeza kuwa, chuo kitajengwa eneo ambalo ni salama na kitalindwa kwa ushirikiano wa wananchi.

Akizungumzia eneo ambalo Chuo kitajengwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi amesema, ujenzi wa kampasi hiyo ukikamilika, itakuwa ni chachu ya maendeleo kutokana na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali watakaokuja kupata mafunzo na utavutia uwekezaji.

Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato itakayojengwa eneo la Rubambangwe lenye ekari 41.66 itahudumia Mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akielezea mpango wa kujenga kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Wilayani Chato, Mkoani Geita alipoenda kukagua eneo ambalo Kampasi ya chuo hicho itajengwa. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani na Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.



Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akimuonyesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika mchoro wa Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato inayotarajiwa kujengwa Wilayani humo. Wanaoshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi.


Sehemu ya kiwanja ambayo kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato itajengwa. Wanaoonekana katika picha ni baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika.


Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika kuhusu mchoro wa Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato utakavyokuwa. Miongoni mwa wanaoshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Mhe. Robert Gabriel Luhumbi.

Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akimuahidi Mhe. Mkuchika kuharakisha upatikanaji wa umeme katika eneo ambalo kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato itajengwa.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika na Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani     wakifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo ya ujenzi wa kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Wilayani Chato inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni.


 

Thursday, December 17, 2020

TPSC YAPONGEZWA KWA KUTUMIA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KUJENGA JENGO LITAKALOBORESHA UTOAJI MAFUNZO

 Na. James K. Mwanamyoto – Tabora

Tarehe 17 Disemba, 2020

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimepongezwa kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kujenga jengo la ghorofa mbili lililoanza kutumika kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Umma na Wananchi katika fani mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kwenye Kampasi ya Tabora.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mkoani Tabora na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika mara baada ya kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

Mhe. Mkuchika amesema hatua ya kutumia fedha za ndani kujenga jengo lenye ofisi na madarasa, linapaswa kuigwa na taasisi nyingine za umma ambazo zinaitegemea Serikali kuwapatia fedha kuboresha ofisi zao.

“Kitendo cha kutumia fedha za ndani kwa maendeleo ya taifa ni jambo zuri ambalo Mhe. Rais amekuwa akisisitiza mara kwa mara, hivyo, ujenzi wa jengo hili linanipa ujasiri wa kuwaalika Viongozi wa Kitaifa kulizindua rasmi, huku kipaumbele kikiwa kwa Mhe. Rais mwenyewe,” Mhe. Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, ushirikiano na uadilifu uliopo baina ya Viongozi na Watumishi ndio ulifanikisha kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, hivyo amewataka kuuendelea na utamaduni huo kwa masilahi ya chuo na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika amesema jengo hilo limekamilika na kuanza kutumika kabla ya uzinduzi rasmi ili kuongeza ufanisi kiutendaji na kubaini mapungufu yanayoweza kujitokeza kwa lengo la kuyadhibiti.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo linalojumuisha maktaba, vyumba vya madarasa ya kompyuta, kumbi, madarasa ya kawaida na ofisi za watumishi ulianza tarehe 5 Novemba, 2014 na kukamilika rasmi tarehe 26 Machi, 2020.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) - Kampasi ya Tabora (hawapo pichani) alipoenda kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

1.   

1. Mwonekano wa jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) - Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani.

 

1. 

1.Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo katika moja ya darasa lililopo ndani ya jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) -Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani. 


1.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akishuhudia mpangilio wa vitabu katika maktaba maalum iliyoko kwenye jengo jipya la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) - Kampasi ya Tabora.

1.  Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzani-Kampasi ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) alipoenda kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.



1.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzani-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.



1. Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akiwasilisha kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika taarifa ya mradi wa jengo jipya la TPSC-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jingo hilo.