Monday, June 30, 2025

KATIBU MKUU MKOMI AWAASA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUJITATHMINI WANAPOTOA HUDUMA KWA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kujitathmini wanapotoa huduma za kiutumishi kwa Watumishi wa Umma kutoka katika taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kwa ujumla

Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake, ikiwa ni muendelezo wa mafunzo kwa watumishi hao ambayo hufanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.

“Ofisi yetu inatoa huduma mbalimbali za kiutumishi, ninawaasa mjitathmini kwa namna mnavyotoa huduma kwa Watumishi wa Umma, wadau na wananchi ili tupate mrejesho mzuri kutoka kwao na hatimaye kufikia malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.” amesema Bw. Mkomi.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo Balozi Mhe. Omar Kashera amewataka watumishi hao kutanguliza mbele uzalendo kwa kujenga taswira nzuri ya ofisi hiyo huku akiwataka kufanya maamuzi sahihi pindi wanapowahudumia wateja.

‘’Ili mtoe maamuzi sahihi ni vizuri mkafikiri kwa kina, muwashirikishe watumishi mnaofanya nao kazi ili kupata maamuzi jumuishi yatakayokuwa sahihi kwa maslahi ya Taifa’’ ameongeza Balozi Mhe. Omar Kashera

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama kulia) akiteta jambo na Mwezeshaji wa mafunzo Balozi Mhe. Omar Kashera (aliyesimama kushoto) baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mwezeshaji wa mafunzo Balozi Mhe. Omar Kashera (aliyesimama) akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


 

Monday, June 23, 2025

WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA ATOA WIKI TANO TAASISI ZA SERIKALI KUJIUNGA NA MFUMO UNAOWEZESHA SERIKALI KUWASILIANA

Na Mwandishi Wetu- DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Taasisi za Serikali ambazo hazijajiunga na mfumo wa kielektroni utakaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana (GovESB) kujiunga na mfumo huo ifikapo Julai 30 mwaka huu ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

“Taasisi zote za umma ambazo hazijajiunga na mfumo huu mwisho ni Julai 30 mwaka huu, wote mhakikishe mmejiunga GovESB, huu ni msisitizo ambao ulitolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kila taasisi ipeleke mfumo wake eGA, idadi ya taasisi zilizounganishwa ni chache, hakuna gharama na hutakiwi kupanga bajeti”

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa mfumo huo unafaida kubwa katika utumishi wa umma kwani utasaidia kurahisisha utendaji, kutoa taarifa kwa wakati, kuondoa makosa ya kibinadamu katika kuwahudumia wananchi pamoja na kuwabana wala rushwa. “Nimefurahi kujulishwa kwamba jumla ya mifumo 223 kutoka kwenye taasisi 185 imeunganishwa na kusomana”. 

Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za umma zenye mifumo na zinazoendelea kubuni mifumo zihakikishe mifumo hiyo inasomana na inaweza kubadilishana taarifa kupitia mfumo huo wa GovESB ikiwa ni njia mojawapo ya kuendelea kuboresha huduma za Serikali.

Kadhalika, Mhe. Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kuhakikisha mifumo iliyounganishwa inaendelea kubadilishana taarifa pamoja na kujiridhisha kwa kila anayeingia awe na uwezo wa kuwasiliana na wengine wote waliomo ndani.

Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa watumishi wa umma kuzingatia miiko na maadili ya utumishi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingitia Sera na Sheria kwa manufaa na maendeleo ya Taifa letu.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza sana watumishi wote wa umma nchini, niwahikishie kuwa serikali ya awamu ya sita iko pamoja nanyi, fanyeni hivyo kwa ajili ya manufaa na maendeleo ya Taifa letu”, amesema Mhe. Majaliwa. 

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene amesema Tanzania imetambulika kimataifa ambapo mwaka 2022 Benki ya Dunia ilifanya utafiti kuhusu ukomavu wa matumizi ya teknolojia duniani katika utoaji wa huduma za Serikali na ushirikishwaji wa wananchi.

Amefafanua kuwa ripoti ya utafiti huo iliyotolewa Machi, 2023 ilibanisha kuwa Tanzania imefanikiwa kupanda daraja kutoka kundi B hadi kundi A na kushika nafasi ya 26 duniani, nafasi ya 2 Afrika na nafasi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki.

Katika tukio hilo, Mhe. Majaliwa amezindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB) pamoja na Mfumo wa e-Wekeza unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund).

Siku ya Utumishi wa Umma husherehekewa Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizindua rasmi Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini (Government Enterprise Service Bus-GovESB) katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuzungumza na Watumishi wa Umma na Wananchi wakati alipomwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Chanangali jijini Dodoma.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kumwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma, Juni 23, 2025.  


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitazama nyaraka za Kiutumishi alipotembeleea banda la Ofisi ya Rais-UTUMISHI alipomwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini dodoma. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitembelea mabada  katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasilioano Serikalini Bi. Mary Mwakapenda.

Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais- UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo maalum ya pongezi Afisa TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Bw. Salum Mohamed kwa kushiriki katika usanifu na ujenzi wa Mfumo wa Ubadilishanaji Taarifa Serikalini ((Government Enterprise Service Bus-GovESB) katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.


Watumishi wa Umma na Wananchi wakiwa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.


Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Wengine ni Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo. 

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Wengine ni Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo. 




Sunday, June 22, 2025

HUDUMA ZA KIUTUMISHI ZATOLEWA NA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa suti) akifurahia pongezi kutoka kwa mwananchi aliyefika katika banda la Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. 

Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimhudumia Mtumishi wa Umma aliyefika katika banda la ofisi hiyo kupata huduma za kiutumishi kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho (kushoto) kusaini kitabu cha wageni katika banda la  Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

 

Afisa TEHAMA, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Selemani Sultan akifafanua jambo kuhusu huduma za e-Utendaji kwa Watumishi wa Umma waliofika banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma


Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakitoa fafanuzi mbalimbali kuhusu majukumu ya ofisi hiyo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Anazak walipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Aveline Ilahuka akiwa na Mtumishi wa Umma kutoka Jeshi la Polisi baada ya kumpatia huduma kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.



Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Aristides Masigati akiwahudumia wananchi waliofika katika banda la Ofisi ya Rais-UTUMISHI kupata huduma za kiutumishi wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.


Friday, June 20, 2025

NAIBU WAZIRI SANGU APONGEZA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWA KUWA NA UTAYARI WA KUWAHUDUMIA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Na. Mwandishi Mwetu-Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ametoa pongezi kwa Wizara na Taasisi za Umma kwa kuwa na utayari wa kuwahudumia watumishi wa umma na wananchi katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

“Tumekuwa tukifanya kliniki katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi wa Umma na Wananchi, lakini kupitia Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamekuwa suluhisho kwa kufanya kazi papo kwa hapo kwani  Watumishi wa Umma na Wananchi wamekuja kuhudumiwa kwa wakati,hii inaonesha ni kwa namna gani mmekuwa na utayari wa kutoa huduma bora kwa maslahi ya taifa, hongereni sana,” Mhe. Sangu amesema

Aidha, Mhe. Sangu ametoa rai kwa Watanzania wote kufika katika Viwanja hivyo ili kupata huduma za moja kwa moja na elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara na taasisi za Umma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Sangu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watumishi wa umma nchini kwa kuboresha maeneo yao ya kazi kwa kuwa sehemu salama ili watanzania waweze kupata huduma bora.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (kulia) baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika Viwanja vya Chinangali Park kutembelea mabanda ya Wizara na Taasisi zilizoshiriki Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akisisitiza jambo kwa Maafisa wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea banda la ofisi hiyo Viwanja vya Chinangali Park katika Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Lindi walioshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la ofisi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga na Mloganzila) yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyekaa kushoto) akifurahia kucheza mchezo wa drafti wakati alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Viwanja vya Chinangali Park kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyenyoosha mkono) akisisitiza jambo alipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kulia) akizungumza na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi-Zanzibar walipokuwa wakijitambulisha baada ya kutembelea Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kwemye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akimsikiliza Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bi. Aveline Ombock (aliyeshika kipaza sauti) alipokuwa akielezea namna walivyoshiriki na kutoa huduma kwa wananchi katika Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 inayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kulia) akimsikiliza Afisa Usajili na Udhibiti Ubora-OSHA, Bw. Ramadhani Kajembe alipokuwa akielezea ushiriki wa ofisi hiyo katika Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 inayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akimsikiliza Meneja Utekelezaji Sheria na Kushughulikia Malalamiko (TIRA), Bw. Okoka Jailo alipokuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda hilo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Viwanja vya Chunangali Park jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (anayesaini kitabu) akifurahia jambo wakati alipotembelea banda la ofisi ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya uzalishaji kwa mauzo ya nje (EPZA) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Viwanja vya Chunangali Park jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akimsikiliza Msanifu Majengo, Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Bi. Mariahildagard Byarufu alipokuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda hilo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Viwanja vya Chunangali Park jijini Dodoma.



Thursday, June 19, 2025

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ATOA SHUKRANI KWA USHIRIKI

 Na. Mwandishi Mwetu-Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea mabanda ya Wizara na Taasisi za Umma ili kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hizo pamoja na kutoa shukrani kwa ushiriki mkubwa katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025.

“Ninapongeza na kutoa shukrani nyingi kwa Wizara na Taasisi zote za Umma zilizoshiriki katika Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma, zimeonesha ushirikiano mkubwa na idadi ya ushiriki imekuwa kubwa,” amesema Bw. Mkomi

Bw. Mkomi ameseongeza kuwa, kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Wizara na Taasisi pamoja na kupata mrejesho wa utendajikazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma.

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ameendelea kutoa wito kwa Watumishi wa Umma, Wananchi na Wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ili kupata huduma mbalimbali.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akimshukuru Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (kushoto) kwa kutembelea mabanda mbalimbali kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akizungumza na Maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati alipotembelea katika banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la TAKUKURU kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko (TPSC), Bw. Shakiru Abdulkarim alipotembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali zinazoelezea elimu juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za usafiri wa anga kutoka kwa Maafisa wa TCAA alipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ofisi yake wakati alipotembelea banda la ofisi hiyo kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.


Mwonekano wa baadhi ya mabanda mbalimbali ya Wizara na Taasisi za Umma yaliyopo Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma yanayotoa huduma katika Wiki ya Utumishi wa Umma.


Mwonekano wa baadhi ya mabanda mbalimbali ya Wizara na Taasisi za Umma yaliyopo Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma yanayotoa huduma katika Wiki ya Utumishi wa Umma.


 

Tuesday, June 17, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUTUMIA MIFUMO YA KIDIJITI KURAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI

Na Mwandishi Wetu - Dodoma 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha zinatumia mifumo katika kuwahudumia wananchi kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma bora, urahisi na haraka. 

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati wa akifungua Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye kaulimbiu ya "Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji" 

Amesema Serikali imejenga mifumo mingi ikiwemo wa kufuatilia utendaji kazi wa watumishi ambao umeondoa ubabaishaji.

Kadhalika, Waziri Simbachawene amewataka wananchi kutumia mfumo wa e-malalamiko na e-mrejesho ili kuweza kuainisha changamoto ambazo Serikali itazifanyia kazi kwa wakati na kuboresha utoaji wa huduma.

"Nizielekeze Taasisi zote za Umma kutumia mifumo iliyojengwa ili kurahisisha utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa urahisi."

Kwa upande wake Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma imeshirikisha Wizara 23, Mikoa 5, Halmashauri 3 na taasisi za umma 101 zimeshiriki.

Amesema kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Taasisi na Wizara kupata mrejesho ili kuboresha utoaji wa huduma.

Katika hatua nyingine, Bw. Mkomi ametoa wito kwa wananchi, watumishi wa umma na wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ambapo Maadhimisho hayo yataendelea hadi Juni 27 mwaka huu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Sehemu ya Wananchi na Watumishi wa Umma, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyeshika kipaza sauti) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene baada ya kuwasili katika banda la ofisi yake wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Wananchi na Watumishi mbalimbali walioshiriki kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta jambo na Katibu Mkuu wa ofisi yake Bw. Juma Mkomi wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyekaa kulia) akimsikiliza Afisa TEHAMA wa ofisi hiyo, Bw. Selemani Sultan alipokuwa akielezea huduma zinazotolewa kwa kutumia mifumo mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma. Aliyekaa kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kulia) akitazama namna ya kujisajili kwenye mfumo wa PSSSF alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa ofisi yake mara baada ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa kaunda suti nyeusi) akitazama moja ya kifaa cha moyo kwenye banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda hilo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Wizara na Taasisi mbalimbali mara baada ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Wasaidizi wa ofisi yake mara baada ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene (kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Bohari Kuu ya Dawa alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Kwaya ya TAKUKURU ikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.