Na. Lusungu Helela - SIMIYU
Amesema Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele
katika vita dhidi ya rushwa, uwekezaji wake wa fedha, rasilimaliwatu na
vitendea kazi ni utashi alionao kwa TAKUKURU ili iweze kufanya kazi yake kwa
ufanisi.
" Rushwa ni adui wa ustawi
wa jamii, rushwa inapofusha, TAKUKURU mpo kamateni vinara wa rushwa katika
maeneo hayo kwani wanajulikana kwa majina na vyeo vyao " amesisitiza
Mhe.Simbachawene.
Amesema katika bajeti ya mwaka
2024/ 2025 kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilitengwa kwa ajili ya
ujenzi wa majengo ya TAKUKURU nchini ikiwemo jengo hilo la TAKUKURU Mkoa
wa Simiyu.
Chalamila amesema ujenzi wa jengo
hilo utachagiza mapambano dhidi ya rushwa ambapo hapo mwanzo jengo walilokuwa
wamepanga lilikuwa kwenye makazi ya watu hali iliyopelekea hata wale
wananchi wenye taarifa fiche kuogopa kuja ofisini hapo kwa hofu ya kuonwa na
watu, " ila kwa ofisi hii naamini wananchi watakuwa huru kutuletea
taarifa bila hofu ya kuonwa na yeyote " amesisitiza Chalamila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na baadhi ya wananchi,
watumishi na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali wakati akizindua Jengo la
TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambalo limegharimu
kiasi cha Sh. Mil. 640 hadi kukamilika kwake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Chrispin Chalamila akizindua Jengo la TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 640 hadi kukamilika kwake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi mbalimbali alipowasili kwa ajili ya kuzindua Jengo la TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 640 hadi kukamilika kwake.
Baadhi ya wanachi, watumishi na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza kabla ya kuzindua Jengo la TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil.640 hadi kukamilika kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kwa ajili ya kuzindua Jengo la TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 640 hadi kukamilika kwake.
No comments:
Post a Comment