Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi
amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kujitathmini wanapotoa huduma za kiutumishi
kwa Watumishi wa Umma kutoka katika taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kwa
ujumla
Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake, ikiwa ni muendelezo
wa mafunzo
kwa watumishi hao ambayo hufanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.
“Ofisi yetu inatoa huduma mbalimbali za kiutumishi, ninawaasa
mjitathmini kwa namna mnavyotoa huduma kwa Watumishi wa
Umma, wadau na wananchi ili tupate mrejesho mzuri kutoka kwao na hatimaye
kufikia malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.” amesema Bw. Mkomi.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo Balozi
Mhe. Omar Kashera amewataka watumishi hao kutanguliza mbele uzalendo kwa
kujenga taswira nzuri ya ofisi hiyo huku akiwataka kufanya maamuzi sahihi pindi
wanapowahudumia wateja.
‘’Ili mtoe maamuzi sahihi ni vizuri mkafikiri kwa
kina,
muwashirikishe watumishi mnaofanya nao kazi ili kupata maamuzi jumuishi
yatakayokuwa sahihi kwa maslahi ya Taifa’’ ameongeza Balozi Mhe. Omar Kashera
Katibu
Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi
watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha
utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi
(aliyesimama kulia) akiteta jambo na Mwezeshaji wa
mafunzo Balozi Mhe. Omar Kashera
(aliyesimama kushoto) baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi,
Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini
Dodoma.
Mwezeshaji wa mafunzo Balozi Mhe. Omar Kashera
(aliyesimama) akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment