Na. Veronica Mwafisi na Eric Amani-Dodoma
Tarehe 04 Juni, 2025
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi ametoa wito kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara kuzingatia misingi na miiko ya Uongozi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi na Watumishi wa Umma.
Bw. Daudi ametoa wito huo leo wakati akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Serikali kwenye mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Jiji Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Daudi amesema, Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji viongozi lakini Ofisi ya Rais-UTUMISHI imeendelea kupokea malalamiko yanayokwamisha utendaji mzuri wa taasisi za umma jambo ambalo linasababishwa na kutozingatia misingi na miiko ya uongozi.
“Pamoja na serikali kufanya jitihada kubwa ya kuwajengea uwezo viongozi kiutendaji, bado ofisi yetu imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali ikiwemo uwepo wa makundi katika ofisi, kukosa utendaji wa pamoja, upendeleo katika kutoa huduma kwa wadau, kutowaendeleza watumishi, kutotenga bajeti kwa ajili ya kuandaa mipango ya mafunzo inayozingatia mahitaji ya Watumishi itakayoleta manufaa katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,” ameongeza Bw. Daudi.
Aidha, Bw. Daudi amewasisitiza Viongozi hao kuwajengea uwezo wa kiuongozi watumishi walio chini yao ili kuwa na mpango wa urithishanaji madaraka pindi kiongozi anapoondoka katika ofisi awepo mtu mahiri kutoka katika ofisi hiyo wa kushika nafasi hiyo.
Amesema masuala yote hayo yasipotekelezwa yanaenda kinyume na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza misingi ya utawala bora na maadili katika utumishi wa umma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amesema Idara anayoiongoza imekuwa ikitoa mafunzo kwa Viongozi na watumishi wa umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.
“Mafunzo ni suala endelevu, hivyo viongozi na watumishi wanapaswa kuendelezwa kwa kujengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ili wafahamu namna ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uongozi bora, maadili, akili hisia na kuufahamu utumishi wa umma.” Bi. Mavika amesisitiza.
Bi. Mavika ameongeza kuwa, mafunzo hayo ni muhimu katika kuendeleza rasilimaliwatu itakayoziwezesha Taasisi za Serikali kufikia malengo ya kuboresha utoaji wa huduma bora kwa ustawi wa taifa.
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia Idara ya
Uendelezaji Rasilimaliwatu imeandaa mafunzo hayo ya siku mbili kwa Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Xavier Daudi akizungumza na Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na
Wizara wakati akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao
kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Sehemu
ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa
na Wizara wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Uendelezaji
Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa lengo la kuwajengea uwezo Viongozi
hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akifungua
mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi
Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya
kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Xavier Daudi akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi na
Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara mara baada ya kufungua mafunzo
yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia
na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Leila Mavika akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) kufungua mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi.
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani)
akifungua mafunzo kwa Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na
Wizara yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi
hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli za kiutumishi.
Sehemu
ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa
na Wizara wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier
Daudi (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya
kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika
Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles
Mhina ambaye ni Mkufunzi akiwasilisha
mada kuhusu Uongozi wa Kimaadili kwenye mafunzo kwa Makatibu Tawala
Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara yaliyoandaliwa
na Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga
kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo
kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiwa katika picha ya
pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi
Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara mara baada ya kufungua mafunzo
yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia
na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika
Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiwa katika picha ya
pamoja na Wakurugenzi wa ofisi hiyo mara baada ya kufungua mafunzo kwa Makatibu
Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na
Wizara (hawapo pichani) yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye
mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli
za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma.
Sehemu ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika ukumbi wa Jiji Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Sehemu ya Wakurugenzi Wasaidizi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wizara wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo kwa viongozi hao yaliyolenga kuwajengea uwezo kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiwa katika picha ya
pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka
Sekretarieti za Mikoa na Wizara mara baada ya kufungua mafunzo yaliyolenga
kuwajengea uwezo Viongozi hao kwenye mabadiliko ya kifikra, kitabia na mtazamo
kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiutumishi yaliyofanyika Mtumba katika
ukumbi wa Jiji Dodoma.
No comments:
Post a Comment