Wednesday, February 15, 2017

SERIKALI YAWAPOKEA WATAALAM SITA WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOKUJA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Roxana Kijazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akipokea kalenda ya JICA ya mwaka 2017 toka kwa Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akipewa maelezo kuhusu kalenda ya JICA ya mwaka 2017 toka kwa Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akiwa katika picha ya pamoja  na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini  mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.  

Friday, February 10, 2017

SERIKALI YAZINDUA RASMI TOVUTI YA WATUMISHI (WATUMISHI PORTAL) KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA KWA WATUMISHI NCHINI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Ofisi ya Rais - UTUMISHI, Bw. Mathias Kabunduguru.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.

Baadhi ya watumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.

Baadhi ya watumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasisitiza watumishi wa umma nchini kutumia Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal)  alipokuwa akizindua Tovuti hiyo mkoani Dodoma leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa tayari kuzindua Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo. Kushoto kwake anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) wakifurahia uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifuatilia maelezo kuhusu Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) baada ya kuizindua rasmi mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi  Stella Manyanya (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.