Sunday, September 25, 2016

LIJUE GAZETI LA SERIKALI

GAZETI LA SERIKALI-sehemu iliyopita tuliona matumizi ya taarifa zinazochapishwa katika gazeti la serikali ikiwamo kufuatilia masuala mbalimbali ya kisheria, na aina ya taarifa hizo.
Leo tunaangalia lugha inayotumika katika Gazeti la Serikali, bila shaka umewahi kujiuliza kuhusu jambo hili. Lugha inayotumika katika taarifa za Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kanuni C. {2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la 2009 na Establishment Circular letter No. 7 ya mwaka 1970, taarifa zote zinatakiwa kuwa katika lugha ya Kiswahili isipokuwa taarifa zinazohusu matangazo ya Kisheria, kwa maana ya Miswada ya Bunge na matangazo ya Serikali, Government Notice, ambayo hutangazwa kwa lugha ya Kiingereza.

https://www.facebook.com/utumishiweek

Gazeti la Serikali hupatikana wapi?, itaendelea..

MHE. KAIRUKI AWATAKA WAAJIRI WOTE SERIKALINI KUHAKIKISHA KUWA WATUMISHI WALIO KATIKA MAMLAKA ZAO WANASAJILIWA KWA AJILI YA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA NDANI YA SIKU 14, NA KUWASILISHA TAARIFA YA ZOEZI HILO OFISI YA RAIS-UTUMISHI. SERIKALI IMEPANGA KUFANYA ZOEZI HILO LA USAJILI NA UTOAJI WA UTAMBULISHO NA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WATUMISHI WA UMMA WOTE KUANZA TAREHE 03 OKTOBA, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu  zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Mkurugezi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw. Mohammed Khamis akifafanua kuhusu zoezi la  Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Vyombo vya Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Mkurugezi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Mohammed Khamis akiwaonesha waandishi wa habari aina ya kitambulisho cha taifa kitakachotolewa na NIDA  wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Vyombo vya Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na vyombo vya Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Friday, September 23, 2016

SERIKALI YAWAAGA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA KUTOA HUDUMA NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mwandamizi wa JICA nchini Tanzania Bw. Takusaburo Kimura (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam watatu (3) wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma nchini, hafla hiyo iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.


Mtaalam wa kujitolea kutoka Japani aliyemaliza kutoa huduma nchini Bi. Shisho Saito (kulia) akieleza shughuli alizozifanya kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (kushoto) akipewa maelezo na Mratibu wa Wataalam wa kujitolea wa Ofisi ya JICA   nchini Tanzania  Bw. Owa Ichiro  juu ya  shughuli zilizofanywa na wataalam  wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma  nchini  wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam  wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma  nchini mara baada ya  hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao  iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.  Wengine ni Maafisa kutoka Ofisi ya Rais –Utumishi na JICA Tanzania.