Friday, September 23, 2016

SERIKALI YAWAAGA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA KUTOA HUDUMA NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mwandamizi wa JICA nchini Tanzania Bw. Takusaburo Kimura (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam watatu (3) wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma nchini, hafla hiyo iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.


Mtaalam wa kujitolea kutoka Japani aliyemaliza kutoa huduma nchini Bi. Shisho Saito (kulia) akieleza shughuli alizozifanya kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (kushoto) akipewa maelezo na Mratibu wa Wataalam wa kujitolea wa Ofisi ya JICA   nchini Tanzania  Bw. Owa Ichiro  juu ya  shughuli zilizofanywa na wataalam  wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma  nchini  wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Agnes Meena (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam  wa kujitolea waliomaliza kutoa huduma  nchini mara baada ya  hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao  iliyofanyika  Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-Utumishi.  Wengine ni Maafisa kutoka Ofisi ya Rais –Utumishi na JICA Tanzania.

No comments:

Post a Comment