Friday, June 24, 2016

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 , DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wakati wwa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathias B. Kabunduguru (kushoto) akijadili jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya Mkoa wa Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kariuki (Mb), na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia Watumishi wa Umma mkoani Dodoma.

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 -MATUKIO,-DODOMA. Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Nchi-Utumishi na Utawala Bora (hayupo pichani)

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 -MATUKIO,-DODOMA. Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Nchi-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) 

Thursday, June 23, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA:SIKU YA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 ,OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

Afisa Malalamiko wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. James Katubuka (kulia) akihudumia mteja katika Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma. 
Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 7 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan, Bi.Yuka ITO, akielezea namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. 
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika  ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Wednesday, June 22, 2016

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016, MKOANI MANYARA

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Eliakim Maswi akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dkt. Joel Bendera akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Watumishi wa Umma wa mkoa wa Manyara kuhusu hoja mbalimbali alizozipokea wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

Afisa Muuguzi Msaidizi, Mkoa wa Manyara,Bi. Josephine Mosha akiwasilisha maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akikabidhiwa ripoti kuhusu kero na maoni kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa (CWT)-Manyara Bw. Qambos Michael Sulle ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
 

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016:MATUKIO KATIKA PICHA MKOANI ARUSHA

Mwakilishi wa chama cha wafanyakazi akiuliza swali wakati wa kikao mkoani Arusha.
Watumishi waliohudhuria mkutano kazi wa Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 mkoani Arusha wakimsikiliza Waziri wa Nchi-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) hayupo pichani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa watendaji wa mkoa wa Arusha wakati wa kikao kazi cha Wiki ya Utumishi wa Umma 2016, mjini Arusha. 

Tuesday, June 21, 2016

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016 : MATUKIO KATIKA PICHA MKOANI KILIMANJARO

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa umma wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. 
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Menejimenti ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro. Mhe. Kairuki amesisitiza Maafisa Rasilimaliwatu wafanye kazi kwa weledi na watakaoshindwa hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro.

Friday, June 17, 2016

Katibu Mkuu-Utumishi afanya kikao na watumishi,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016

Mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi akiwasilisha maoni kuhusu Utumishi wa Umma katika kikao cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma yaliyoulizwa na watumishi wa ofisi yake katika kikao cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi.

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA VIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MKOA WA SINGIDA

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Sehemu ya Watumishi wa Umma mkoani Singida wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angellah Kairuki (Mb), (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2016, mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Utawala katika Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji akifafanua masuala yanayohusu Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi na Watumishi wa Umma mkoano Singida. Kikao hicho ni moja ya matukio ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea hadi Tarehe 23 Juni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akipokea Ripoti ya Utendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Singida kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho Dkt. Henry Mambo, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala wa TPSC Bw. Rajabu Mirambo na Mkurugenzi wa TPSC Tawi la Singida Bw. Ramadhani Marijani (kushoto mwisho)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani) katika siku ya kwanza ya Wiki yaUtumishi wa Umma mwaka 2016, mkoani Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Mathew Mtigumwe, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Saidi Amanzi

PICHA YA PAMOJA TPSC: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma naUtawala Bora, Mh. Angellah Kairuki (Mb) (wa pili kulia aliyekaa) katika picha ya pamoja na Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la mkoani Singida mara baada ya kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.

Waziri Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.

“Najua miongoni mwa watumishi wa umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka watumishi wenye tabia hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote wa ndani na nje ya taasisi.

Aidha, Mhe. Kairuki amewataka Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.

“Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta matokeo bora kwa taifa.

“Tuwewabunifu, tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliwasisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika kutekeleza hilo, Mhe. Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”


Kaulimbiu hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.

Thursday, June 16, 2016

Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora yaanza rasmi Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kusikiliza kero za watumishi wa umma na wananchi

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt.Laurean Ndumbaro (kushoto) akisikiliza matatizo/maoni kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi yake katika siku ya kwanza ya wiki ya Utumishi wa Umma 2016. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt.Laurean Ndumbaro (kushoto) akisikiliza matatizo/maoni kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi yake katika siku ya kwanza ya wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Baadhi ya wateja waliofika kuhudumiwa siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. Anayeelekeza (katikati) ni Afisa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Rehema Msemo.

Saturday, June 11, 2016

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) azungumza na vyombo vya habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 katika ukumbi wa Ofisi ya Rais- Utumishi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 katika ukumbi wa Ofisi ya Rais- Utumishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 katika ukumbi wa Ofisi ya Rais- Utumishi.