Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana serikalini
kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima
kwa wanaowahudumia.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.
“Najua
miongoni mwa watumishi wa umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao
wahuduma unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani
watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka
watumishi wenye tabia hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba
wa Huduma kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote
wa ndani na nje ya taasisi.
Aidha,
Mhe. Kairuki amewataka Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza
kero na changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
“Uzoefu
unaonyesha kuwa watumishi wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo
hapa basi huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa
ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi
la Singida na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao
kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta matokeo
bora kwa taifa.
“Tuwewabunifu,
tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu nyingine ili kuweza
kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliwasisitiza
watumishi hao kuwa na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti,
mafunzo na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.
Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka,
kwa mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji wanakutana
na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na kusikiliza kero zao na
kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
kutekeleza hilo, Mhe. Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na
watumishi wa mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
Kauli
Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni
“Uongozi
wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”
Kaulimbiu
hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika
Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha
Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki
za Wanawake.
No comments:
Post a Comment