Friday, March 29, 2019

MHE. MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA TaGLA KUWA WABUNIFU ILI KUWAVUTIA WATANZANIA KUPENDA KUTUMIA MAWASILIANO KWA NJIA YA VIDEO NA KUIPUNGUZIA SERIKALI GHARAMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo   wakishuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya, alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo na watumishi wa TaGLA wakishuhudia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video kwa kuunganishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Nairobi, Kenya.
Meneja TEHAMA wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Emmanuel Tessua akitoa ufafanuzi jinsi teknolojia inavyofanya kazi katika wakala huo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Thursday, March 28, 2019

MHE. MKUCHIKA AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI NA MAMA MARIA NYERERE IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), wa pili kushoto ni Mama Siti Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na watoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipomtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Andrew Nyerere na wa kwanza kushoto ni Magige Nyerere. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).

Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono, akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mkuchika ya kuwatembelea Viongozi Wastaafu wa Kitaifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiagana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).

Wednesday, March 27, 2019

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIPONGEZA OFISI YA RAIS - UTUMISHI KWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWA WAKATI KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akizungumza  na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo jipya  la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Saturday, March 23, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAANDIKA HISTORIA YA KUWA TAASISI YA KWANZA KUZINDUA HUDUMA ZAKE KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA













Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Mkuu-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro  wameshiriki tukio hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakifurahia uzinduzi wa ofisi yao iliyojengwa  kwenye mji wa serikali jijini Dodoma, mara baada ya Mhe. Mkuchika kuzindua ofisi hiyo.

Mwonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya TBA kulikabidhi jengo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa kwenye ofisi yake iliyopo kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma mara baada ya kuizindua.

Mkurugenzi wa Ujenzi, Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Hamphrey Kilo akiwasilisha taarifa ya ujenzi  wa jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) mara baada ya kumkadhi waziri huyo jengo hilo lililopo kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akimkabidhi hati ya kiwanja mtumishi wake Bi. Zena Makaye, mara baada ya waziri huyo kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akimkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi yake Bw. Peter Mhimba, mara baada ya waziri huyo kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi yake mbele ya ofisi aliyoizindua ambayo  imejengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma. Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Mkuu-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro  ni miongoni mwa waliojumuika katika picha hiyo.