Wednesday, March 20, 2019

DKT. MWANJELWA AWATAKA WAAJIRI SERIKALINI KUZINGATIA UBUNIFU KATIKA UJUMUISHWAJI WA MASUALA YA KIJINSIA SEHEMU ZA KAZI ILI KULETA TIJA KIUTENDAJI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya Kijinsia mahali pa kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Bi. Agnes Meena akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  (hayupo pichani) kufungua kikao kuhusu Ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi Idara wa Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta akitoa neno la shukrani katika kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Bi. Leila Mavika akiwasilisha mada katika kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.


No comments:

Post a Comment