Monday, August 31, 2026

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI AWATAKIA KHERI NA BARAKA WATUMISHI WALIOZALIWA MWEZI AGOSTI HUKU AKIWASISITIZA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA UFASAHA

Na Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 31 Agosti, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, ameungana na Menejimenti na Watumishi wa Ofisi hiyo kuwatakia kheri na baraka Watumishi waliozaliwa mwezi Agosti, katika kumbukizi ya siku zao za kuzaliwa huku akiwasisitiza kuwatumikia wananchi kwa ufasaha.

Bi. Lwangili ametoa pongezi hizo leo tarehe 31 Agosti, 2026 mara baada ya kuhitimisha mafunzo yaliyohusu Taratibu za Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu yaliyotolewa katika eneo maalumu la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba Jijini Dodoma

Ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watumishi hao kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kujituma, uadilifu na kuzingatia uwajibikaji katika utumishi.

Amewatakia Watumishi hao afya njema, furaha na mafanikio katika maisha yao, huku akiwahimiza kuendelea kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na nafasi ya kuwatumikia wananchi.

Aidha, amewaombea Mungu awabariki, awaongoze na awatimizie kila jambo jema alilolipanga kuwapa Mwenyezi Mungu katika maisha yao, huku akiwatakia maisha yenye amani, furaha, upendo na mafanikio.









NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI ASISITIZA UZINGATIAJI WA SHERIA KATIKA USHUGHULIKIAJI WA MASHAURI YA NIDHAMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Na Antonia Mbwambo – Dodoma

Tarehe 31 Agosti, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni katika kushughulikia mashauri ya nidhamu katika Utumishi wa Umma, akieleza kuwa uzingatiaji wa misingi hiyo ni muhimu katika kuhakikisha haki inatendeka.

Bi. Lwangili ameyasema hayo leo, tarehe 31 Agosti, 2026, wakati akihitimisha mafunzo ya uelewa kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

Bi. Lwangili amesema katika kushughulikia masuala ya nidhamu ni muhimu kuhakikisha kuwa thamani na utu wa mtu vinalindwa, huku hatua zote zikichukuliwa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizowekwa.

“Ni muhimu kuhakikisha kuwa katika kushughulikia mashauri ya nidhamu, Sheria, Taratibu na Kanuni zinafuatwa ili haki itendeke, huku tukilinda thamani na utu wa mtu, amesema Bi. Lwangili.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwakumbusha Watumishi wa Umma kuhusu madhara ya kutokuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao, akieleza kuwa uelewa huo utasaidia kupunguza makosa na kuwaepusha watumishi na changamoto ya kufikishwa katika mashauri ya kinidhamu.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni  Afisa Sheria Mwandamizi, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Edwin Bilikundi, amesema usimamizi wa nidhamu katika Utumishi wa Umma umejengwa katika dhana mbili kuu ambazo ni kurekebisha mwenendo wa Mtumishi (corrective measures) na utoaji wa adhabu (sanction approach). Amesema njia ya kurekebisha inalenga kumsaidia Mtumishi kutambua kosa na kujirekebisha, wakati utoaji wa adhabu hutumika pale kosa linapothibitika, hususan kwa makosa yanayojirudia au yenye uzito.

Bw. Bilikundi ameongeza kuwa mchakato wa kinidhamu unapaswa kuanza kwa uchunguzi wa awali unaolenga kubaini ukweli na uzito wa tuhuma, pamoja na kuamua hatua stahiki za kuchukua.

Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa hatua na muda uliowekwa katika Sheria, Kanuni na Taratibu ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa nidhamu unakuwa wa haki na wenye msingi sahihi wa kisheria.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) wakati Naibu Katibu Mkuu huyo akihitimisha mafunzo yaliyolenga kuwajengea Watumishi hao uelewa kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma, yaliyofanyika tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji leo tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Afisa Sheria Mwandamizi, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Edwin Bilikundi akiendesha mafunzo ya uelewa kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Ofisi hiyo leo tarehe 31 Agosti 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma Mtumba Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili  akisisitiza jambo wakati akihitimisha mafunzo ya kuwajengea Watumishi hao uelewa kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma, yaliyofanyika tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji leo tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji leo tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji leo tarehe 31 Agosti, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa pili kutoka kushoto) akifurahia jambo wakati alipokuwa akifuatilia mafunzo kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma leo Agosti 31, 2026 Mtumba Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma Mtumba Jijini Dodoma




 

Thursday, August 27, 2026

 WAZIRI KIKWETE: SOMALIA IMEKUJA KUJIFUNZA MAFANIKIO YA  MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIJITARI KATIKA UTUMISHI WA UMMA  NCHINI TANZANIA

 Na Lusungu Helela, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete, amesema uamuzi wa Serikali ya Somalia kumtuma Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma nchini Tanzania ni ishara ya kutambua mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika eneo la matumizi ya mifumo katika masuala ya Utumishi wa Umma nchini.

Kikwete amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na ujumbe wa Serikali ya Somalia unaoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Hirsi  Ganni, uliofika nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Amesema ujio wa ujumbe huo unaonyesha kuwa Somalia inatambua na kuthamini uzoefu wa Tanzania katika uendeshaji wa Serikali, utumishi wa umma na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Ukiona wenzako wanakufuata hasa katika eneo hili ambalo sisi ni watoa huduma, ni wazi kuwa huduma tunayotoa wapo wenzetu wanatambua na kuthamini tunachokifanya na ndiyo maana wameamua kuja kujifunza na kupata uzoefu,” amesema Mhe. Kikwete

Amesema anaamini uzoefu ambao Somalia itaupata kupitia ziara hiyo utasaidia kuboresha zaidi masuala ya utumishi wa umma nchini humo.

Mhe. Kikwete amesema ujumbe huo unapata fursa ya kujifunza maeneo mbalimbali, ikiwemo namna Serikali inavyohusiana na wananchi, uratibu wa masuala ya kazi na ajira, usalama wa wafanyakazi mahali pa kazi pamoja na mifumo ya pensheni kwa watumishi wanaostaafu katika taasisi za Serikali na sekta binafsi.

“Hii ziara ni kielelezo tosha kuwa Somalia imedhamiria, ndiyo maana haijaweza kutuma maafisa pekee, lakini Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ameamua kuja mwenyewe na timu yake kwa lengo la kujifunza na kuja kuona kwa macho yake kazi kubwa iliyofanyika Tanzania,” amesisitiza Mhe. Kikwete

Kwa upande wake, Mhe. Hirsi Ganni amesema ujumbe wake umefika Tanzania kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa katika masuala ya utumishi wa umma, hususan matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kuboresha utoaji wa huduma.

Amesema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi, huku watumishi wa umma wakitumia mifumo ya kidijitali kuwahudumia wananchi na kuhakikisha wanapata haki zao.

Mhe. Ganni amesema ujio wao ni muhimu kutokana na hatua ambazo Tanzania imepiga katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Amesema wamevutiwa pia na namna mifumo ya Serikali inavyowawezesha watumishi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Akizungumzia mfumo wa e-Mrejesho,  Mhe. Ganni amesema ni miongoni mwa mifumo waliyoona ina umuhimu katika kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, hivyo wanatarajia kujifunza namna unavyofanya kazi na uwezekano wa kutumia uzoefu huo katika kuboresha huduma nchini Somalia.

Ziara hiyo ya ujumbe wa Somalia inalenga pia kujifunza kuhusu mifumo ya Baraza la Mawaziri, usimamizi wa rasilimali watu, uajiri kwa kuzingatia sifa, Serikali mtandao, usimamizi wa ajira na mifumo ya taarifa za soko la ajira.

Ujumbe huo pia unatarajiwa kutembelea Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na Jiji la Serikali jijini Dodoma, kwa ajili ya kujionea namna shughuli za Serikali zinavyoratibiwa na kutekelezwa.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hirsi  Ganni,leo jijini Dodoma akioongoza  ujumbe wa Serikali ya Somalia, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete akimkabidhi zawadi ya mfano wa mlango ambao unapatikana Zanzibar Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hirsi  Ganni,leo jijini Dodoma mara baada ya kikao na ujumbe wa Serikali ya Somalia unaoongozwa na Waziri huyo, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete kuzungumza kwenye kikao na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hirsi  Ganni,leo jijini Dodoma akioongoza  ujumbe wa Serikali ya Somalia, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini


Baadhi ya Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi, Wataalamu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete kwenye kikao na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hirsi  Ganni,leo jijini Dodoma akioongoza  ujumbe wa Serikali ya Somalia, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hirsi  Ganni akizungumza kwenye kikao,leo jijini Dodoma akioongoza  ujumbe wa Serikali ya Somalia, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete kufungua kikao hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma, Mhe.Hirsi Ganni,leo jijini Dodoma wakiwa pamoja na viongozi na wataalamu mbalimbali mara baada ya kikao cha  ujumbe wa Serikali ya Somalia, uliofika nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya mifumo ya kidigitali katika masuala ya utumishi wa umma nchini




Sunday, August 23, 2026

TUZO YA RAIS WA AWAMU YA KWANZA NA MBEBA MAONO WA TAIFA LA TANZANIA, HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Tuzo ya Rais wa Awamu ya Kwanza na mbeba maono wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kutambua mchango wake katika kuasisi na kuwa na maono ya ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

Imepokelewa kwa niaba yake na   Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili.

Tuzo hii ni ishara ya heshima na kutambua mchango wake katika kuasisi maono ya Taifa ya kuwa ba umeme wa uhakika kwa maendeleo ya Tanzania.



TUZO YA RAIS WA AWAMU YA TATU, HAYATI BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Tuzo ya Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa, kwa kutambua, mchango wake katika kuhakikisha utekelezaji wake wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

Imepokelewa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili.

Tuzo hii ni ishara ya heshima na kutambua mchango wake katika kutimiza maono ya Taifa ya kuwa na umeme wa uhakika kwa maendeleo ya Tanzania.



Friday, August 21, 2026

WAZIRI KIKWETE: SERIKALI YAONGEZA TAASISI ZINAZOKAGULIWA KUHUSU UZINGATIAJI WA SHERIA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ILI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI

Na Lusungu Helela, Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema Serikali imeongeza idadi ya taasisi zitakazokaguliwa kuhusu uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa utumishi wa umma kutoka 160 mwaka 2025/26 hadi 300 mwaka 2026/27

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa, Agosti 21, 2026, mkoani Morogoro, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, mara baada ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha uadilifu, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amesema ukaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 12(1)(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298, Marejeo ya Mwaka 2023, kwa lengo la kufuatilia na kutathmini kiwango cha uzingatiaji wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika usimamizi wa masuala ya kiutumishi na kiutawala.

Kwa mujibu wa Mhe. Kikwete, ukaguzi huo utasaidia taasisi kubaini na kurekebisha kasoro za kiutendaji, kuimarisha uwajibikaji, kupunguza migogoro ya kiutumishi na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Ameongeza kuwa ukaguzi huo utaiwezesha Serikali kupata taarifa kuhusu hali ya utumishi wa umma nchini na kutoa mapendekezo ya kuboresha sera, sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kikwete amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili na wajibu wao, huku akiwaagiza waajiri kutoa motisha kwa wanaofanya vizuri na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wanaokiuka maadili ya utumishi.

Amesisitiza kuwa rasilimaliwatu ni msingi muhimu wa maendeleo kwa kuwa ndiyo inayosimamia rasilimali nyingine zote, hivyo inapaswa kusimamiwa kwa ufanisi.

Aidha, Mhe. Kikwete amesema Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kwa kuzingatia uwezo wa bajeti, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola, ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha Tume kuendelea kuimarisha shughuli zake, ikiwemo matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutekeleza majukumu ya ukaguzi.

Amesema matumizi ya teknolojia yamerahisisha kwa kiasi kikubwa kazi ya ukaguzi kwa kuwezesha ukusanyaji, uchambuzi na ufuatiliaji wa taarifa kwa ufanisi zaidi, hivyo kuongeza kasi na ubora wa utekelezaji wa majukumu ya Tume.

Awali, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda, amesema ukaguzi huo ni muhimu katika kubaini maeneo yenye changamoto na kusaidia waajiri kuchukua hatua za kuboresha usimamizi wa rasilimaliwatu. “Lengo ni kuhakikisha waajiri na watumishi wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,” amesema Kipanda.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ukaguzi linafanyika katika mikoa 16 na linatekelezwa na wataalamu wa Tume hiyo anayoiongoza.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Bw. Emmanuel Mkongo, amesema halmashauri hiyo itaendelea kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Umma kuhakikisha usimamizi wa utumishi unazingatia Sheria na Kanuni zilizopo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  mara baada ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi viongozi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na vingozi wa  Tume ya Utumishi wa Umma, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa ajili ya kuzungumza  na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwenye uzinduzi wa zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda akizungumza kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete  kuzungumza  na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwenye uzinduzi wa zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo,


Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakimsililiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati  akizungumza nao mara baada ya kuzindua zoezi la ukaguzi katika halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.


 

 

 

 

 

 

 

 

WAZIRI KIKWETE AISISITIZA TAKUKURU KUJIRIDHISHA NA USHAHIDI WA KESI ZA WATUHUMIWA KABLA YA KUZIPELEKA MAHAKAMANI


Na Lusungu Helela, Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameisisitiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kujiridhisha na ushahidi wa kutosha kabla ya kufikisha kesi mahakamani ili kuepuka kuwapotezea watu muda, hasa pale ambapo mtuhumiwa huachiwa au kushinda kesi kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo  Alhamisi Juni 20, 2026, alipokuwa akizungumza na watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni TAKUKURU imeshindwa kufanikiwa kwenye baadhi ya kesi na hii sio kwamba inaonewa, yawezekana kuna sehemu katika ushahidi hawajajipanga vizuri.

“Nawaombeni sana Maafisa Uchunguzi wetu tujiridhishe, msitumike katika kuwapotezea watu muda, ni muhimu tukajiridhisha juu ya ushahidi wa kesi zetu na utayari wa kupeleka kesi Mahakamani. Haipendezi kesi kuendeshwa kwa zaidi ya miezi mitano, halafu mwisho mtuhumiwa ashinde kwa kukosekana kwa ushahidi wa kutosha,” amesema.

Ameongeza kuwa watumishi wa taasisi hiyo wanapaswa kuhakikisha haki inatendeka bila kumuonea haya mtu yeyote wala kupindisha Sheria, Taratibu na Kanuni katika kila hatua ya uchunguzi.

Aidha, ameipongeza Taasisi hiyo kwani pamoja na kutofanikiwa katika baadhi ya kesi kwa kukosa ushahidi lakini amewapongeza kwa kesi walizoshinda ambazo zilikuwa na ushahidi wa kutosha huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii.

Amesema takwimu za mwaka uliopita zinaonyesha TAKUKURU imeshinda zaidi ya asilimia 70 ya kesi za rushwa ilizofikisha mahakamani.

Awali , Mkurugenzi  Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin  Chalamila, amesema taasisi hiyo itaendelea kutanguliza uzalendo, weledi, uwajibikaji na haki katika kushughulikia kesi za rushwa na uhujumu uchumi.

Chalamila amesema TAKUKURU ina Kitengo cha Maadili ya Watumishi kinachoongozwa na Mkurugenzi na moja ya majukumu yake ya msingi ni kuchunguza watumishi wa taasisi hiyo ili kuhakikisha wanakuwa mfano bora kwa jamii.

“Tuna Kitengo cha Maadili ya Watumishi wa TAKUKURU na kinaongozwa na Mkurugenzi. Moja ya jukumu lake la msingi ni kuwachunguza watumishi ili tuwe mfano na kioo bora kwa jamii,” alisema


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, (katikati) akiwa ameongozana na viongozi wengine akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Usimamizi Miliki ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dkt. Emmanuel Kiabo kuhusiana na jengo la   Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya Watumishi wa TAKUKURU  wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, wakati akizungumza nao leo Mkoani wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongozi na  watumishi mara baada ya kuwasili katika  Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

 Mkurugenzi  Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, kuzungumza na watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Itumishi wa Umma na Utawala Bora, akipanda mti mara baada ya  kuzungumza na watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Itumishi wa Umma na Utawala Bora, akimwagilia  mti mara baada ya kuupanda katika Ofisi za  TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake na kusikiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

 

 

 

 

Karibu Tukuhudumie

 




Mpendwa Mteja Wetu, Mrejesho wako ni muhimu sana kwetu.

 





Monday, August 17, 2026

WATUMISHI WAPATIWA ELIMU KUHUSU HATI YA KUSAFIRI, NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI ASISITIZA UMUHIMU WA MAFUNZO YA MARA KWA MARA KUJENGA UTUMISHI WA UMMA WENYE WELEDI

 Na Eric Amani, Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amesisitiza umuhimu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi wa Umma, akieleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuongeza maarifa na ujuzi, kujenga uwezo na kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi.

Bi. Lwangili ameyasema hayo leo wakati akihitimisha mafunzo yaliyohusu uelewa na maarifa ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu hati ya kusafiri, ikiwemo taratibu za kuomba, kupata na kutumia hati hiyo kwa usahihi yaliyofanyika leo Agosti 17, 2026, katika eneo la wazi la Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, Naibu Katibu Mkuu Lwangili amesema kuwa kuendelea kuwawezesha watumishi kupata elimu na ujuzi katika maeneo mbalimbali ni sehemu ya juhudi za Serikali za kujenga Utumishi wa Umma wenye weledi, ufanisi na unaozingatia viwango vya ubora katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji, Bw. Segere Zonzo, amewakumbusha watumishi umuhimu wa kuwa na uelewa sahihi wa taratibu za kupata na kutumia hati ya kusafiri.

Bw. Zonzo amesema kuwa uelewa huo utawawezesha watumishi kuzingatia taratibu na kutumia hati hiyo kwa usahihi, hivyo kurahisisha safari zao za nje ya nchi, hususan wanaposafiri kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kikazi au shughuli binafsi.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utaratibu wa Ofisi ya Rais – Utumishi wa kuwawezesha watumishi kuendelea kujifunza na kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Utumishi wa Umma, sambamba na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Prisca Lwangili akizingumza na watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) mara baada ya mafunzo ya kuongeza uwezo yanayofanyika kila jumatatu katika ukimbi wa ofisi hiyo, Agosti 17, 2026


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw. Baraka Manono akizingumza na watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) kabla kuanza kwa mafunzo ya kuongeza uwezo yanayofanyika kila jumatatu katika ukimbi wa ofisi hiyo, Agosti 17, 2026


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Prisca Lwangili akiwa na Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi wakipata elimu juu ya hati ua kusafiri Agosti 17, 2026.


Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakipatiwa elimu kuhusu hati ya kusafiri kutoka kwa Afisa wa Idara ya uhamiaji Mrakibu Msaidizi Bw. Segere Zonzo (Hayupo pichani) Agosti 17, 2026 katika ukumbi wa ofisi hiyo.



Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Bw. Monge Mnzava akitoa elimu kuhusu hati ya kusafiri kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa mafunzo ya kuongeza uwezo katika ofisi hiyo.


Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Bw. Segere Zonzo akitoa elimu kuhusu hati ya kusafiri kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa mafunzo ya kuongeza uwezo katika ofisi hiyo.