Na Eric Amani, Dodoma
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete amesisitiza wafugaji kuendelea kutumia mbinu bora za ufugaji katika
kuongeza thamani ya mifugo ili kukidhi matakwa ya soko la ushindani wa mifugo ndani
na nje ya nchi.
Mhe. Kikwete
amebainisha hayo leo tarehe 5 Agosti, 2026 wakati akifungua Paredi ya Mifugo
katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima maarufu kama Nanenane yanayoendelea
katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela Jijini Dodoma.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa paredi hiyo, Mhe. Kikwete alisema kuwa sekta ya mifugo
ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa kupitia uzalishaji, biashara
na ajira. Hivyo, hatuna budi kuongeza juhudi na jitihada za kuimarisha mbinu za
ufugaji bora kwa maslahi ya taifa.
Vile
vile, Mhe. Kikwete aliwataka wadau wa sekta ya mifugo kuendelea kushirikiana na
Serikali katika utekelezaji wa sera na programu mbalimbali zinazolenga
kuboresha huduma za ugani, udhibiti wa magonjwa ya mifugo na kuimarisha
miundombinu ya masoko.
“Nitumie fursa kuwahamasisha wafugaji wote nchini
kubadilisha mtazamo wa ufugaji wa kimazoea kwenda ufugaji unaotumia sayansi,
takwimu na teknolojia na pia kushiriki na kuleta mifugo yao kwa
ajili ya gwaride na mashindano kwa mwaka ujao 2027” alisema Kikwete.
Aidha, Paredi hiyo ilihusisha maonesho ya aina
mbalimbali za mifugo ikiwemo ng'ombe, mbuzi na mifugo mingine ambapo wafugaji
na taasisi mbalimbali walipata fursa ya kuonesha ubora wa mifugo yao pamoja na
teknolojia na ubunifu unaotumika katika kuendeleza sekta hiyo.
Waziri
Kikwete pia alitoa rai kwa taasisi za fedha nchini kuendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu na kubuni
huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wafugaji, hususan wanawake na vijana,
ili waweze kuwekeza katika sekta hii.
Pamoja na ufunguzi wa paredi ya mifugo, Mhe. Kikwete
amezindua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha Wizara ya Kilimo na Uvuvi
ambacho kitakuwa mahususi kwa ajili ya kutoa nakupokea taarifa za Kilimo na
Uvuvi.
![]() |
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete alipotembelea banda la Sekretariati ya Ajira katika maonesho
ya nanenane katika viwanja vya malecela vilivyopo Nzuguni Dodoma |







No comments:
Post a Comment