Monday, September 21, 2026

KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO WA KUPIMA AFYA ILI KUONGEZA TIJA, UFANISI NA UWAJIBIKAJI MAHALI PA KAZI

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 21 Septemba, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma kupima afya zao mara kwa mara ili kujijua na kuona namna bora ya kuishi kwa lengo la kuongeza tija, ufanisi na uwajibikaji mahali pa kazi kwa maslahi mapana ya nchi.

Bw. Mkomi ametoa wito huo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo mara baada ya madaktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), kutoa mafunzo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi.

“Kupima afya mara kwa mara kunasaidia kujikinga na mambo mengi ikiwemo kubadilisha mtindo wa maisha, hivyo ni muhimu Watumishi wa Umma tukajenga utamaduni wa kuangalia afya zetu bila kulazimishwa,” amesisitiza Katibu Mkuu Mkomi.

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi amewahimiza watumishi hao kwenda kwa wakati katika maeneo maalum ya ofisi hiyo yaliyotengwa kwa ajili ya kupima afya na kutoa ushirikiano kwa wataalam wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) waliofika kutoa huduma hiyo.  

Awali, Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Mkubwa Suleiman alisema ni muhimu watumishi hao wakazingatia mazoezi na mlo kamili utakaowafanya kuwa na afya bora ambayo ni nguzo muhimu kwa kila mtu.

Kwa upande wake, Daktari Adam Hussein pia kutoka katika Taasisi hiyo alisema, Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wana majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua afya yake ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananchi wakiwa na utimamu wa afya.

Wataalam hao wamelenga kutoa huduma mbalimbali kwa watumishi wa ofisi hiyo ikiwemo huduma ya mifupa, mgongo, mishipa ya fahamu, magonjwa ya ndani pamoja na mazoezi ya tiba na lishe.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokuwa akihitimisha mafunzo yaliyolenga kuwajengea Watumishi hao uelewa kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma. Waliopo mstari wa mbele ni Watumishi kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI).


Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Adam Hussein akisisitiza jambo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na taasisi hiyo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wapili kutoka kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, wa ofisi hiyo, Bi. Nyasinde Mukono (wakwanza kushoto) wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika katika ofisi hiyo leo tarehe 21 Septemba, 2026 Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Nyasinde Mukono akizungumza jambo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kuzungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Mkubwa Suleiman akisisitiza jambo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na taasisi hiyo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

 



Friday, September 18, 2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA UTUNZAJI WA MIRADI YA TASAF

Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu – Geita

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amesisitiza umuhimu wa kutunzwa na kutumiwa ipasavyo miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili iweze kutoa huduma endelevu na kunufaisha wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia TASAF katika Mkoa wa Geita, ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Fazilibucha, iliyopo Kata ya Bombambili, Manispaa ya Geita.

Aidha, Mhe. Qwaray ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) pamoja na jengo la Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Zahanati ya Kakora, iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Qwaray amesema kuwa uwekezaji unaofanywa na Serikali kupitia TASAF ni kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi, hivyo ni wajibu wa viongozi na Wananchi kuhakikisha miradi hiyo inatunzwa na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Miradi hii ni mali ya wananchi na imejengwa kwa lengo la kuwapatia huduma bora na endelevu. Ni muhimu kuhakikisha inatunzwa vizuri, inatumika ipasavyo na kila mmoja anawajibika kulinda uwekezaji huu ili uweze kunufaisha jamii.”Mhe. Qwaray amesema.

Ameongeza kuwa utunzaji wa miundombinu hiyo utasaidia kuongeza muda wa matumizi ya majengo na kuhakikisha Wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za kijamii bila kulazimika kutumia rasilimali nyingi katika ukarabati wa mara kwa mara.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati, inazingatia viwango vinavyohitajika na inatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.


Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Grace Kingalame, akitoa neno la utangulizi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kabla ya Naibu Waziri huyo kukagua mradi wa maendeleo unayotekelezwa na TASAF Mkoani Geita

Wananchi na wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kushoto) akikagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Zahanati iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.



Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.


Muonekano wa mbele wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Zahanati ya Kakora, iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na viongozi na wananchi wa, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya kuwasili katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kakora unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii  (TASAF) Septemba 17, 2026 .


Thursday, September 17, 2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ATOA MAELEKEZO KUZINGATIA ANUAI ZA JAMII KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu- Nyang’hwale -Geita

Tarehe 17 Septemba, 2026.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi unazingatia anuai za jamii na mahitaji ya makundi mbalimbali bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa.

Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo leo, Septemba 17, 2026, wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoani Geita, katika ziara yenye lengo la kutembelea miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za Watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.

Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa anuai za jamii unapaswa kuonekana katika utoaji wa huduma, usimamizi wa watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki za watumishi.

“Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu wahakikishe kuwa utoaji wa huduma, usimamizi wa Watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki unazingatia mahitaji na tofauti za makundi mbalimbali ya jamii, bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa,” amesema Mhe. Qwaray.

Aidha, Mhe. Qwaray amesema Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea na ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi katika Taasisi za Umma, na kuwataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana kikamilifu, kurekebisha mapungufu yatakayobainika na kutekeleza maelekezo ya Tume kwa wakati.

 “Kwa ujumla, tunahitaji Utumishi wa Umma unaowajibika, unaozingatia sheria, unaoheshimu haki na kuzingatia anuai za jamii, na unaotoa huduma kwa ufanisi, usawa na kwa wakati,” amesema Mhe. Qwaray.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale, Bi. Kaunga Amani, amemshukuru Mhe. Qwaray kwa kutembelea miradi ya maendeleo na kukutana na watumishi ili kusikiliza changamoto zao. Amesema Halmashauri imepokea maelekezo yaliyotolewa na itaendelea kuyatekeleza ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale (hawapo pichani) leo tarehe 17 Septemba 2026 wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa katika ziara iliyolenga kutembelea miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za Watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akisalimiana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika Ofisi hiyo katika ziara ya kikazi leo tarehe 17 Septemba, 2026 Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale katika ziara ya kikazi Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Husna Toni wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoani Geita

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Grace Kingalame akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) kuzungumza na Watumishi wa Wilaya hiyo Mkoani Geita.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa shule wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi katika ziara yake ya kikazi Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiagana na Watumishi na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhiytimisha ziara ya kikazi leo tarehe 17 Septemba, 2026 Mkoani Geita

Mtumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale akiuliza swali kwa Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akipokea changamoto mbalimbali kutoka kwa Watumishi hao Septemba 17, 2026 Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nyang'hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi leo tarehe 17 Septemba, 2026 Mkoani Geita


Watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Geita


 


Wednesday, September 16, 2026

KATIBU MKUU MKOMI AWASISITIZIA MAADILI, NIDHAMU, MSHIKAMANO UTUMISHI SC

 Na Eric Amani, Dodoma

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi, Bw. Juma Mkomi, amewaaga na kuwatakia kila la kheri wanamichezo wa Utumishi Sports Club (UTUMISHI SC) wanaokwenda kuiwakilisha Ofisi katika Mashindano ya Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI 2026) yanayotarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa kuwaaga wanamichezo hao katika Ukumbi wa Ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Bw. Mkomi amewataka kwenda kushindana kwa kuzingatia nidhamu, mshikamano, heshima, na uadilifu, huku wakitambua kuwa wanapokuwa uwanjani wanawakilisha siyo tu UTUMISHI SC, bali pia Ofisi ya Rais – Utumishi.

“Nawatakia kila la kheri katika mashindano haya. Nendeni mkaiwakilishe Ofisi yetu kwa vizuri. Ushindi ni muhimu, lakini zaidi ya yote tunataka kuona mnakuwa mabalozi wazuri wa Utumishi wa Umma,” amesema Bw. Mkomi.

Aidha, amewapongeza wanamichezo na viongozi wa UTUMISHI SC kwa juhudi na maandalizi waliyofanya kuelekea mashindano hayo. UTUMISHI SC imeendelea kufanya maandalizi kupitia michezo ya kirafiki, ikiwemo ushindi wa mabao 4–0 dhidi ya Mkonze Veterans katika mchezo uliofanyika Septemba 5, 2026 jijini Dodoma.

UTUMISHI SC inaingia katika mashindano hayo ikiwa na dhamira ya kufanya vizuri, baada ya kutwaa ubingwa wa SHIMIWI mwaka 2025 yaliyofanyika jijini Mwanza.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, akiwaaga na kuwatakia kila la kheri wanamichezo wa Utumishi Sports Club 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, akiwaaga na kuwatakia kila la kheri wanamichezo wa Utumishi Sports Club 

Baadhi ya wanamichezo wa Utumishi SC wakimsikiliza Katibu Mkuu Bw. Juma Mkomi (Hayupo pichani) wakati wanamichezo hao wakiagwa na kutakiwa kila la Kheri kwenye ushiriki wa mashindano ya SHIMIWI 2026


Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Juma Mkomi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Prisca Lwangili pamoja na wanamichezo wa mpira wa pete wakati wa kuwaaga kuelekea mashindano ya SHIMIWI 2026 Mkoani Kilimanjaro


Picha ya pamoja ya wanamichezo wa mchezo wa Soka kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa kuwaaga kuelekea mashindano ya SHIMIWI 2026 Mkoani Kilimanjaro


Picha ya pamoja ya Uongozi wa UTUMISHI SC wakiwa na Katibu Mkuu Bw. Juma Mkomi Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa kuwaaga kuelekea mashindano ya SHIMIWI 2026 Mkoani Kilimanjaro


Picha ya pamoja ya wanamichezo wa michezo ya Jadi kutokea Ofisi ya Rais - UTUMISHI



MHE.QWARAY AWATAKA WATUMISHI KUKUMBATIA MIFUMO YA KIDIJITI

Na. Antonia Mbwambo na  Lusungu Helela

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka watumishi wa umma nchini kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2026  wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri za Manispaa na  Wilaya ya Geita  mkoani Geita   kwa lengo la  kusikiliza changamoto za watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji katika Utumishi wa Umma

Amesema matumizi sahihi ya teknolojia ya TEHAMA ni muhimu katika kuongeza kasi ya utendaji na uwajibikaji katika utumishi wa umma na itasaidia kuchagiza jitihada za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Wajibu wetu wa kwanza chini ya Dira hii mpya ni kuongeza kasi ya utendaji, kukumbatia kikamilifu mifumo ya kidijiti ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa wakati na bila usumbufu,” alisema.

Aidha, alibainisha kuwa mfumo wa e-Watumishi na Watumishi Portal inawezesha watumishi kupata huduma mbalimbali za kiutumishi kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na taarifa za mishahara, likizo na uhamisho. Hivyo, amewataka kuitumia kwa makini.

Aliongeza kwa kuwataka watumishi kuhimiza wananchi kutumia mfumo wa e-Mrejesho ambao unatoa fursa kwa wananchi na watumishi kuwasilisha maoni, pongezi, malalamiko na mapendekezo kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali.

“Matumizi ya mifumo hii yanapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji, weledi na uadilifu kwa kuwa teknolojia ni nyenzo ya kurahisisha utendaji, lakini mafanikio yake yanategemea namna viongozi na watumishi wanavyoitumia,” amesema.

Vile vile, alisisitiza matumizi ya mfumo wa GSD ambao unaweka taarifa za huduma za Serikali katika sehemu moja ya kidijitali na kuwawezesha wananchi, wafanyabiashara na wageni kupata taarifa kuhusu huduma, gharama, masharti na namna ya kuzipata huduma hizo kwa haraka.

Ziara ya Qwaray katika mikoa ya Mwanza na Geita  inalenga kusikiliza changamoto za watumishi wa umma na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na  watumishi wa  Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita  zilizopo  mkoani Geita  mara  baada ya kuwasili kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi

Baadhi ya watumishi wa  Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita  zilizopo mkoani Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray mara  baada ya kuwasili kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi

 



Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombat akizungumza na watumishi wa  Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita  zilizopo  mkoani Geita kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza nao na  kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi


Mtumishi wa Manispaa ya Geita Bw. Hamza Shabani  akizungumza  mbele ya Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akitoa changamoto yake ya utofauti ya mishahara ya watumishi waliosoma kozi moja na wakati huo huo wakiwa wameajiriwa mwaka mmoja.

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Oscar Maduhu akizungumza na watumishi wa  Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita  zilizopo  mkoani Geita kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza nao na  kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi

 



Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombati mara baada kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kuzitafutia ufumbuzi

 


Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na baadhi ya watumishi na wananchi  mara  baada ya kuwasili leo katika Ofisi ya Mkuu wa  mkoa wa Geita  kwa lengo la kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi

 

 

KIKAO KAZI

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI (DTP) UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA