Friday, September 18, 2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA UTUNZAJI WA MIRADI YA TASAF

Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu – Geita

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amesisitiza umuhimu wa kutunzwa na kutumiwa ipasavyo miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili iweze kutoa huduma endelevu na kunufaisha wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia TASAF katika Mkoa wa Geita, ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Fazilibucha, iliyopo Kata ya Bombambili, Manispaa ya Geita.

Aidha, Mhe. Qwaray ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) pamoja na jengo la Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Zahanati ya Kakora, iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Qwaray amesema kuwa uwekezaji unaofanywa na Serikali kupitia TASAF ni kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi, hivyo ni wajibu wa viongozi na Wananchi kuhakikisha miradi hiyo inatunzwa na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

“Miradi hii ni mali ya wananchi na imejengwa kwa lengo la kuwapatia huduma bora na endelevu. Ni muhimu kuhakikisha inatunzwa vizuri, inatumika ipasavyo na kila mmoja anawajibika kulinda uwekezaji huu ili uweze kunufaisha jamii.” – Mhe. Qwaray amesema.

Ameongeza kuwa utunzaji wa miundombinu hiyo utasaidia kuongeza muda wa matumizi ya majengo na kuhakikisha Wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za kijamii bila kulazimika kutumia rasilimali nyingi katika ukarabati wa mara kwa mara.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati, inazingatia viwango vinavyohitajika na inatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Grace Kingalame, akitoa neno la utangulizi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kabla ya Naibu Waziri huyo kukagua mradi wa maendeleo unayotekelezwa na TASAF Mkoani Geita

Wananchi na wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Mkoani Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kushoto) akikagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Zahanati iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu vyumba vinavyotumika kutolea huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Kakora, wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Muonekano wa mbele wa jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Zahanati ya Kakora, iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita

Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na viongozi na wananchi wa, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya kuwasili katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kakora unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii  (TASAF) Septemba 17, 2026 .

No comments:

Post a Comment