Na. Antonia Mbwambo na Lusungu Helela
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka watumishi wa umma nchini kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mhe. Qwaray ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Geita mkoani Geita kwa lengo la kusikiliza changamoto za watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji katika Utumishi wa Umma
Amesema matumizi sahihi ya teknolojia ya TEHAMA ni muhimu katika kuongeza kasi ya utendaji na uwajibikaji katika utumishi wa umma na itasaidia kuchagiza jitihada za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
“Wajibu wetu wa kwanza chini ya Dira hii mpya ni kuongeza kasi ya utendaji, kukumbatia kikamilifu mifumo ya kidijiti ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa wakati na bila usumbufu,” alisema.
Aidha, alibainisha kuwa mfumo wa e-Watumishi na Watumishi Portal inawezesha watumishi kupata huduma mbalimbali za kiutumishi kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na taarifa za mishahara, likizo na uhamisho. Hivyo, amewataka kuitumia kwa makini.
Aliongeza kwa kuwataka watumishi kuhimiza wananchi kutumia mfumo wa e-Mrejesho ambao unatoa fursa kwa wananchi na watumishi kuwasilisha maoni, pongezi, malalamiko na mapendekezo kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali.
“Matumizi ya mifumo hii yanapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji, weledi na uadilifu kwa kuwa teknolojia ni nyenzo ya kurahisisha utendaji, lakini mafanikio yake yanategemea namna viongozi na watumishi wanavyoitumia,” amesema.
Vile vile, alisisitiza matumizi ya mfumo wa GSD ambao unaweka taarifa za huduma za Serikali katika sehemu moja ya kidijitali na kuwawezesha wananchi, wafanyabiashara na wageni kupata taarifa kuhusu huduma, gharama, masharti na namna ya kuzipata huduma hizo kwa haraka.
Ziara ya Qwaray katika mikoa ya Mwanza na Geita inalenga kusikiliza changamoto za watumishi wa umma na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita zilizopo mkoani Geita mara baada ya kuwasili kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuziBaadhi ya watumishi wa Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita zilizopo mkoani Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray mara baada ya kuwasili kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombat akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita zilizopo mkoani Geita kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza nao na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Oscar Maduhu akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Manispaa na wilaya ya Geita zilizopo mkoani Geita kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza nao na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombati mara baada kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kuzitafutia ufumbuzi
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na baadhi ya watumishi na wananchi mara baada ya kuwasili leo katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita kwa lengo la kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi








No comments:
Post a Comment