Saturday, May 28, 2022

WASIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SERIKALINI MNALO JUKUMU LA KUONDOA UTAMADUNI WA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA - Mhe. Ndejembi

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 28 Mei, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kuhakikisha wanaondoa utamaduni wa baadhi ya Watumishi wa Umma kufanya kazi kwa mazoea ili wananchi wapate huduma bora katika taasisi zote za umma nchini.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo jijini Dodoma, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa kufunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini.

Mhe. Ndejembi amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeweka mipango mizuri katika Utumishi wa Umma lakini kama baadhi ya watumishi wataendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea ni wazi kuwa Serikali haitoweza kutimiza lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi. 

“Ninyi wasimamizi wa Rasilimaliwatu ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia Serikali kubadili utamaduni wa kufanya kazi wa mazoea katika taasisi zenu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza. 

Ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akieleza azma ya Serikali yake ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye kuwajibika bila kushurutishwa, hivyo amewataka wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuondoa utendaji kazi wa mazoea katika maeneo yao ya kazi ili kumsaidia Mhe. Rais kutimiza azma yake. 

Akizungumza na washiriki wa kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewaeleza wasimamizi hao wa raslimaliwatu serikalini kuwa, wajibu wao ni kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025. 

Waziri Bashungwa amesema wasimamizi hao wa rasilimaliwatu wamejifunza mengi katika kikao kazi hicho, hivyo ametaka kuiishi kwa vitendo kaulimbiu ya kikao kazi hicho inayosema “UTUMISHI WA UMMA WENYE UADILIFU, NIDHAMU, UBUNIFU, WELEDI NA UWAJIBIKAJI WA HIARI KWA USTAWI WA TAIFA”. 

Mhe. Bashungwa amewakumbusha wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuwa, wao ndio mameneja wa rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma hivyo hakuna namna yoyote ambayo kaulimbiu hiyo itatekelezwa ipasavyo bila mchango wao wa kiutendaji. 

Kikao Kazi hicho cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu chenye lengo la kuboresha utendaji kazi Serikalini kiliandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa (hayupo pichani) alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao kilichofanyika jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi atoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akielezea namna kikao cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilivyofanyika kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akiteta na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi  kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akitunuku tuzo kwa mwakilishi wa taasisi ya serikali kwa kutambua utendaji kazi bora uliofanywa ka taasisi hiyo kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, ACP. Ibrahim Mahumi akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kuhusu usimamizi na matumizi ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara na Masilahi, Bibi Mariam Mwanilwa akiwasilisha mada kuhusiana na Miundo ya Maendeleo ya Utumishi wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


 

Thursday, May 26, 2022

OFISI YA RAIS UTUMISHI YAKUTANA NA WASIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUTATHMINI UTENDAJI KAZI

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 26 Mei, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake inafanya kikao kazi cha siku mbili na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili kutathmini utendaji kazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Jenista ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua kikao kazi hicho kilichanza leo jijini Dodoma.

Mhe. Jenista amesema ofisi yake imeamua kufanya kikao kazi hicho na watendaji hao kwani ndio wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu katika sekta zote za umma nchini kwa ajili ya ustawi wa taifa.

“Tukiongozwa na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, nimeona nikutane na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kwa mara ya kwanza ili kuweka msingi wa kutathmni utendaji kazi katika utumishi wa umma ambao utatuwezesha kujitathmini kwa lengo la kuongeza ufanisi kiutendaji.” Mhe. Jenista ameongeza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, ofisi yake inatarajia kufanya tathmni ili kupima utekelezaji wa malengo yaliyowekwa katika kikao kazi cha mwaka jana na kuweka malengo mapya yatakayotekelezwa katika mwaka wa fedha ujao kwenye eneo la utumishi wa umma.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, Mhe. Rais amefanya kazi kubwa ya kusimamia na kutoa haki na stahiki kwa watumishi wa umma, hivyo ofisi yangu inao wajibu wa kukutana na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu ili kuweka mkakati endelevu wa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma.

 “Tumeshuhudia Mhe. Rais amefanya mambo mengi mazuri kwa Watumishi wa Umma ikiwemo upandishaji wa madaraja, ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, kutoa ajira na kupandisha mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini, hivyo watumishi tumuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii bila kushurutishwa, weledi, uzalendo kwa taifa na kutoa huduma bora kwa wananchi,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Kikao kazi hicho kinaongozwa na kaulimbiu isemayo “Utumishi wa Umma wenye Uadilifu, Nidhamu, Ubunifu, Weledi na Uwajibikaji wa Hiari kwa Ustawi wa Taifa”



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao kilichoanza leo jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama  kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe akitoa salamu za Ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao kilichoanza leo jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa zawadi ya shukrani kwa mwakilishi wa PSSSF ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa shirika hilo katika kuwezesha kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Alex Mfungo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.



Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

 

TPSC IMEPEWA DHAMANA YA KUTOA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA KWA UMMA KUWANUFAISHA WATANZANIA - Mhe. Jenista

Na. James K. Mwanamyoto-Mbeya

Tarehe 25 Mei, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimepewa dhamana ya kutoa mafunzo yenye tija kwa Watumishi wa Umma na wanaotarajiwa kuhusu utoaji wa huduma bora kwa umma katika fani mbalimbali ili kuwanufaisha watanzania wengi walio kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Mhe. Jenista amesema hayo wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

Waziri Jenista amesema, kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Serikali inatarajia kuwa na wahitimu wenye weledi, ari, morali na bidii ya kulitumikia taifa ili kutoa mchango kwenye Utumishi wa Umma na hasa kwenye maendeleo taifa.

“Wahitimu wa TPSC mara nyingi wanakuwa wameiva kwenye eneo la uadilifu na weledi, hivyo anataraji watakuwa na mchango kwenye maendeleo ya taifa pamoja na kuwa viongozi na vinara wa uadilifu kwa Watumishi wa Umma na jamii inayowazunguka,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Aidha, Mhe. Jenista amesema kuwa, dhamana hiyo ya kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahitimu ili wawe na tija katika Utumishi wa Umma na maendeleo ya taifa ni lazima itekelezwe kwa vitendo na menejimenti pamoja na watumishi wote wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka amesema bodi yake ina imani kuwa, wahitimu wamepata mafunzo ya kutosha na wako tayari kulitumikia taifa kwa uadilifu, ujuzi na weledi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema, haiba ni jambo linalotarajiwa serikalini kutoka kwa wahitimu wa TPSC ambao watabahatika kuajiriwa na Serikali kwani itawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TPSC, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Emmanuel Shindika amesema chuo chake kinasheherekea Mahafali ya 35 yanayojumuisha wahitimu 1895 kutoka katika Kampasi zote 6 za Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Mbeya, Singida na Tanga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewatunuku vyeti wahitimu hao 1895 kwa ngazi ya Astashahada ya Awali, Astashahada na Stashahada katika fani za Menejimenti ya Kumbukumbu, Mafunzo ya Uhazili, Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Utawala wa Umma, Ununuzi na Ugavi pamoja na Utawala wa Serikali za Mitaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wahitimu wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

Wahitimu wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wahitimu hao kabla ya kuwatunuku vyeti wakati wa Mahafali ya 35 ya TPSC yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

 
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Florens Turuka akieleza jukumu la bodi yake, wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na wahitimu wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

 
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa taarifa ya utekelezaji wa chuo chake kwa Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiongoza maandamano ya kitaaluma ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 35 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho jijini Mbeya.