Tarehe 26 Mei, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake inafanya
kikao kazi cha siku mbili na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi
wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili kutathmini utendaji kazi kwa
lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mhe. Jenista
ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya
kufungua kikao kazi hicho kilichanza leo jijini Dodoma.
Mhe. Jenista amesema ofisi yake imeamua kufanya
kikao kazi hicho na watendaji hao kwani ndio wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu
katika sekta zote za umma nchini kwa ajili ya ustawi wa taifa.
“Tukiongozwa
na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, nimeona
nikutane na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kwa mara ya kwanza ili kuweka msingi wa kutathmni
utendaji kazi katika utumishi wa umma ambao utatuwezesha kujitathmini kwa lengo
la kuongeza ufanisi kiutendaji.” Mhe. Jenista ameongeza.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, ofisi yake inatarajia kufanya tathmni ili kupima utekelezaji wa malengo yaliyowekwa katika kikao kazi cha mwaka jana na kuweka malengo mapya yatakayotekelezwa katika mwaka wa fedha ujao kwenye eneo la utumishi wa umma.
Mhe.
Jenista ameongeza kuwa, Mhe. Rais amefanya kazi kubwa ya kusimamia na kutoa
haki na stahiki kwa watumishi wa umma, hivyo ofisi yangu inao wajibu wa
kukutana na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu ili kuweka mkakati endelevu wa
kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma.
“Tumeshuhudia Mhe. Rais amefanya mambo mengi mazuri kwa Watumishi wa Umma ikiwemo upandishaji wa madaraja, ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, kutoa ajira na kupandisha mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini, hivyo watumishi tumuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii bila kushurutishwa, weledi, uzalendo kwa taifa na kutoa huduma bora kwa wananchi,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Kikao kazi hicho kinaongozwa na kaulimbiu isemayo “Utumishi wa Umma wenye Uadilifu, Nidhamu, Ubunifu, Weledi na Uwajibikaji wa Hiari kwa Ustawi wa Taifa”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua
kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini
Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao
kilichoanza leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean
Ndumbaro akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara
na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza
leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe
akitoa salamu za Ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao
kilichoanza leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.
Alex Mfungo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine baada ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama kufungua kikao kazi cha siku mbili
cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment