Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma
Tarehe 21 Mei, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
amesema, Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha ofisi yake tangu
kianze kutoa huduma, kimewapunguzia gharama watumishi wa umma na wananchi waliokuwa
wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuatilia utekelezaji wa masuala yao ya
kiutumishi yaliyowasilishwa ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kufanyiwa
kazi.
Mhe. Jenista amesema hayo jijini Dodoma, alipofanya
ziara ya kikazi katika moja ya Idara yake ya Ukuzaji Maadili iliyoko Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM) ili kujionea namna Kituo cha Huduma kwa Mteja kinavyofanya
kazi.
Waziri Jenista amesema toka kituo hicho kianze kutoa
huduma rasmi imeonekana kuwa, kina faida kubwa katika kuwapunguzia gharama
watanzania wanaofualia masuala yao ya kiutumishi na wanaohitaji ufafanuzi wa
masuala yao ya kiutumishi katika ofisi yake.
“Watoa huduma katika kituo chetu wamekuwa wakipokea baadhi
ya hoja zinazoihusu ofisi yangu na nyingine nyingi zinahusu taasisi nyingine za
Serikali hivyo, ofisi yangu imekuwa ikitoa ufafanuzi na elimu kwa watanzania
ili wawasilishe hoja zao mahala sahihi,” Mhe. Jenista amefafanua.
Mhe. Jenista amesisitiza kuwa, kituo hicho kimeisaidia
ofisi yake kufuatilia mwenendo mzima wa hali na ustawi wa Utumishi wa Umma
nchini, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watumishi wa umma kuwa karibu na ofisi yake
iliyopewa dhamana ya kusimamia masuala ya kiutumishi na utawala bora.
Mhe. Jenista amefafanua kuwa, kituo hicho kinatoa
huduma siku za kazi kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa mbili na nusu hadi
saa kumi jioni.
“Ukitaka kupata huduma katika kituo chetu tumia
namba 0262 160 240 na kila atakayeipata namba hii ampatie na mwingine
ili ofisi yangu itoe huduma, ikiwa ni sehemu ya kuuunga mkono jitihada
za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,”
Mhe. Jenista amesisitiza.
Akizungumzia maadili ya watoa huduma wa kituo hicho,
Mhe. Jenista amesema watoa huduma wote wamepatiwa mafunzo ya maadili hivyo ni
waadilifu na wanatoa huduma kwa kuwajali wateja.
Aidha, Mhe. Jenista amepata fursa ya kutoa huduma
kwa watumishi wa umma waliopiga simu katika kituo hicho, hivyo kutatua
changamoto za kiutumishi zilizokuwa zikiwakabili watumishi hao.
Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiilianza kutoa huduma rasmi mwezi Juni, 2021.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya Watendaji wa ofisi yake (hawapo
pichani) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kutembelea Idara yake
ya Ukuzaji Maadili na kukagua utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) kilichopo katika ofisi zake
ziIlizoko UDOM Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bi. Leila Mavika akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Idara yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya
kikazi ya Mhe. Jenista katika Idara hiyo iliyolenga kukagua utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call
Centre).
Mkurugenzi wa Idara ya
Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bi. Leila Mavika akimuonyesha Kanuni za Maadili ya Utendaji katika
Utumishi wa Umma Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kukagua utendaji kazi wa Idara hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimhudumia mtumishi aliyepiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa
Mteja (Call Centre) alipowatembelea
watoa huduma wa kituo hicho kwa lengo la kujionea utendaji kazi wao. Wengine ni baadhi ya watendaji wa Ofisi
yake alioambatana nao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na Watendaji wa ofisi yake mara baada ya
kumhudumia Mtumishi aliyepiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha ofisi yake, alipokitembelea
kituo hicho ili kujionea utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia namna ambavyo mtoa
huduma wa kituo cha huduma kwa mteja (Call
Centre) wa Ofisi yake anavyotoa
huduma kwa mteja aliyepiga simu kwa ajili ya kupata huduma kwenye kituo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasili katika Ofisi yake iliyopo UDOM kwa lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili wa ofisi yake.
No comments:
Post a Comment