Saturday, May 28, 2022

WASIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SERIKALINI MNALO JUKUMU LA KUONDOA UTAMADUNI WA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA - Mhe. Ndejembi

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 28 Mei, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kuhakikisha wanaondoa utamaduni wa baadhi ya Watumishi wa Umma kufanya kazi kwa mazoea ili wananchi wapate huduma bora katika taasisi zote za umma nchini.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo jijini Dodoma, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa kufunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini.

Mhe. Ndejembi amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeweka mipango mizuri katika Utumishi wa Umma lakini kama baadhi ya watumishi wataendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea ni wazi kuwa Serikali haitoweza kutimiza lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi. 

“Ninyi wasimamizi wa Rasilimaliwatu ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia Serikali kubadili utamaduni wa kufanya kazi wa mazoea katika taasisi zenu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza. 

Ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akieleza azma ya Serikali yake ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye kuwajibika bila kushurutishwa, hivyo amewataka wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuondoa utendaji kazi wa mazoea katika maeneo yao ya kazi ili kumsaidia Mhe. Rais kutimiza azma yake. 

Akizungumza na washiriki wa kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewaeleza wasimamizi hao wa raslimaliwatu serikalini kuwa, wajibu wao ni kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025. 

Waziri Bashungwa amesema wasimamizi hao wa rasilimaliwatu wamejifunza mengi katika kikao kazi hicho, hivyo ametaka kuiishi kwa vitendo kaulimbiu ya kikao kazi hicho inayosema “UTUMISHI WA UMMA WENYE UADILIFU, NIDHAMU, UBUNIFU, WELEDI NA UWAJIBIKAJI WA HIARI KWA USTAWI WA TAIFA”. 

Mhe. Bashungwa amewakumbusha wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuwa, wao ndio mameneja wa rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma hivyo hakuna namna yoyote ambayo kaulimbiu hiyo itatekelezwa ipasavyo bila mchango wao wa kiutendaji. 

Kikao Kazi hicho cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu chenye lengo la kuboresha utendaji kazi Serikalini kiliandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa (hayupo pichani) alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao kilichofanyika jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi atoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akielezea namna kikao cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilivyofanyika kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akiteta na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi  kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akitunuku tuzo kwa mwakilishi wa taasisi ya serikali kwa kutambua utendaji kazi bora uliofanywa ka taasisi hiyo kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, ACP. Ibrahim Mahumi akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kuhusu usimamizi na matumizi ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara na Masilahi, Bibi Mariam Mwanilwa akiwasilisha mada kuhusiana na Miundo ya Maendeleo ya Utumishi wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.


 

No comments:

Post a Comment