Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma
Tarehe 17 Mei, 2022
Viongozi
wa dini mbalimbali nchini wameupongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kuridhia pendekezo la nyongeza ya mshahara
wa kima cha chini kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma.
Viongozi
hao wa dini wametoa pongezi hizo katika mjadala wa mtandaoni uliohusisha wadau
mbalimbali katika kutathmini ongezeko la mshahara kwa asilimia 23.3 na
maboresho ya masilahi ya watumishi wa umma yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya
Sita.
Askofu
wa Dayosisi ya Karagwe, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.
Benson Bagonza amempongeza Mhe. Rais kwa uamuzi huo muhimu ambao utajenga ari
ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma.
Askofu
Bagonza amesema dhamira ya Mhe. Rais ni ya kupongezwa na kuungwa mkono na Watanzania
wote kwani watumishi wa umma ni kiungo muhimu kwani wanatoa mchango katika
ujenzi wa uchumi wa Taifa.
“Dhamira
ya Mhe. Rais kulitazama suala la nyongeza ya mshahara inalenga moja kwa moja
kutekeleza dhamira yake ya kuhakikisha kwamba watumishi wanakuwa na ari ya
kujenga uchumi wa nchi na ustawi wa Taifa,” Askofu Bagonza amesisitiza.
Kwa upande wake, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Hemedi Jalala amesema ongezeko la mshahara na maboresho yaliyofanywa na Mhe. Rais katika utumishi wa umma yanadhihirisha namna serikali inavyowajali watumishi wake.
“Nina
imani kuwa ongezeko la mshahara la asilimia 23.3 na maboresho mengine
yaliyofanywa na serikali katika utumishi wa umma ni ishara ya upendo wa
Serikali kwa watumishi wake,” Sheikh Jalala ameongeza
Awali,
akieleza maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika utumishi wa
umma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema, azma ya Mhe. Rais ni kuhakikisha watumishi
wanafanya kazi kwa bidii, weledi, uzalendo na kujituma bila kushurutishwa na
ndio maana ametoa kipaumbele cha kuboresha masilahi ya watumishi.
“Kama
Mhe. Rais amejitoa kikamilifu kuboresha masilahi ya watumishi wa umma nasi
watumishi tunao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na uzalendo kwa ustawi wa
Taifa letu,” Mhe. Jenista amehimiza.
Mjadala
huo wa mtandaoni uliofanyika kwa zaidi ya saa mbili, uliandaliwa na Watch Tanzania News Agency na kuongozwa
na Bw. Omari Kibanga.
Picha
ya mtandaoni ikimuonyesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akishiriki mjadala
uliohusisha wadau mbalimbali katika kutathmini ongezeko la mshahara kwa
asilimia 23.3 na maboresho ya masilahi ya watumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment