Saturday, December 29, 2018

UJUMBE KUTOKA KWA DKT. LAUREAN NDUMBARO


UTUMISHI YAUNGA MKONO KWA VITENDO KAMPENI YA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU YA KULIFANYA JIJI LA DODOMA KUWA KIJANI KWA KUPANDA MITI



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan  mara baada ya watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kukamilisha zoezi la upandaji miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama akishiriki katika zoezi la upandaji miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akishiriki kuchimba mashimo kwa ajili  kupanda miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Baadhi ya  watumishi wa  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa tayari  kupanda miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma ili kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani,  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 21,2017.

Saturday, December 22, 2018

DKT. MWANJELWA AELEKEZA KUSIMAMISHA MISHAHARA YA WAAJIRI NA MAAFISA UTUMISHI WATAKAOWASILISHA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA (HCMIS)



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi  wa Idara ya Usimamizi wa Rasimali Watu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Ibrahim Mahumi (kushoto) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.